Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wa Uganda waliohujumu demokrasia

Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo vya usafiri dhidi ya maafisa wakuu wa serikali ya Uganda ambao wanaaminika kuhusika na njama ya kuhujumu mfumo wa demokrasia nchini Uganda.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Beckham aitaka Man Utd konyesha 'motisha'

    G

    Chanzo cha picha, Getty Images

    David Beckham amewataka wachezaji wa Manchester United kuthibitisha kuwa wana ari ya kuichezea klabu hiyo yenye matatizo.

    Nyota wa zamani wa United, Beckham alikuwa Manchester siku ya Alhamisi kuhudhuria onyesho la kwanza la filamu mpya kuhusu timu iliyoshinda mara tatu mwaka wa 1999.

    Beckham alikuwa mchezaji muhimu katika timu ya United ambayo ilishinda Ligi ya Premia, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA chini ya kocha mkuu Alex Ferguson .

    Meneja wa United Erik ten Hag anapambana kukwepa kufukuzwa huku timu yake ikilala katika nafasi ya nane kwenye Ligi ya Premia baada ya Jumatatu kupoteza kwa aibu 4-0 dhidi ya Crystal Palace.

    Beckham anaamini wachezaji lazima wachukue sehemu yao ya lawama, akisema: "Unatumai kwamba meneja hafai kufanya mengi. "Nadhani hiyo ndiyo maana kamili ya kuwa mchezaji wa Manchester United na kucheza katika michezo hii mikubwa - unapaswa kuwa na motisha."

    Msimu mgumu wa Ten Hag wa pili kuinoa unaweza kukombolewa ikiwa United watawashinda wapinzani wao Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA.

    Unapokuwa mchezaji wa kulipwa na unafanya kazi unayoipenda na uko kwenye klabu unayoipenda, unapocheza katika mchezo wowote, iwe ni mchezo wa kawaida wa msimu au ikiwa ni fainali ya Kombe la FA dhidi ya wapinzani wako, hiyo inapaswa kuwa motisha tosha," alisema.

  2. Marekani: Rubani atua kwa dharura baada ya sehemu ya ndege kudondoka

    Ndege ya abiria ilipoteza kipande cha kiunzi chake wakati ilipokuwa inapaa angani, jambo lililomlazimu rubani kutua kwa dharua katika uwanja wa ndege uliopo katika jimbo la Oregon, nchini Marekani, Ijumaa.

    Ndege hiyo aina ya Boeing 737 Max 9 inayomilikiwa na kampuni ya ndege ya Alaska , ilirejea jijini Portland, dakika 35 baada ya kupaa angani, kipande cha nje cha dirisha moja kilipodondoka.

    Kampuni hiyo ya ndege ya Alaska imesema kwamba abiria 177 na wahudumu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo, ‘walitua salama.’

    Aidha imesema kwamba itasitisha kwa muda safari za ndege zote 65 za aina ya 737 Max 9 ili kufanya ukaguzi wa kina.

    Kampuni ya kutengeza ndege ya Boeing imesema kwamba ina taarifa kamili kuhusu ajali iliyotokea Marekani na inajukumikia, ‘ukusanyaji wa taarifa zaidi.’

    Mamlaka ya safari za anga nchini Uingereza imeiambia BBC kwamba ina’angazia hali hiyo kwa karibu,’

    Ilipotangaza kusimamishwa kwa safari za ndege hizo 65, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya ndege ya Alaska Ben Minucucci alisema: ‘Kila ndege itarejeshwa katika shughuli za usafiri pindi tu itakapokamilisha kuchunguzwa wa kina na kupata huduma za kiufundi na pia kupita uchunguzi wa usalama.’

    Minucci, amepongeza juhudi za wafanyikazi sita waliokuwa kazini kwenye ndege hiyo, ambayo ilikuwa imepaa na kufikia umbali wa futi {not sure this is the right one to use} 16,000 juu ya ardhi, wakati ambapo ndege ilianza hatua ya dharura ya kushuka ardhini kwa ajili ya kutua , kulinga na takwimu za kuangazia safari za ndege.

