Mama Samia: Rais Magufuli anawasalimia sana
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi, Esther Namuhisa and Asha Juma
Babu Owino: Mahakama yakataa ombi la kufuta kesi ya jaribio la mauaji dhidi ya mbunge maarufu Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbunge Babu Owino nchini Kenya amepata pigo baada ya mahakama kupinga ombi la kutupilia mbali kesi ya jaribio la mauaji dhidi yake.
Mahakama moja mjini Nairobi imetupilia mbali ombi la DJ Evolve la kutaka itupilie mbali kesi dhidi ya mbunge Babu Owino kwa madai kwamba amemsamehe na anataka kuangazia uponaji wake.
Hakimu Mkuu Bernard Ochoi amesema kuwa kujiondoa tu mwenyewe sio jambo stahiki katika kesi ambayo mbunge huyo anashitakiwa kwa makosa ya kumpiga risasi Felix Orinda maarufu kama DJ Evolve.
Hakimu mkuu Benard Ochoi Jumatatu amesema kwamba ombi hilo halikufikia mahitajika yanayotakikana ili kesi hiyo iweze kutupiliwa mbali kwa sasa.
Lakini hakimu Ochoi amesema fursa ya majadiliano zaidi bado iko wazi.
Hakimu Ochoi amesema hawezi kutupilia mbali kesi hiyo kwasababu hajui Babu Owino amempa nini DJ Evolve.
"Kujiondoa tu mwenyewe sio sahihi katika hali kama ya kesi hii; wahusika wote wanastahili kujitokeza wazi kuambia mahakama kile ambacho Babu ametoa kwa ajili ya fmailia," Ochoi amesema.
Mwaka jana mbunge huyo alishitakiwa kwa makosa ya jaribio la kuua kwa kukusudia dhidi ya DJ Evolve katika klabu B.
Aliachiwa huru kwa dhamana.
Iwapo atapatikana na hatia, mbunge huyo anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.
Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa na wengi katika mitandao ya kijamii nchini kenya ambo wanakiu ya kutaka kujua hatma ya kesi hiyo.
Soma zaidi:
Wanafunzi wa shule ya msingi watekwa nyara

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaume waliokuwa na silaha wameteka nyara wanafunzi kadhaa wa shule ya msingi na walimu wao kaskazini mashariki mwa Nigeria jimbo la Kaduna, siku kadhaa tu baada ya wanafunzi wengine wa chuo kutekwa nyara katika jimbo hilo.
Wakaazi wamezungumza na BBC na kueleza kwamba waliowateka nyara walivamia shule ya serikali katika kijiji cha Rema, eneo la Birnin-Gwari, Jumatatu asubuhi walipokuwa wanawasili kwa masomo yao kama kawaida.
Bado haijafahamika waliotekwa nyara ni wangapi.
Mamlaka imesema inafuatilia kujua ni watoto wangapi na walimu wao waliotekwa nyara.
Tangu mwezi Desemba, zaidi ya wanafunzi 700 wametekwa nyara na magenge ya uhalifu kote nchini Nigeria.
Lakini hii ni mara ya kwanza wanafunzi wa shule ya msingi wamelengwa.
Wanafunzi 39 wengi wao wakiwa wasichana wadogo walitekwa nyara kutoka chuo cha masuala ya misitu Alhamisi na bado wameshikiliwa mateka.
Kawaida, waliotekwa nyara huachiwa huru baada ya majadiliano na waliowateka nyara ambao mara nyingi huitisha fidia.
Wakati huo huo, maafisa wa jimbo la Kaduna walisema walitibua jaribio jingine la kuteka nyara wanafunzi wa shule ya sekondari lililokuwa limepangwa kufanyika wikendi.
Soma zaidi:
- Wasichana zaidi ya 300 wa shule ya sekondari ya Zamfara watekwa nyara Nigeria
- Boko Haram wathibitisha kuwateka wanafunzi
- Shambulio la shule Nigeria: 'Jinsi nilivyotoroka watekaji'
Mama Samia: Rais Magufuli anawasalimia sana
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Hussein
- Nafasi, BBC Africa

