Kifo cha Rais Magufuli: Wanyarwanda wako pamoja na Tanzania wakati huu mgumu
Dunia yaomboleza kifo cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Moja kwa moja
Asha Juma and Dinah Gahamanyi
Tuna imani na Samia Hassan Suluhu
Maelezo ya sauti, Tuna imani na Samia Hassan Suluhu
Jaji mkuu mstaafu mzee Joseph Sinde Warioba ameiambia BBC ana imani na Mama Samia na hana shaka lolote juu ya namna mabadiliko ya utawala yatakavyofanyika kwani katiba ya Tanzania iko wazi na itafuatwa. Zuhura Yunus alimtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumza naye na swali la kwanza alimuuliza ameupokeaje msiba wa rais Magufuli.
Muhammadu Buhari: Rais Magufuli atakumbukwa daima
Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Nigeria Muhammadu
Buhari amejiunga na serikali na watu wa
Tanzania katika maombolezo ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli, aliyefariki
dunia akiwa na umri wa miaka 61.
Kiongozi huyo wa Nigeria amesema Magafuli “urithi wa uzalendo na kujitolea kwa ajili ya Uafrika
itaendelea kukumbukwa kote barani .”
Rais Buhari anasema Hayati rais wa Tanzania “alitumia
muda wake mwingi zaidi wa maisha yake kulitumikia taifa na ubinadamu .”
Taarifa kutoka katika ofisi ya rais ya Nigeria inasema Bw
Buhari “anaamini ujasiri na upendo kwa nchi wa Hayati rais wa Tanzania vilihamasisha mageuzi mbalimbali ambayo vizazi vitaendelea kuyakumbuka ”
Kwa mujibu wa Bw Buhari, John Magufuli atakumbukwa kwa mambo mbali mbali ikiwa ni
pamoja na “ kupunguza ukubwa na gharama za utawala, kusisitiza kuhusu bajeti
inayowalenga watu, yenye vipaumbele vya
wazi kuhusu elimu na afya, na kupambana wakati wote na ubadhirifu katika
matumizi ya umma.”
Kiongozi huyo wa Nigeria ametoa salamu za rambi rambi kwa
familia ya marehemu “ kiongozi mwenye maono
wa Tanzania”, marafiki na washirika wake, pamoja na wananchi wote wa Tanzania.
Rais Buhari amesema anaimbea roho ya marehemu
ipumzike kwa Amani.
Spika wa bunge aagiza kamati za bunge mikoani kurejea Dodoma
Chanzo cha picha, BUNGE
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ameagiza Kamati
zote za Bunge zilizokuwa katika ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo mikoani
kurejea Dodoma mara moja.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutangazwa kwa kifo
cha Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea
hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Job Ndugai, amesema kuwa amepokea kwa huzuni
na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Magufuli.
‘’Tumempoteza Rais wetu kipenzi aliyejitoa kuwatumikia
Watanzania wote kwa uadilifu, umahiri, bidii na moyo wa uzalendo wa hali ya
juu. Kwa niaba ya Bunge natoa pole kwa Janeth Magufuli na familia ya marehemu,
makamu wa rais pamoja na Watanzania wote kufuatia msiba huu mzito wa kitaifa.’’
Wasanii wa muziki Tanzania wamlilia Magufuli
Baadhi ya Wasanii wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakielezea hisia zao za huzuni kuhusu kifo cha rais wa nchi hiyo Dkt John Pombe Magufuli ambaye amefariki dunia jana kutokana na maradhi ya moyo.
Wasanii hao ambao ni pamoja na Diamond Platnumz, RayVanny, Jux, Marioo, Malkia Karen, Zuchu, Khadija Kopa, Christina Shusho, wamejikusanya na kuingia studio kuandaa wimbo wa pamoja wa kumuaga Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Baadhi ya wasanii hao walielezea hisia zao kuhusu kifo cha Bw Magufuli kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Instagram ujumbe, 4
'Nilikuwa na Magufuli dawati moja darasani'
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Watanzania wameamkia taarifa kuwa rais wao amefariki dunia.