    Mamlaka ya safari za ndege nchini Marekani FAA imethibitisha kwamba ndeeg hiyo ya kampuni ya ndege ya Alaska yenye nambari ya safari 1282 ‘ilirejea salama….baada ya wafanyikazi kuripoti tukio hilo la shinikizo la hewa,’

  3. Uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano Gaza unapungua-Qatar

    Wanajeshi wa Israel wameelekeza nguvu zao katika mji wa Khan Younis ulioko kusini mwa Gaza

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel wameelekeza nguvu zao katika mji wa Khan Younis ulioko kusini mwa Gaza

    Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza ni "yanapunguza uwezekano" wa kufikiwa kwa mapatano mapya ya kusitisha vita, waziri mkuu wa Qatar amesema.

    Akizungumza katika Kongamano la Doha, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema Qatar itaendeleza juhudi zake za kuzishinikiza pande zote mbili kusitishaji mapigano.

    Taifa hilo la Ghuba lilichukua jukumu muhimu katika mazungumzo ya kusitishwa kwa ghasia kwa wiki nzima mwishoni mwa Novemba, ambayo iliruhusu kuachiliwa kwa mateka.

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Jumapili "vita vinaendelea".

    Alisema katika siku za hivi karibuni "magaidi kadhaa wa Hamas" wamejisalimisha, na "wanaweka silaha zao chini na kujisalimisha kwa wapiganaji wetu mashujaa".

    "Huu ni mwanzo wa mwisho kwa Hamas," alisema.

    Kauli hizi zinakuja huku mzozo wa kibinadamu huko Gaza ukiendelea kuwa mbaya zaidi.

    Hapo jana, shirika la afya linaloendeshwa na Hamas huko Gaza lilisema karibu Wapalestina 18,000 sasa wameuawa.

    Katika ujumbe wa sauti kwa kituo cha habari cha Al Jazeera, mrengo wenye silaha wa Hamas ulisema usitishaji mapigano kwa muda "umethibitisha uaminifu wake" na kwamba hakuna mateka zaidi atakayeachiliwa hadi Israel ifanye mazungumzo.

  4. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatatu 11.12.2023

    Tunatumai umekuwa na wikendi njema. Ikiwa ndio mwanzo unajumuika nasi zifuatazo ni taarifa kuu kwa mukhtasari:

    • Wanadiplomasia katika Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kupiga kura nyingine kesho ya kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika ukanda wa Gaza.
    • Afisa mwandamizi wa wanamgambo wa Hamas akiionya Israel kuwa hakuna mateka hata mmoja ataachiwa hadi wafungwa zaidi wa Kipalestina watakapoachiwa na Israel
    • Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewataka Hamas kuweka chini silaha akiwaonya kuwa baada ya vita vikali vilivyodumu miezi miwili,mwisho wao uko karibu.
    • Rais wa Marekani Joe Biden amemualika mwenzake wa Ukraine Volodomyr Zelensky kuzuru Washington kesho Jumanne kujadili mahitaji ya Ukraine ya misaada ya dharura ya kijeshi na kifedha
    • Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema limeshtushwa na kusikitishwa na shambulizi la makusudi lililolenga msafara wa malori ya kubeba misaada ya kibinadamu katika mji mkuu wa Sudan,Khartoum.
  5. Ajenti wa FBI aliyefanyia Urusi upelelezi apatikana akiwa amefariki gerezani

    Ajenti wa Shirika la upepelelezi la Marekani FBI, aliyegeuka jasusi wa Urusi na mmoja wa majasusi hatari zaidi katika historia ya Marekani amepatikana akiwa amefariki gerezani.

    Robert Hanssen aligunduliwa katika kituo kilicho na ulinzi mkali huko Florence, Colorado, Jumatatu asubuhi.

    Hanssen, 79, alipokea zaidi ya dola milioni 1.4 taslimu, almasi, na pesa zilizolipwa katika akaunti za Urusi. Maajenti 300 walifanyia kazi kesi yake.

    Alihukumiwa kifungo cha maisha gerezanimwaka 2002 kwa kosa la ujasusi.

    Hanssen aliishi katika nyumba ya kawaida ya vyumba vinne katika kitongoji cha Virginia na mke wake na watoto sita kabla ya kukamatwa.

    Kwa sababu ya jukumu lake la kukabiliana na ujasusi, alipata habari za siri na mnamo 1985 alianza shughuli yake ya uhalifu, kutuma nyenzo kwa Urusi na iliyokuwa Muungano wa Sovieti.

