Kufuatia
kifo cha Rais John Magufuli wa Tanzania watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na serikali
wamelezea hisia zao na namna walivyopokea taarifa za kifo cha kiongozi huyo,
ambaye ni Rais wa awamu ya tano wa taifa hilo.
Miongoni
mwao ni Waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Fredrick Sumaye, ambaye wakati huo
akiwa waziri mkuu, Rais Magufuli alikuwa kwenye nafasi ya naibu waziri na baadaye
waziri katika wizara ya Ujenzi.
Sumaye
anaeleza alivyopokea taarifa hii ya msiba huu,
‘’Mimi niliziona taarifa hizi kwenye runinga nikashutuka
kama sio kitu cha kweli, na mwanzoni watu walionipigia simu nilisema siamini
kama ni za kweli, lakini sasa naamini ni za kweli. Ni taarifa imetushutusha
sana, ni taarifa imetusikitisha sana kama taifa, kwasababu taifa kupoteza rais
ambaye yuko kwenye kiti siyo jambo dogo. Rais Magufuli wote tunamjua ni mchapa
kazi, ni msema kweli na lile alaolisema ndilo analotenda. Tumesikitika sana
kumpoteza kiongozi wetu huyu, Rais wetu mpendwa lakini ndio kazi ya Mungu.’’
Mheshimiwa Sumaye amekuwa kwenye serikali kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 25 na amehudumu kama waziri mkuu na amemtaja Rais Magufuli kama mtu ambaye
haogopi kufanya maamuzi.
‘’Nimepokea
taarifa za msiba wa Rais Magufuli kwa masikito makubwa, nimemuona makamu rais
akitangaza msiba huu na vilevile nimempigia simu ya kumpa pole kwasababu sasa kwa
mujibu wa katiba yetu yeye ndio rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani
ya muda mfupi atakula kiapo cha kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni majukumu mazito sana kwake na pia msiba huu ni mkubwa
sana. Kwa niaba ya chama cha ACT- Wazalendo na kwa niaba yangu binafsi, natoa
pole kwa mama yetu Janet Magufuli na familia nzima ya hayati John Pombe Joseph Magufuli,
tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Natuma salamu zangu pia za rambirambi kwa makamu mwenyekiti wa CCM na wanachama wa CCM kwa kuondokewa na mwenyekiti wao
wa taifa’’.
Bwana Zitto Kabwe amemzungumzia Bwana Magufuli ambaye
amekuwa kiongozi wa nchi yao katika nyadhifa mbalimbali na ‘’kwa hakika
alitekeleza wajibu wake kwa juhudi kubwa. Taifa litamkumbuka kwa
mchango wake kwenye maendeleo yetu’’.
Fatma Karume, mwana wa Abeid Karume naye pia amezungumza na BBC na kutoa risala zake.
‘’Inasikitisha
sana imechukua muda mrefu kwa wananchi kuambiwa ukweli, Kwa muda mrefu nchi
ilikuwa kwenye taharuki. Lakini Mungu mlaze mahala anapostahiki kumlaza’’. Fatuma
Karume amemuelezea kama rais wa nchi hana uhakika kama atakumbukwa na watu
wengi kwa mema kwa maana kwamba tangu alipoingia kwenye urais, nchi ya Tanzania
imebadilika sana, imekuwa nchi ya huzuni, akidai kuwa uhuru wao binafsi umechukuliwa.
‘’Naomba tuache kuumizana, turudi kwenye upendo’’.