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Amesema kuwa rais Magufuli anawasalimia sana Watanzania na anawasihi waendelee kuchapa kazi.
‘’Mheshimiwa rais anawasalimia na anawashukuru sana sana, kwa kazi nzuri mlioifanya mwaka jana mwezi wa kumi ya kurudisha serikali ya chama cha mapinduzi madarakani, anasema tuko salama, tuchape kazi, tujenge upendo na mshikamano.’’ Anasema Samia Suluhu.
Mama Samia amewataka pia watanzania kuacha kusikiliza maneno ya watu wa nje na kuwa na umoja katika wakati huu.
‘’Nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu wa watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja ni wakati huu, si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa, uimara wa taifa letu unaleta maneno mengi.’’ Anasema Makamu wa rais Samia suluhu.
Kauli hii ya makamu wa rais inakuja wakati kukiwa na uvumi katika mitandao ya kijamii kuhusu kutokuonekana kwa rais John Magufuli.
Hadi sasa watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kusambaza uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa rais Magufuli anaumwa.
Mara ya mwisho kwa rais Magufuli kuonekanaka hadharani ilikuwa Jumamosi ya Februari 27 hali amabayo imezua fununu na maswali juu ya alipo na hali yake kiafya.
Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivunja ukimya na kueleza kuwa rais Magufuli anaendelea na shughuli zake kama kawaida na si lazima aonekane kila siku.
Soma pia taarifa nyingine:
- Kassim Majaliwa: Rais Magufuli yupo na anaendelea vizuri
- Chadema yataka serikali Tanzania 'ivunje ukimya na kueleza alipo rais Magufuli'
Bobi Wine akamatwa polisi wakiwafyatulia waandamanaji mabomu ya machozi
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Patience Atuhaire
- Nafasi, BBC News, Kampala
Mwanasiasa wa Uganda ambaye pia alikuwa mgombea urais wa chama cha upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala.
Wakati Bobi Wine anakamatwa, alikuwa anaongoza timu ya wabunge kutoka chama chake cha National Unity Platform, kufanya maandamano dhidi ya kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama chake katika kipindi cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari.
Vikosi vya usalama vilifyatua vitoza machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.
Inasemekana kwamba waliokamatwa ni pamoja na wabunge 15.
Katika mkutano uliofanyika kupitia njia ya video, Bobi Wine alitoa wito kwa wafuasi wake kutumia njia za amani kuandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi – ambayo anaendelea kudai kuwa vikosi vya usalama itoe wale wasiojulikana walipo.
Kukamatwa kwake kutokana na mkutano wa kampeni uliofanyika Novemba kulianza siku mbili baada ya maandamano ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa.
Gazeti la Uganda la Daily Monitor limeweka kwenye mtandao picha za Bobi Wine akikamatwa Jumatatu:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Nigeria yalidhibiti jaribio lingine la uvamizi wa shule

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wanafunzi 39 bado hawajulikani walipo baada ya taasisi yao kuvamiwa jimboni Kaduna Alhamisi iliyopita. Maafisa nchini Nigeria wanasema vikosi vya usalama vimefanikiwa kulidhibiti jaribio lingine la utekajinyara wanafunzi katika shambulio la usiku wa Jumapili dhidi ya shule katika jimbo la Kaduna.
Wanafunzi 39 bado hawajulikani walipo baada ya taasisi yao kuvamiwa katika jimbo hilo Alhamisi iliyopita.
Afisa wa serikali ya jimbo la Kaduna amewapongeza maaskari na wanajeshi, kwani majambazi walijihami kwa silaha hawakufanikiwa kuwateka wanafunzi wowote kutoka shule ya sekondari iliyopo viungani mwa mji wa Ikara.
"Katikati ya nyakati za usiku wa Jumamosi na ma alfajiri ya Jumapili watu wanaoshukiwakuwa majambazi walivamia Shule ya upili ya Sayansi ya Serikali, Ikara... katika jaribuo la utekaji nyara wanafunzi," Samuel Aruwan, kamishena wa usalama na masuala ya ndani wa jimbo hilo, alinukuliwa kusema na shirika la habari la AFP.
Bw. Aruwan amesema wanafunzi wote 307 katika shile hiyo wako salama.
Serikali ya Nigeria imekosolewa vikali kufuatia ongezeko la visa vya utekaji nyara mashuleni katika miezi ya hivi karibuni.
Mamlaka haijatoa tamko lolote kuhusiana na video ambayo umesambazwa mitandaoni na wavamizi hao kupitia akaunti ya mitandao ya kijamii ya wanafunzi waliotekwa Alhamisi iliyopita.
Watu wanne wakamatwa kwa kusambaza 'uvumi wa kuugua Rais Magufuli'
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Hussein
- Nafasi, BBC Africa