    Hanssen, ambaye alikua afisa wa FBI mnamo 12 Januari 1976, alitumia jina la "Ramon Garcia" alipowasiliana na wahudumu wake.

    Kulingana na tovuti ya FBI, "alihatarisha vyanzo vingi vya kibinadamu, mbinu za kukabiliana na kijasusi, uchunguzi, nyaraka kadhaa za siri za serikali ya Marekani, na shughuli za kiufundi zenye umuhimu na thamani ya ajabu".

    Ijapokuwa shughuli zake za mara kwa mara zisizo za kwaida zilitiliwa shaka hakukamatwa kwa miaka kadhaa.

  6. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 06.06.2023.

  7. Tumefika tamati ya taarifa zetu za moja kwa moja, mpaka Jumatatu panapo majaaliwa

  8. Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wa Uganda waliohujumu demokrasia

    Antony Blinken is a veteran diplomat who's on home turf in the department

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken

    Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo vya usafiri dhidi ya maafisa wakuu wa serikali ya Uganda ambao wanaaminika kuhusika na njama ya kuhujumu mfumo wa demokrasia nchini Uganda, wakati wa uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata ulioandaliwa Januari tarehe 14 mwaka huu . Rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo na tume ya uchaguzi, matokeo ambayo yalipingwa vikali na mgombea mkuu wa upinzani wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi, al maarufu Boby Wine.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa marekani , Anthony Blinken

    Vitendo vya maafisa wakuu wa serikali ya uganda vilisambaratisha mchakato wa kidemokrasia nchini humo na ukiukwai wa haki za kibinadamu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Orodha ya maafisa waliowekewa vikwazo na Marekani hata hivyo haijatolewa lakini ripoti zilizotolewa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu zimeshutumu idara za usalama na ulinzi kwa kuhusika na mauaji, utekaji nyara na kukamatwa kwa wafuasi wa upinzani wakati wa msimu wa uchaguzi mkuu nchini Uganda

    Serikali ya Uganda imekanusha madai kuwa ilihusika na utekaji nyara wa wafuasi wa upinzani.

    lakini hapo jana ilikiri kuwa zaidi ya watu elfu moja walikamatwa wakati wa kipindi cha uchaguzi .

    Viongozi wa upinzani nchini Uganda wamedai kuwa zaidi ya watu 360 walitekwa nyara na maafisa wa ulinzi nyakati za usiku na hadi sasa hawajulikani waliko.

  9. Wahamiaji takribani 20 wafa maji pwani ya Tunisia

    Maelfu ya wahamiaji hujaribu kuvuka bahari ya Mediterania wakitoka nchi za Afrika kaskazini wakielekea Ulaya kila mwaka

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Walinzi wa pwani ya Tunisia wamesema wahamiaji karibu 20 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama.

    Wengine hawajulikani walipo, lakini shughuli za kuwatafuta zimesimamishwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

    Watu watatu pekee walipatikana wakiwa hai.

    Chombo hicho kilikuwa kimetoka mji wa Sfax nchini humo.

    Mara kwa mara umekuwa kikitumika kama kituo cha kuondokea wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya.

    Karibu watu 40 walizama kwenye tukio kama hilo nchini Tunisia mwezi uliopita.

  10. Wakamatwa kwa kosa la kula wakati wa mfungo wa Ramadhani Nigeria

    Kufunga kwa watu wazima ni suala la wajibu hasa kwa wale wenye uwezo wa kutokula na kunywa.

    Chanzo cha picha, AFP

    Watu wanane wamekamatwa na polisi wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria Kano kwa madai ya kukataa kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

    Polisi wa Hisbah wanasimamia sheria za Kiislam huko Kano - moja ya majimbo 12 ya Waislamu kaskazini mwa Nigeria wanaotumia mfumo wa sheria wa Sharia pamoja na sheria za kidunia za nchi hiyo.

    "Wahusika walikuwa wanawake watano na wanaume watatu, wakila alasiri katika mwezi wa Ramadhan," Aliyu Kibiya, Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Hisbah Jimbo la Kano alinukuliwa akisema.

