Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 16.04.2021: Haaland, Milenkovic, Mbappe, Nketia, Flick

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji hatari wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland
Iliyochapishwa

West Ham wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 21, mwishoni mwa msimu.

Manchester United wapo tayari kumsajili beki wa klabu ya Fiorentina na timu ya taifa ya Serbia Nikola Milenkovic, japo dau la usajili la beki huyo ni pauni milioni 38. (Sun)

mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah

Miamba ya soka ya Uhispania klabu za Barcelona na Real Madrid zinaweza kuangukia pua katika mbio za usajili wa mshambuliaji hatari wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 20. Mshambuliaji huyo anataka dau la Euro million 35 kwa mwaka, day amble Barca na Madrid hued wasilifikie. (Goal)

Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe

Paris St-Germain wanamshinikiza mshambuliaji wao tegemezi Kylian Mbappe, 22, kusaini mkataba mpya, japo Mfaransa huyo hataki mkataba huo uwe mrefu. (L'Equipe - in French)

West Ham wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 21, mwishoni mwa msimu. (Evening Standard)

Carlos Vinicius
Maelezo ya picha, Carlos Vinicius

Wolves watatupa karata yao katika mbio za usajili wa mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius, 26, mwishoni mwa msimu baada ya Tottenham kuamua kutompa mkataba mchezaji huyo ambaye yupo Spurs kwa mkopo. (TVI24 - in Portuguese)

Manchester United na Arsenal wanahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili kiungo kinda wa klabu ya Rennes, Mfaransa Eduardo Camavinga, 18, amble ameamua kutoongeza mkataba na klabu yake ya sasa. (Marca)

Manchester United wanataka beki wa Denmark Joachim Andersen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United wanamtaka beki wa Denmark Joachim Andersen

Manchester United wanataka beki wa Denmark Joachim Andersen, 24, ambaye anaichezea Fulham kwa mkopo akitokea Lyon. (B.T - in Danish)

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amekanusha uvumi kuwa amefanya mazungumzo na klabu ya Bayern Munich ili kuchukua nafasi ya Hansi Flick. (ESPN)

Kocha wa Bayern Massimiliano Allegri

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bayern wanapanga kumsajili kocha Massimiliano Allegri

Bayern wanamfikiria kocha Massimiliano Allegri kama mbadala wa Flick. Allegri hana timu toka alipoondoka Juventus mwaka 2019. (Sport Mediaset - in Italian)

Chelsea bado wangali katika mawindo ya beki wa Uruguay na Atletico Madrid Jose Maria Gimenez, 26, lakini chaguo lao la kwanza ni beki wa Sevilla Jules Kounde, 22. (La Razon - in Spanish)external-link

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero

Barcelona watatuma ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32, amble anaondoka klabuni halo mwishoni mwa msimu, lakini Barca hawataweza kufikia dau la mshahara lilitolewa na Juventus la Euro million 10 kwa msimu kwa mshambuliaji huyo. (Sport)external-link

Spurs wanapiga darubini za kumsajili mshambuliaji raia wa Austrian Sasa Kalajdzic,23, ambaye anachezea klabu ya Stuttgart. (Eurosport)external-link

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic

Manchester United wamehuisha nia yao ya kumsajilili kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26. Kiungo huyo pia anafuatiliwa na Real Madrid na PSG.(Gazzetta - in Italian)external-lin

Juventus wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 23, mkataba wake utakapoisha 2022. (Mundo Deportivo - in Spanish)external-link