Marais sita wapanga mkutano wa dharura juu ya mgogoro wa Msumbiji

Viongozi sita wa Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Msumbiji , Maputo,ambapo kutakuwa na mkutano wa dharura unaoangazia mashambulizo yanayotokea kusini mwa Afrika, tovuti ya serikali ya Zimbabwe imeripoti.

Moja kwa moja

Esther Namuhisa

  1. Uhaba wa Oksijeni wasababisha hospitali za Kenya kusitisha upasuaji

    mitungi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Hospitali kubwa ya rufaa Afrika Mashariki, Kenyatta iliyopo nchini Kenya,imesitisha kufanya operesheni kwa wagonjwa waliokuwa wanasubiri kwa kuwa kuna uhaba wa upatikanaji wa Oksijeni.

    Mkurugenzi wa hospitali , Evanson Kamuri, amesema hospitali hiyo itaendelea kufanya upasuaji mara tu hali ya upatikanaji wa oksijeni utakapo imarika.

    “Lakini baadhi ya huduma za dharura za upasuaji unaohusiana na ugonjwa wa kansa, magonjwa ya yanayoambukizi kama Covid-19 na wale walio katika hali mahututi upasuaji unaendelea,” Dkt. Kamuri ameeleza katika taarifa yake.

    Mahitaji ya wastani ya Oksijeni katika hospitali yameongezeka kutoka lita 4,000 mpaka lita 8,000 kwa siku kutokana na idadi ya wagonjwa wanaohitaji mashine ya kusaidia kupumua na waliokuwa katika hali mahututi kuongezeka.

    Waziri wa afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa kuna uhaba wa oksijeni wiki mbili zilizopita.

    Aliwalaumu watu wenye uwezo, hospitali na vituo vingine kuficha mitungi ya oksijeni.

    Zaidi ya wagonjwa 200 wak katika kitengo cha dharura -ICU katika hospitali mbalimbali nchini humo - 53 kati yao wanatumia mashine ya kusaidia kupumua na wengine 253 wanapumua kwa msaada wa oksijeni.

  2. Spika wa bunge la Tanzania awataka wabunge waishauri serikali juu ya manunuzi ya ndege

    MM

    Chanzo cha picha, IKULU

    Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kuishauri serikali kama iendelee na mpango wake wa kununua ndege au isitishe hadi itakapoweka mambo sawa, gazeti la Mwananchi nchini humo limeripoti.

    Bwana Ndugai ameuliza swali hilo leo bungeni mjini Dodoma, mara baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania, Charles Kicheere kutoa ripoti kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeingiza hasara ya takribani Shilingi Bilioni 150 kwa miaka mitano iliyopita.

    Na kwa mwaka mmoja uliopita, ATCL imeingiza hasara ya Shilingi bilioni 60. Bw. Kicheere ameyasema hayo leo Alhamisi alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Bungeni mjini Dodoma.

    Aidha Spika amewaambia wabunge kuwa wanatakiwa kuishauri Serikali kama iendelee na mpango wa kuongeza ununuzi wa ndege au wasitishe kwanza badala ya kusubiri kuja kukosoa mambo yatakapoenda kombo.

    Vilevile amewataka wabunge hao kushauri pia katika ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) kama ni vyema yakanunuliwa na Serikali au ununuzi ukafanywa na wabia wa sekta binafsi.

    Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa Ndugai alieleza kuwa kuna nchi zinafanya uwekezaji wa miundombinu ya reli na suala la mabehewa linafanywa na wawekezaji binafsi.

    • CAG ataja changamoto nne zinazoikabili ATCL
    • Shirika la ndege Tanzania leo kuidhinisha safari za kwenda Mumbai India
  3. Mwandishi mmoja Kenya auawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake

    Mwandishi wa habari wa Shirika la utangazaji Kenya -KBC ameuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake ambako ni pembezoni mwa mji mkuu wa Nairobi.

    Wanaume wawili wenye silaha waliingia nyumbani kwa Barasa wakati alipokuwa anaendesha gari akiwa anatoka kazini kwake majira ya jioni.

    Walimuamuru mume wa mwandishi huyo na watoto wake kulala chini na mwanaume mmoja mwenye silaha akampeleka bi. Barasa chumbani kwake.

    Baada ya muda walisikia milio ya risasi mara mbili na wanaume hao wakawa wanatoka chumbani humo.

    Polisi wa eneo la Ngong wanasema bi. Barasa alikuwa na jeraha katika kichwa.

    Chanzo cha mauaji hayo hakijaelezwa.

    Baraza la habari nchini Kenya limelaani vikali mauaji hayo na kutaka uchunguzi kuharakishwa;

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Aliyekamatwa kwa kutengeneza bango la picha ya Rais Kenyatta kulalamikia mikopo ya IMF aachiwa huru kwa dhamana

    Mwanaharakati Edwin Kiama aliyeshikiliwa kwa kutengeza bango lenye picha ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Kenya ili kulalamikia hatua ya serikali kuuchukua mkopo mwingine wa shilingi dola bilioni 255 au dola bilioni 2.34 ameachiwa huru kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea.

    Picha hiyo ilishirikishwa mtandaoni na Wakenya wengi wakilalamikia mkopo wa IMF kutochukuliwa nchini humo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mutemi Kiama ameachiwa huru Alhamisi kwa dhamana ya dola 4,600 (£3,300) na kutakiwa kuripoti kila siku kwa afisa wa uchunguzi.

    Mwanaharakati huyo aliwekwa kuzuizini kwa muda wa siku mbili wakati akihojiwa kwa uchunguzi .

    Wakenya mtandaoni wamekuwa wakilalamikia fedha za mkopo wa dola bilioni 2.4 zilizotolewa na IMF kwa taifa la Kenya kukabiliana na Covid-19 na kudai kuwa hiyo ni rushwa.

    Ingawa IMF ilitetea uamuzi wake wa kutoa mkopo licha ya malalamiko ya umma.

    Ilisema kuwa Kenya imejidhatiti kutumia vyema fedha hizo kwa walengwa na imejipanga kuunga mkono jitihada za taifa hilo katika kulinda rasilimali za wananchi.

  5. Kwanini Akon apewe ardhi Uganda?

    Uganda Presidency

    Chanzo cha picha, Uganda Presidency

    Maelezo ya picha, Akon atangaza kuanzisha mradi huohuo Senegal

    Waganda wamehoji tangazo lililotolewa na serikali ya Uganda juu ya uamuzi wa kumpa ardhi mwanamuziki wa Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon ili aweze kujenga mji ambao utaendeshwa kwa fedha za mwanamuziki huyo.

    Akon amesema tayari amesha ainisha eneo la ardhi ambalo atalitumia baada ya kupewa achague maeneo mbalimbali.

    Akon amesema mji huo utakuwa sawa na mradi anaopanga kufanya nchini Senegal lakini hakuweka wazi gharama ambazo atatumia kujenga mji huo au nani watashiriki kufadhili mradi huo.

    Waganda katika mitandao ya kijamii wameiuliza serikali kwanini ardhi itolewe kwa Akon wakati kuna wawekezaji wa ndani na wana uhitaji wa ardhi hiyo.

    "Je hakuna Waganda wenye fedha ambao wanaweza kufanya uwekezaji huo katika ardhi hiyo. Ni suala tu la kuwa na uongozi ambao unajipambanua vyema , kila kitu kinawezekana. Akon hawezi kuinua uchumi uliodorora Uganda kwa kupewa ardhi ya bure,Rogers Ishimwe aliandika katika Tweeter yake.

    "Akon kuepwa maili moja ya ardhi bure inaweza kueleweka kama serikali itatoa kiasi hicho hicho cha ardhi kwa vijana 640 kila mmoja aweze kulima ,"Kawalya aliandika katika Twitter.

  6. Marekani yawatahadharisha raia wake dhidi ya Kusafiri Kenya

    coro

    Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) kimetoa tahadhari kwa raia wake kutofanya safari nchini Kenya kwa maelezo kuwa nchi hiyo ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya Covid-19, kitaalamu (A Level 4 alert).

    Tahadhari hiyo imetolewa Aprili 07, ikionya juu ya usalama wa kiafya kutokana na kasi ya maambukizi ya corona nchini Kenya pamoja na ongezeko la uhalifu, ugaidi na utekaji.

    Wasafiri wa Marekani wameshauriwa na CDC , kuangalia kurasa ya idara ya usafiri kabla ya kupanga safari yeyote kutokana na changamoto ya COvid 19.

    Licha ya tahadhari hiyo kutolewa ndege za kimataifa bado zinafanya kazi nchini Kenya.