    Kufunga kwa watu wazima ni suala la wajibu hasa kwa wale wenye uwezo wa kutokula na kunywa.

    Walio wagonjwa na wale ambao wanaweza kupata athari za kiafya iwapo watafunga kula na kunywa, wakiwemo watoto, wanawake wajawazito, wasafiri na wanawake wanaonyonyesha.

    Mwandishi wa BBC Khalifa Shehu Dokaji yuko Kano anasema wanawake hao waliiambia Hisbah kwamba walikuwa na msamaha kwa kuwa wako kwenye hedhi, lakini polisi waliwaambia pamoja na hali hiyo hawakupaswa kula hadharani.

    Ikiwa watashtakiwa mahakamani, wanaweza kulipishwa faini au kupelekwa kwa taasisi ya marekebisho ya tabia.

    Taarifa ya Bw Kibiya ilionya kuwa uvamizi zaidi utafanywa katika jimbo lote kuhakikisha watu wanazingatia wajibu wao wa kidini.

  11. Malimbikizo ya malipo ni sababu ya kuondoka kwa Sven Vandenbroeck simba?

    Kocha wa zamani wa Simba SC, Sven Vandenbroeck

    Ni miezi mitatu baada ya kuondoka kwenye klabu ya Simba SC, Sven Vandenbroeck ameishtaki klabu hiyo kwa Shirikisho la soka, Fifa kuwa anaidai kiasi cha dola za marekani 44,000 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ziada.

    Baada ya miezi kadhaa ya kuomba kupewa fedha hizo, Vandenbroeck ambaye sasa ni kocha wa klabu ya AS FAR ya Morocco, ameamua kulipeleka suala hilo kwa Fifa.

    Suala hilo liliripotiwa Fifa majuma matatu yaliyopita na chombo hicho kinachosimamia mchezo wa soka ulimwenguni kimethibitisha kuwa kinafanya uchunguzi kabla ya kufungua kesi.

    Chanzo cha habari kilicho karibu na Mbelgiji huyo kimesema kutopata malipo hayo ni sehemu ya sababu za yeye kuondoka katika klabu hiyo.

    Kuondoka kwake ghafla Simba kuliwaacha wafuatiliaji wa kandanda wa Tanzania na na mshtuko wakijiuliza kwa nini anaondoka baada ya kuwawezesha kufikia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu katika historia ya Tanzania.

    ‘’Kuna sababu nyingi , lakini hasa ni suala la malipo ya tangu msimu uliopita wa mwaka 2019/20. Simba iliahidi mara nyingi kulipa lakini haikufanya hivyo,’’ chanzo hicho kiliuambia mtandao wa PanAfrican Football.

    Jitihada za BBC kuupata uongozi wa klabu ya Simba kuzungumzia madai ya kocha huyo wa zamani zimegonga mwamba.

  12. Mauaji ya Indianapolis: Watu wanane wauawa kwa kupigwa risasi katika ghala la FedEx

    Watu wanane wameuawa

    Watua wanane wameuawa kwa kupigw arisasikatika jiji la Indianapolis ,polisi wamesema

    Walioshuhudia tukio hilo wanasema walisikia milio ya risasi katika kituo hicho cha FedExna mmoja alisema alimuona mwanamme aliyekuwa na bundukiya rashasha.

    Mwanamme huyo aliyejihami anadhaniwa alikuwa pekee yake na inaripotiwa alijiua .Mamlaka zinasema kwamba hakuna tishio jingine la usalama kwa umma .

    Polisi wamesema watu kadhaa waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini .Safari za ndege katika uwanja wa ndege ulio karibuhazijaathiriwa .

    Watu hao wanane walitangazwa kuaga dunia papo hapo.

  13. Pierre-Emerick Aubameyang: Mshambuliaji wa Arsenal atibiwa Malaria hospitalini

    Aubameyang came on as a substitute in the Europa League quarter-final first leg against Slavia Prague on 8 April

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ametibiwa hospitalini baada ya kuugua malaria wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa na Gabon.Mchezaji huyomwenye umri wa miaka 31 alifunga katika ushindi wao wamabao 3-0 wa Gabon dhidi ya DR Congo katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa bingwa Afrika mnamo Machi 25.

