Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais Magufuli: Je, Katiba ya Tanzania inatoa mwongozo gani anapofariki Rais?
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Magufuli alishinda uchaguzi kwa mara ya pili mwezi Oktoba mwaka jana
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefariki dunia Jumatano jioni; na swali la wengi ndani na nje ya Tanzania kwa sasa ni nini kitakachofuata kwa mujibu wa Katiba?
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli:Balozi wa Marekani atuma salamu za rambirambi kwa Watanzania
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright ametuma salamu za rambirambi kwa Watanzania kupitia ukurasa wake wa Twitter; "Kwa niaba ya watu wa Marekani, Ninatuma salamu zangu za rambirambi kwa kila mmoja anayeomboleza kifo cha Rais Magufuli hii leo.
Ifahamike kuwa Marekani iko pamoja na Watanzania katika wakati huu mgumu".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Habari za hivi punde, Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Watanzania waomboleza kifo cha Magufuli
Maelezo ya video, Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Watanzania wamuomboleza rais wao
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: 'Nikifa nizikwe nyumbani kule alikozikwa baba ''Chato''
Raila Odinga amuomboleza rafiki yake rais Magufuli
Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga
ametuma risala za rambirambi kwa familia ya rais John Pombe Magufuli na raia wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Raila amemtaja marehemu kama
kiongozi aliyejaribu kuimarisha hali ya raia wa Tanzania.
Amesema kwamba rais Magufuli amekuwa rafiki yake wa muda mrefu na kwamba
amekuwa kando yake wakati mgumu alipomuhitaji.
Amesema kwamba tangazo la kifo chake amelipokea na huzumi kubwa
akiongezea kwamba anasimama na familia ya marehemu wakati huu wa maombolezo.
Kiongozi huyo amesema kwamba kwa
miaka kadhaa iliopita ameshirikiana na rais Magufuli haswa katika kuiunganisha
Afrika mashariki kupitia miundo msingi.
Amewataka Watanzania wote kusalia watulivu na
kufuata utamaduni uliowachwa na rais wa kwanza wa taifa hilo Julius Nyerere na
wa viongozi waliofuata katika kukabidhiana mamlaka kulingana na katiba ya taifa
hilo
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Tarehe za matukio Muhimu katika maisha ya Rais John Pombe Magufuli
Chanzo cha picha, Getty Images
1959- Azaliwa Chato
kaskazini magharibi mwa Tanzania
1995- Achaguliwa kuwa
mbunge kwa mara ya kwanza
2000- Ateuliwa kuwa Waziri
2015- Achaguliwa kuwa rais
kwa muhula wake wa kwanza
2020- Achaguliwa kwa
kipindi cha pili kuwa rais
2020 Novemba tarehe 5 –
Aapishwa kwa muhula wa Pili
2021 Machi Tarehe 7- Uvumi
unaanza kuenea kuhusu aliko rais Magufuli baada ya kukosa kuonekana kwa muda wa
wiki moja
2021 Machi tarehe 11 –
Vyama mbali mbali vya Upinzani nchini Tanzania vyataka kujua hali ya rais
Magufuli na aliko
2021 Machi Tarehe 12 -Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akana kwamba rais
Magufuli anaugua asema yupo ‘ buheri wa afya na anaendelea kuchapa kazi’
2021 Machi Tarehe 15 –
Makamu wa Rais Samia Suluhu awapa Watanzania ‘salamu’ kutoka kwa Rais Magufuli
huku hofu ikizidi kuhusu hali yake na aliko
2021 Machi, tarehe 6 -
Alazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa
umeme
2021 Machi tarehe 7 -
Aliruhusiwa kurejea kazini
2021 Machi tarehe 14 -
Alikimbizwa Hospitali ya Mzena Dar es Salaam kuendelea na matibabu
2021 Machi tarehe 17 saa
kumi na mbili jioni - Magufuli afariki dunia
2021 Machi tarehe 17 Usiku
– Makamu wa rais Samia Suluhu atangaza kupitia runinga kifo cha rais Magufuli
.Siku 14 za maombolezo zatangazwa.Bendera kupeperushwa nusu mlingoti.
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Buriani Rais John Pombe Magufuli
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Risala za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali Tanzania
Kufuatia
kifo cha Rais John Magufuli wa Tanzania watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na serikali
wamelezea hisia zao na namna walivyopokea taarifa za kifo cha kiongozi huyo,
ambaye ni Rais wa awamu ya tano wa taifa hilo.