    Mwishoni mwa mwezi Machi, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza zuio la kukutoka nje katika kaunti tano nchini humo ukiwemo mji mkuu Nairobi ,Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru ili kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona .

    Hatua hii ilikuja kwasababu Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi kwa mujibu wa maelezo ya rais Kenyatta.

    Hakuna usafiri wa barabarani ,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kutoka sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga 'zilizoathiriwa sana na Corona.

    • Kituo cha afya CDC Marekani chatahadharisha raia wanaokwenda Afrika Mashariki
    • Rais Uhuru Kenyatta aifunga Nairobi na kaunti nyingine nne
  7. Marais sita wapanga mkutano wa dharura juu ya mgogoro wa Msumbiji

    MM

    Chanzo cha picha, IKULU

    Maelezo ya picha, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussen Mwinyi tayari yupo nchini Msumbiji, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

    Viongozi sita wa Afrika watakutana katika mji mkuu wa Msumbiji , Maputo,ambapo kutakuwa na mkutano wa dharura unaoangazia mashambulizo yanayotokea kusini mwa Afrika, tovuti ya serikali ya Zimbabwe imeripoti.

    Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) imeitisha mkutano huo wa Extraordinary Double Troika Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi. Ukiondoa Msumbiji ambaye ndio mwenyeji, mataifa mengine yatakayokuepo katika mkutano huo ni Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Malawi na Tanzania.

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagngawa tayari ameondoka katika kikao hicho.

    Awali rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema ataitisha mkutano wa baraza la ulinzi na usalama lakini hakuweka wazi ni lini mkutano huo utafanyika.

    Wanamgambo wa kiislamu walivamia mji wa Palma uliopo kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado Machi 24, na kuuwa watu kadhaa na mamia kulazimika kukimbia makazi yao huku wengine wakikimbilia Tanzania.

    Kundi la wanamgambo wa kiislamu (IS) walidai kuhusika na shambulio hilo.

    Kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu limlenga eneo hilo tangu Oktoba mwaka 2017, na hivi karibuni shambulio lao lililazimisha kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa kusitisha mipango yake ya uzalishaji wa gesi asilia katika eneo la Afungi Peninsula.

    • Kwanini ni vigumu kukabiliana na kundi la IS Msumbiji?
    • Uhusiano uliopo kati ya mali asili,uasi na mapigano nchini Msumbiji
    • Wanamgambo wa Kiislamu 'wawavamia wafanyakazi waliokuwa wakitoroka hotelini'
  8. Mbunifu wa fulana ya Jay Z yenye nembo ya msikiti wa Lamu aomba radhi

    RIYADHA MOSQUE LAMU

    Chanzo cha picha, RIYADHA MOSQUE LAMU

    Mbunifu wa Marekani aliyetumia picha ya msikiti wa kihistoria uliopo pwani ya Kenya, Lamu katika fulana aliyoivaa nyota wa Marekani Jay-Z aomba radhi.

    Viongozi wa msikiti wa Riyadha walioghadhabishwa na kupinga kwa fulana yenye msikiti wa Lamu kuvaliwa na msanii kwa kuhofia kuvaliwa katika sehemu za starehe wameridhia maombi ya msamaha wa mbunifu huyo.

    "Tumekubali msamaha wake kwa kuwa alifanya kwa nia njema," maofisa wa msikiti wamesema.

    Mbunifu Zeddie Loky aliripotiwa kutengeneza fulana hiyo ili kuutangaza mji wa Lamu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    BBC iliwasiliana naye na akasema;.

    Lamu imetajwa na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO-kuwa eneo la urithi wa dunia na msikiti huo uliojengwa karne ya 19 ni miongoni mwa vivutio vikubwa.

    Ni msikiti ulioanza tangu mwaka 1837, ni miongoni mwa taasisi za zamani zaidi za ufundishaji za Kiislamu katika Afrika Mashariki.

    Waumini walipata ghadhabu walipoona picha ya mwanamuziki wa Marekani akiwa amevaa fulana yenye picha ya msikiti wa Lamu katika makundi ya WhatsApp , alisema katibu mkuu wa msikiti huo bwana Abubakar Badawy.

    • Kwa nini Jay Z ameghadhabisha Waislamu Lamu, Kenya?
  9. Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili leo 08/04/2021.