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

    Aliichezea Arsenal katika mchuao wao wa kombe la bara Uropadhidi ya Slavia Praguetarehe 8 Aprili lakini akosa mechi walioishinda Sheffield United Siku ya Jumapili

    " Nimekuwa hospitalini kwa siku chache wiki hii’ alisema kupitia Instagram

    " Ninahisi nauu kila siku kwa hisani ya madaktaru borawaliogunduana kunitibu haraka’

  14. Kampuni ya Lesotho yaruhusiwa kuuza bidhaa za bangi EU

    Bangi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.

    Kampuni yenye makao yake nchini Lesotho imeruhusiwa kukuuza mazao ya bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

    Kampuni hiyo kwa jina, MG Health, imesema Alhamisi kwamba imepokea uthibitisho rasmi kwamba mchakato wake wa utengenezaji unakidhi viwango vya uzalishaji vya Muungano wa Ulaya.

    Kampuni hiyo inakuwa ya kwanza barani Afrika kuuza bangi kwa ajili ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

    "Kile ambacho hii inamaanisha ni kwamba tuna idhini ya kuuza bidhaa zetu kama API [ kiungo cha kifamasia] ndani ya Ujerumani, na soko pana la Muungano wa Ulaya . Tunatarajia kuanza mwezi Juni ," Shirika la habari la Reuters lilimnukuu Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Andre Bothma akisema.

    Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.

  15. Rais wa Nigeria arejea nchini mwake baada ya ziara ya matibabu Uingereza

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea kutoka London, alikokuwa amesafiri kufanyiwa kimatibabu.

    Kurudi kwake siku ya Alhamisi kulitangazwa kupitia ujumbe wa akaunti ya Twitter ya serikali:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rais, ambaye alifanya ziara ya ‘kawaida ya matibabu’ kwenda Uingereza mnamo Machi 30, amekosolewa sana kwa kuamua kutibiwa nje ya nchi wakati mfumo wa huduma ya afya nchini mwake ‘ukisimamiwa vibaya na kukosa ufadhili wa kutosha’vyombo vya habari vya huko viliripoti,Nigeria pia inakabiliwa na ukosefu wa usalama, huku mashambulizi kadhaa yakiripotiwa wakati Rais Buhari alipokuwa hayupo

  16. Mrundi atuzwa medali ya dhabahu kwa kutengeneza pombe bora zaidi ya mwaka

    JOHN CHRIS KAVAKURE

    Chanzo cha picha, JOHN CHRIS KAVAKURE

    Maelezo ya picha, John Chris Kavakure anasema alifunzwa na nyanya yake kutengeza pombe

    Raia wa Burundi aamejipatia medali ya dhahabu baada ya kushinda tuzo la mtu aliyetengezeza pombe bora na tamu zaidi ya mwaka.

    John Chris Kavakure amejipatia ushindi huo baada ya pombe yake kwa jina Red Flo Bio kuzipiku kwa utamu pombe 3,100 zilizotengenezwa katika nchi 90 duniani.

    Shindano hilo linalofahamika kama Monde selection, linaloandaliwa na kampuni ya Ubelgiji ya viwango (International Quality Institute) hushindanisha utamu wa aina mbali mbali za pombe zenye kiwango cha kileo cha 7.5.

    JOHN CHRIS KAVAKURE

    Chanzo cha picha, JOHN CHRIS KAVAKURE

    John Chris Kavakure Mrundi ambaye pia ana uraia wa ubelgiji ameeleza kufurahishwa kwake na medali hiyo ambayo amesema inaonesha kuwa Waafrika kwa ujumla na Warundi wanaweza.

    Kavakure tayari amekwisha tengeneza aina 20 za pombe katika kiwanda chake cha pombe kinachofahamika kama Les Brasseries de Flobecq kilichopo nchini, chenye uwezo wa kutengeneza lita 30,000 kwa siku.

    KAVAKURE

    Chanzo cha picha, JOHN CHRIS KAVAKURE

    John Chris anasema alifundishwa kutengeneza pombe na bibi (nyanya)yake.

    "Bibi yangu ndiye aliyenifanya nipende kutengeneza pombe kwasababu nilikua nikiona anavyoitengeneza, anavyoweka mchanganyiko na mimi nafuata hivyo hivyo ."

  17. Karibu kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 16.04.2021