Miongoni
mwao ni Waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Fredrick Sumaye, ambaye wakati huo
akiwa waziri mkuu, Rais Magufuli alikuwa kwenye nafasi ya naibu waziri na baadaye
waziri katika wizara ya Ujenzi.
Sumaye
anaeleza alivyopokea taarifa hii ya msiba huu,
‘’Mimi niliziona taarifa hizi kwenye runinga nikashutuka
kama sio kitu cha kweli, na mwanzoni watu walionipigia simu nilisema siamini
kama ni za kweli, lakini sasa naamini ni za kweli. Ni taarifa imetushutusha
sana, ni taarifa imetusikitisha sana kama taifa, kwasababu taifa kupoteza rais
ambaye yuko kwenye kiti siyo jambo dogo. Rais Magufuli wote tunamjua ni mchapa
kazi, ni msema kweli na lile alaolisema ndilo analotenda. Tumesikitika sana
kumpoteza kiongozi wetu huyu, Rais wetu mpendwa lakini ndio kazi ya Mungu.’’
Mheshimiwa Sumaye amekuwa kwenye serikali kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 25 na amehudumu kama waziri mkuu na amemtaja Rais Magufuli kama mtu ambaye
haogopi kufanya maamuzi.
‘’Nimepokea
taarifa za msiba wa Rais Magufuli kwa masikito makubwa, nimemuona makamu rais
akitangaza msiba huu na vilevile nimempigia simu ya kumpa pole kwasababu sasa kwa
mujibu wa katiba yetu yeye ndio rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani
ya muda mfupi atakula kiapo cha kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni majukumu mazito sana kwake na pia msiba huu ni mkubwa
sana. Kwa niaba ya chama cha ACT- Wazalendo na kwa niaba yangu binafsi, natoa
pole kwa mama yetu Janet Magufuli na familia nzima ya hayati John Pombe Joseph Magufuli,
tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Natuma salamu zangu pia za rambirambi kwa makamu mwenyekiti wa CCM na wanachama wa CCM kwa kuondokewa na mwenyekiti wao
wa taifa’’.
Bwana Zitto Kabwe amemzungumzia Bwana Magufuli ambaye
amekuwa kiongozi wa nchi yao katika nyadhifa mbalimbali na ‘’kwa hakika
alitekeleza wajibu wake kwa juhudi kubwa. Taifa litamkumbuka kwa
mchango wake kwenye maendeleo yetu’’.
Chanzo cha picha, FATMA KARUME/FACEBOOK
Fatma Karume, mwana wa Abeid Karume naye pia amezungumza na BBC na kutoa risala zake.
‘’Inasikitisha
sana imechukua muda mrefu kwa wananchi kuambiwa ukweli, Kwa muda mrefu nchi
ilikuwa kwenye taharuki. Lakini Mungu mlaze mahala anapostahiki kumlaza’’. Fatuma
Karume amemuelezea kama rais wa nchi hana uhakika kama atakumbukwa na watu
wengi kwa mema kwa maana kwamba tangu alipoingia kwenye urais, nchi ya Tanzania
imebadilika sana, imekuwa nchi ya huzuni, akidai kuwa uhuru wao binafsi umechukuliwa.
‘’Naomba tuache kuumizana, turudi kwenye upendo’’.
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amuomboleza Rais Magufuli
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameelezea kusikitishwa na kifo cha rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
Amekuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza duniani kutuma salamu za rambi rambi baada ya kutangazwa kwa kifo cha Magufuli . '‘ Fikra zangu zipo na wapendwa wake pamoja na Watanzania’amesema kupitia ujumbe aliondika kwenye twitter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kulingana na katiba ya Tanzania makamu wa rais wa nchi hiyo Samia Hassan Suluhu ataapishwa kuhudumu kama rais mpya ili kukamilisha muda uliosalia wa muhula wa miaka mitano wa Magufuli ulioanza mwaka jana''.
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Mkuu wa WHO amuomboleza Magufuli
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom ametuma salamu za rambirambi kwa Watanzania na serikali ya nchi hiyo kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli.Kupitia ujumbe wa Twitter Teodros amesema Shirika hilo limewaweka Watanzania pamoja na familia ya rais Magufuli wakati huu mgumu:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Hujambo na Karibu kwa matangazo haya maalumu ya moja kwa moja kuhusu kifo cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli