Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Hayati Magufuli azikwa Chato Tanzania

Hatimaye baada ya kuagwa kwa siku tano mfululizo katika mikoa mbalimbali na kisiwani Zanzibar mwili wa John Pombe Magufuli amezikwa nyumbani kwao huko Chato

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu and Lizzy Masinga

  1. Sisi asifu oparesheni ya kuindoa Meli iliyokwama katika mfereji wa Suez

    Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi amesifu operesheni ya Kundolewa kwa meli kubwa ya makontena ambayo ilikuwa imekwama katika Mfereji wa Suez na kusababisha msongamano mkubwa wa meli zinazofaa kupita katika mfereji huo

    "Kwa kurudisha mambo kuwa katika hali ya kawaida, kwa mikono ya Wamisri, ulimwengu wote unaweza kuhakikishiwa njia ya bidhaa na mahitaji ambazo zinachukuliwa kupitia njihii ya baharini’ Bwana Sisi amenukuliwa akisema.

    Mwandishi wa habari wa Euronews ameiweka mtandaoni video ya meli hiyo iliyo na urefu wa mita 400 (1,300ft) ikwa jina Ever Givenikielea tanguilipokwama wiki jana

  2. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja, tukutane tena Jumatatu tarehe 29/03/2021, Shukrani.

  3. Hayati Magufuli azikwa Chato

    Ni safari ya mwisho ya Hayati Rais John Pombe Magufuli , amelazwa katika nyumba yake ya milele.

    Amezikwa kwa taratibu zote za kijeshi ambazo anapaswa kupatiwa Amiri Jeshi Mkuu.

    Mizinga 21 imepigwa ikiashiria heshima kubwa kwa kiongozi huyu.

    Hayati Magufuli amezikwa katika eneo la makaburi ya familia mjini chato , mkoani geita.

    Watu wa karibu na familia pamoja na viongozi ndio wameshiriki moja kwa moja katika mazishi haya kwa kufika Geita na wengine kufuatilia moja kwa moja kwenye matangazo ya Televisheni.

    Mapema hii leo Hayati magufuli, aliagwa kwa misa maalum, ambayo ilifanika katika kiwanja cha wazi, Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

  4. Rais Uhuru Kenyatta,mkewe, mawaziri wapata chanjo dhidi ya corona

    Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza maafisa wakuu wa serikali kupokea chanjo ya corona katika Ikulu ya Nairobi.

    Baada ya kutangaza masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya Covid 19 nchini Kenya rais alikuwa wa kwanza kuchanjwa kisha mkewe Margaret Kenyatta akachomwa chanjo hiyo .

    Wengine waliochanjwa ni waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i , Waziri wa Afya Mutahi Kagwe waziri wa mashauri ya kigeni Raychelle Omamo ,Kaimu Jaji mkuu Philomena Mwilu na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kidini .

    Rais amewasisitiza Wakenya wachanjwe dhidi ya virusi hivyo baada ya serikali kutangaza kwamba itawapa kipaumbele watiu walio na umri wa miaka 58 na zaidi katika kutoa chanjo hiyo .

  5. Rais Uhuru azifunga kaunti tano Kenya kutokana corona

    Rais Uhuru Kenyatta amezifunga kaunti tano nchini Kenya kutokana na ongezeko la wagonjwa wa corona.Kaunti hizo ni Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru.

    Marufuku hiyo inaanza ifikapo saa sita usiku.

    Hakuna usafiri wa barabarani,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kuondoka katika sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga ‘kubwa la corona’.

    Maeneo hayo yatakuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 zijazo . 'Ukiwapima Corona Wakenya 100 ,20 watapatikana na virusi hivyo.Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi’ rais Kenyatta amesema.

    Rais Uhuru amesema wimbi la tatu la janga ilo nchini Kenya linatarajiwa kufika kilele chake katika siku 30 zijazo .

  6. Kikwete: Magufuli alikuwa jembe langu

    Rais wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema taarifa ya kifo cha Magufuli ilikuwa jambo gumu kulipokea na kulikubali.

    Akieleza mahusiano yake na hayati Magufuli tangu alipokuwa waziri wake, Kikwete amesema alikuwa 'jembe lake'.