Mwalimu aliyestaafu Kasara Mnaku amemkumbuka aliyekuwa
mwanafunzi mwenzake – Hayati mzee John Magufuli, ambaye amefariki dunia akiwa
na umri wa miaka 61.
Katika mahojiano na mwandishi wa BBC Aboubakar Famau,
Bwana Mnaku amesema:
''Tuliishi katika
kijiji kimoja. Tulikuwa darasa moja na tukaketi dawati moja. Katika maisha yake
ya awali, hadi alipokuwa rais, tulikuwa pamoja na alikuwa rafiki yangu. Kila
alipohitaji ushauri angenipigia simu na tungezungumza''.
Bw Mnaku Aliongeza: ''Tulipokuwa
watoto tulikuwa na uhusiano wa karibu kweli na kusaidiana na tulipenda mno
kusoma.Hili lilitusaidia kufika
tulipofika, Nikawa mwalimu na yeye pia akawa mwalimu lakini hatimaye akaamua
kuacha taaluma hiyo na kuhudumia nchi."
Mwanafunzi mwingine
aliyesoma naye, Elias Kwaswahili, amesema:
''Tuliishi
kijiji kimoja cha Rubambangwe na sote tulisomea katika shule ya msingi ya Chato. Na
baadaye tukakutana katika shule ya sekondari ya Lake Mwanza''.
Elias Kwaswahili: ''Alikuwa mwanafunzi mzuri sana
darasani hasa katika sayansi. Tuliona masomo ya sayansi yakiwa magumu hasa
hisabati. Lakini alikuwa mzuri sana katika hesabu na hili ndili lililo msukuma
kufanya masomo ya sayanasi. Hivyo ndivyo nilivyo mfahamu".
Bwana Magufuli alikuwa na shahada ya uzamili ya kemia
na aliwahi kufanya kazi kama mwalimu wa sayansi na hisabati. Alikuwa mbunge
mwaka 1995 na kupanda cheo hadi kuwa rais mwaka 2015.
Serikali imesema Bwana
Magufuli amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo.
Jinsi Magufuli anakavyokumbukwa katika kijiwe hiki cha kahawa,Geita
Maelezo ya video, Kifo cha Magufuli:Jinsi Magufuli atakavyokumbukwa katika kijiwe hiki cha kahawa,Geita
Kifo cha Rais Magufuli: Rais wa Malawi asema Magufuli alikuwa kiungo muhimu
"Ni pigo kwa Afrika," asema Rais wa Malawi Lazarus Chakwera baada ya kupokea taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania John Magufuli, 61.
"Rais Magufuli walikuwa ishara kuu ya ufufuo wa uchumi wa Afrika, na kifo chake ni pigo kubwa kwa bara hili," Bw. Chakwera aliongeza katika ujumbe wake wa Twitter.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais John Magufuli:CCM kufanya kikao maalum machi 20
Wakuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanatarajia kufanya kikao maalumu Jumamosi Machi 20, kufuatia kifo cha mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli.
Philip Mangula makamu mwenyekiti Tanzania bara na Mzee Ali Mohamed
Shein makamu mwenyekiti Tanzania visiwani wamekubaliana kufanya kikao
maalumu na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa Jumamosi katika ukumbi wa Lumumba jijini Dar
es salaam.
Aidha chama kitakuwa katika maombolezo kwa siku 21 sambamba na tangazo la
serikali.
Maelezo zaidi:
Je, Katiba ya Tanzania inatoa mwongozo gani anapofariki Rais?
Kifo cha Rais John Magufuli: Wafahamu viongozi wa Afrika waliofariki madarakani
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills
Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani. Katika kipindi cha miaka 20 iliopita mkosi huo umeathiri mataifa mengi barani Afrika .
Lakini ni kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais Magufuli: Mechi za kirafiki zasimamishwa Tanzania na Kenya kupisha maombolezo
Shirikisho la
mpira wa miguu nchini Tanzania TFF
limesimamisha mechi zake zote za ndani
kwa wiki mbili ili kuungana na watanzania katika maombolezo.
