Uhaba wa Oksijeni wasababisha hospitali za Kenya kusitisha upasuaji
Hospitali kubwa ya rufaa Afrika Mashariki, Kenyatta iliyopo nchini Kenya,imesitisha kufanya operesheni kwa wagonjwa waliokuwa wanasubiri kwa kuwa kuna uhaba wa upatikanaji wa Oksijeni.
Mkurugenzi wa hospitali , Evanson Kamuri, amesema hospitali hiyo itaendelea kufanya upasuaji mara tu hali ya upatikanaji wa oksijeni utakapo imarika.
“Lakini baadhi ya huduma za dharura za upasuaji unaohusiana na ugonjwa wa kansa, magonjwa ya yanayoambukizi kama Covid-19 na wale walio katika hali mahututi upasuaji unaendelea,” Dkt. Kamuri ameeleza katika taarifa yake.
Mahitaji ya wastani ya Oksijeni katika hospitali yameongezeka kutoka lita 4,000 mpaka lita 8,000 kwa siku kutokana na idadi ya wagonjwa wanaohitaji mashine ya kusaidia kupumua na waliokuwa katika hali mahututi kuongezeka.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa kuna uhaba wa oksijeni wiki mbili zilizopita.
Aliwalaumu watu wenye uwezo, hospitali na vituo vingine kuficha mitungi ya oksijeni.
Zaidi ya wagonjwa 200 wak katika kitengo cha dharura -ICU katika hospitali mbalimbali nchini humo - 53 kati yao wanatumia mashine ya kusaidia kupumua na wengine 253 wanapumua kwa msaada wa oksijeni.