    Nilipokuwa Rais, Magufuli alikuwa Waziri wangu kwa miaka 10, alikuwa mmoja wa mawaziri niliowaamini na kumtumaini.

    ‘’Alikuwa jembe langu ndio maana nilimuweka kwenye wizara tatu zilizokuwa ngumu ili anyooshe mambo.’’ Alisema Kikwete.

    ‘’Yalikuwa matumaini yangu na matarajio yangu angemaliza kipindi chake cha uongozi salama, akastaafu na kuishi maisha marefu baada ya hapo na kupata nafasi ya kutuzika sisi watangulizi wake ambao ni kaka zake, hili la kututoka kabla ya kumaliza muhula wake na sisi kumzika yeye ni jambo ambalo sikuwahi kulifikiria kabisa.’’ Alisema Kikwete.

    Amesema uongozi wake bado ulikuwa ukihitajika Tanzania, na kuwa alikuwa akitamani akamilishe kazi yake nzuri aliyokwisha ianza.

    • Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Aliyotufanyia kiongozi huyo hatutamsahau
    • Kifo cha rais John Magufuli: Je kiongozi huyu atakumbukwaje nje ya Tanzania?
  7. Mkuu wa Majeshi Tanzania aahidi utii kwa Rais Samia Suluhu Hassan

    Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo ameahidi utiifu kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu.

    Bw. Mabeyo amemhakikishia kuwa ulinzi wa nchi na mipaka yake ni salama na vitaendelea kumlinda, kumtii kama Amiri Jeshi Mkuu na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

    ‘’Tunakuahidi utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kama ilivyo ada ya mila na desturi ya majeshi yetu katika awamu zote zilizopita kwa manufaa ya ulinzi, usalama na ujenzi wa taifa letu’’. Amesema Jenerali Mabeyo.

    Jenerali Mabeyo amesema hayo mjini Chato wakati akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Amirijeshi Mkuu.

    Kuhusu namna alivyomfahamu na kufanya naye kazi hayati Magufuli Jenerali Mabeyo alisema;

    ‘’Aliviamini na kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama alihakikisha kuwa anaviwezesha kwa mahitaji ya kiutendaji na utawala ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi mkubwa.’’

    ‘’Alisema hatuwezi kuwa na vyombo vya ulinzi imara bila kuwa na uchumi madhubuti, hatuwezi kutegemea misaada ya kuimarisha vyombo vyetu lazima tuimarishe uchumi wetu ili tuweze kuimarisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.’’

    Mabeyo amesema walishiriki katika kulinda mgodi wa Tanzanite, na kabla ya kulinda, kujenga ukuta kuzunguka mgodi huo.

  8. Rais kenyatta awaagiza maafisa, mawaziri wake kupata chanjo ya Covid-19

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaagiza mawaziri wote na maafisa wakuu serikalini wawe kielelezo kwa kupokea chanjo dhidi ya Corona.

    Maafisa kadhaa wakuu katika serikali akiwemo mkuu wa wafanyakazi katika Ikulu Nzioka Waita ni miongoni mwa waliochanjwa .

    Kupitia Ujumbe wa Twitter uliokuwa na picha akipokea chanjo hiyo Waita amethibitisha maelekezo hayo ya rais kuhusu kuchanjwa kwa maafisa wakuu .

    Hatua hiyo ni kinyume na msimamo wa hapo awali wa serikali kwamba wanasiasa hawataruka foleni kwa kuchanjwa kwanza kabla ya makundi ya watu wengine waliopangwa kuchanjwa mwazoni.

    Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe amesema Wakenya milioni 1.25 watapokea dozi ya shehena ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca na wanasiasa sio miongoni mwa watakaopewa chanjo hiyo .

    Kumekuwa na hofu miongoni mwa Wakenya kuhusu usalama wa chanjo ya Corona na serikali imechukua hatua za uhamasishaji ili kuwarai watu kwenda kuchanjwa.

  9. Viongozi wawaongoza Watanzania katika ibada ya mazishi

    Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekua Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli.

  10. Eritrea kuondoa vikosi vyake Tigray, asema Waziri Mkuu Abiy

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema Eritrea imekubali kuondoa vikosi vyake kutoka mpaka wa Tigray baada ya makabiliano ya kijeshi ambayo yalilaaniwa vikali.