Chanzo cha picha, TFF
Aidha Kenya imehairisha mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Tanzania iliyopangwa kuchezwa Alhamisi hii jijini Nairobi.
Kocha Jacob Mulee,ameeleza kuwa mechi hiyo imeitishwa kufuatia kifo cha raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli.
Hakuweka wazi ikiwa mechi hiyo itachezwa siku gani.
Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa sehemu ya maandalizi ya Kenya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Misri na Togo zilizopangwa baadae mwezi huu.
Kifo cha Magufuli: Vichwa vya habari magazetini
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Watanzania waliamkia taarifa za kifo cha Rais Magufuli
Kifo cha Magufuli: Wanyarwanda wako pamoja na Tanzania wakati huu mgumu
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametuma salamu zake za rambirambi kupitia kurasa ya Twitter.
"Tunasikitika kumpoteza kaka na rafiki yangu, Rais Magufuli , Mchango wake katika taifa lake na kwa bara la Afrika hautasahaulika.
Salamu zangu za dhati ziende kwa familia na Watanzania.
Wanyaruanda wako pamoja na Watanzania katika wakati huu mgumu.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Rais Magufuli alifanikiwa kurudisha uhusiano mzuri na taifa la Rwanda na Tanzania baada ya mvutano wa miaka miwili kati ya mataifa hayo uliokuepo wakati wa utawala wa rais Jakaya Kikwete.
Katika safari yake nchini Rwanda, bwana Magufuli alisema alialikwa maeneo mengi na hakwenda lakini wakati rais Kagame alivyomualika ,aliamua kwenda”.
Rais Kagame alimpa rais Magufuli ng'ombe watano wakati alipotembelea Rwanda ikiwa ishara ya urafiki wa kweli na imara.
Kifo cha Magufuli: Mfahamu Samia Suluhu Hassan, Rais ajaye wa Tanzania
Chanzo cha picha, Getty Images
Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.
Kifo cha Rais Magufuli: Bobi Wine atuma salamu za rambirambi kwa Watanzania
Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha upinzani nchini
Uganda Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine atuma salamu za rambirambi
kwa raia wa Jamuhuri ya muungano wa
Tanzania.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais Magufuli: Wafahamu viongozi wa Afrika waliofariki madarakani
Kifo cha Rais Magufuli: Afrika Kusini yaungana na Tanzania katika maombolezo
Chanzo cha picha, twitter
Raisi
wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Katika
taarifa yake, raisi Ramaphosa amesema
amezungumza na Makamo wa Raisi wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimweleza
huzuni yake na kwa niaba ya raia wa Afrika Kusini.
‘’Afrika Kusini inaungana na serikali na watu wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu’’alisema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais Magufuli: Museveni asema Magufuli alikuwa kiongozi anayeongoza kwa uhalisia
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Uganda, Yoweri Mseveni ametuma salamu za rambirambi katika ukurasa wake wa Twitter.
Rais Museveni amesema, amesikitishwa sana na kifo cha Rais Magufuli.
Alikuwa kiongozi ambaye anaongoza kwa uhalisia na aliyeamini katika kukuza uchumi wa Afrika Mashariki.
Tunajumuika na Watanzania kuomboleza kifo cha mtoto wa Afrika.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kifo cha Rais Magufuli:'Nimempoteza rafiki, mwenzangu na mshirika mwenye maono'
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na kutuma salamu za rambi rambi kwa mjane Janet Magufuli, serikali na watu wa Tanzania.
Rais Kenyatta amesema Magufuli alikuwa was kiongozi wa Afrika mwenye maono. ‘Nimempoteza rafiki, mwenzangu na mshirika wa karibu, alisema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametangaza siku saba ya maombolezo kitaifa nchini Kenya kwa heshima ya hayati Rais John Magufuli.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bendera ya Kenya zitapeperushwa nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali nchini Kenya na katika balozi zake nje ya nchi, hadi siku Magufuli atakapozikwa.