    Bwana Abiy mapema wiki hii alikiri kwa mara ya kwanza kwamba wanajeshi wa Eritrea walivuka mpaka baada ya miezi kadhaa ya kukana.

    Aliwaambia Wabunge kuwa vikosi vya Eritrea walifika wakihofu watashambuliwa na wapiganaji wa Tigray.

    Katika taarifa siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu alisema majadiliano na rais wa Eritrea Isaias Afwerki yametamatisha kuwa vikosi vya Ethiopia ‘’vitachukua jukumu la kulinda maeneo ya mipaka haraka ‘’.

    Ethiopia na Eritrea ‘’wataendelea kuimarisha mahusiano yao na ushirikiano wa kiuchumi ‘’ aliongeza.

  11. Wakazi wa Chato wapiga kambi usiku kucha karibu na uwanja wa Magufuli

    Kwa siku kadhaa hivi sasa, baadhi ya wakazi wa mji wa Chato na viunga vyake waliokuja kuaga mwili wa rais John Pombe Magufuli.

    Wamelazimika kulala katika mazingira magumu huku wakipigwa na baridi ya usiku kutoka Ziwa Victoria.

  12. Mwili wa Magufuli kuzikwa katika makaburi ya familia Chato

    Mwili wa hayati John Pombe Magufuli hii leo utazikwa katika makaburi ya familia huko mjini Chato, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

    Maelfu ya wananchi tayari wameanza kujitokeza katika uwanja wa Magufuli ambapo kutakuwa na misa maalumu hapo baadae.

    Mapema hii leo, mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ambae alifariki tarehe 17 mwezi Machi kutokana na tatizo la moyo utapelekwa kanisani kwa ibada maalumu.

  13. Rais Samia Suluhu Hassan awapongeza Watanzania kwa kumuomboleza Magufuli

  14. Wakaazi wa Chato wakiusubiri mwili wa John Pombe Magufuli

  15. Habari za hivi punde, Aliyekuwa rais wa awamu ya tano Tanzania kuzikwa hii leo

    Raia wa Tanzania wanauomboleza aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli lakini kwa wakazi wa Chato ni zaidi ya hilo kwasababu hii ndio itakuwa mara ya mwisho kumuona mwana wao .

    Ikilinganishwa na awali ambapo alisimama kandokando ya barabara ili kuwahutubia , wakati huu hatozungumza kwa makumi ya maelfu ambao watamsubiri kandokando ya barabara inayoelekea nyumbani kwake huko Chato.

    Hii Leo mwili wa kiongozi huyo wa Tanzania utazikwa huku maelfu ya raia wa taifa la Tanzania wakisubiri kuhudhuria mazishi yake.

    Rais Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam tarehe 17 Machi.

    Hii ni mara ya kwanza kwamba Watanzania kumzika rais aliyefariki akiwa madarakani katika miaka 60 ya Uhuru.

    Kama inavyotarajiwa , taifa hilo limekuwa likikumbwa na huzunitangu kifo chake kilipotangazwa na makamu wake usiku wa tarehe 17 mwezi Machi.

    Hii leo Misa mbili maalum zitafanyika. Ya kwanza ikifanyika katika kanisa ambalo alikuwa akienda kufanya ibadaChatona misa ya pili ikifanyika katika uwanja wa Mgufuli , ambapo maelfu ya waombolezaji wamekongamana.

    Kutoka hapo atazikwa katika makaburi ya familia chini ya itifaki zote za kumzika amiri jeshi mkuu.

    Bwana Magufuli atakumbukwa kwa kuwa mkatoliki mkakamavu , atakumbukwa na wengi kwa vita vyake dhidi ya ufisadi, na ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo.

    Hili lilishuhudiwa siku ya Jumatatu wakati viongozi kadhaa wa Afrika walipomuenzi katika mazishi ya kitaifa yaliofanyika katika mji mkuu wa Dodoma.

    Kwengineko pia atakumbukwa kama kiongozi ambaye hakuvumilia wapinzani wake wa kisiasa , alikandamiza vyombo vya habari na wanaharakati.

    Pia atakumbukwa kwa jinsi alivyokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

  16. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ambayo hii leo tutaendelea kukujuza kuhusu mazishi ya Rais John Pombe Magufuli