Watu wanne wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kwa madai ya kusambaza habari za uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa ikiwa ni kinyume na sheria ya makosa ya kimtandao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka jeshi la polisi nchini humo, mtu mmoja alikamatwa mkoani Iringa, mwingine jijini Dar es salaam na wawili wamekamatwa mkoani Kilimanjaro.
Watu hao wanatuhumiwa kuchapicha katika mitandao ya kijamii ikiwemo mtandao wa facebook taarifa hizo za uzushi kuwa rais Magufuli anaumwa.
‘’Tutaendelea kuchukua hatua kali sio tu kwa wanaosambaza taarifa za uongo za rais Magufuli bali zozote zitakazobainika ni za uongo’’ amesema kamanda msaidizi wa polisi mkoa wa Iringa Rienda Millanzi.
Mara ya mwisho kwa rais Magufuli kuonekanaka hadharani ilikuwa Jumamosi ya Februari 27.
Hata hivyo mwishoni wa juma lililopita Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema kuwa Magufuli yupo na anaendelea na kazi.
Majaliwa alitahadharisha kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaofanyika juu ya afya na alipo rais Magufuli katika siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga amewataka watanzania kuacha kusikiliza maneno ya watu wa nje na kuwa na umoja.
‘’Nataka niwaambie kwamba wakati muhimu wa watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja ni wakati huu, si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa, uimara wa taifa letu unaleta maneno mengi,’’ amesema Makamu wa rais Samia suluhu.
- Kassim Majaliwa: Rais Magufuli yupo na anaendelea vizuri
- Chadema yataka serikali Tanzania 'ivunje ukimya na kueleza alipo rais Magufuli'
Ongezeko la bei ya petroli kuzua gumzo Kenya

Chanzo cha picha, Google
Hatua ya mamlaka ya udhibiti wa nishati na mafuta nchini Kenya kupandisha bei ya mafuta ya Petroli ,dizeli na mafuta ya taa imelalamikiwa miongoni mwa wakenya wanaotumia mitandao ya kijamii.
Malalamiko yamekuja baada ya kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya kudhibiti nishati na mafuta Daniel Bargoria kusema lita moja ya Petroli ,dizeli na mafuta taa imeongezwa bei kwa shilingi 7.63, 5.75, na 5.41 kwa kipindi cha kati ya tarehe 15 Machi na Aprili, 14.
Waliokerwa na ongezeko hilo la bei ya mafuta walishangazwa jinsi serikali inavyoweza kupandisha bei ya bidhaa hiyo wakati ambapo uchumi na kipato cha watu vimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la Corona.

Chanzo cha picha, Twitter
Hata hivyo baadhi ya waliotoa maoni yao mitandaoni walionekana kuwakejeli wenzao ambao wana mazoea ya kulalamika tu kwa maneno hasa katika majukwaa ya kijamii na maandamano yanapoitishwa kuonyesha kero zao hawajitokezi kushiriki katika hatua kama hizo.
Muda mfupi baada ya kutumwa kwa tangazo hilo la kuongezwa kwa bei ya mafuta, chama cha upinzani ODM kilituma taarifa kikisema kinapinga kuongezwa kwa bei ya mafuta hasa wakati huu ambapo Wakenya wengi wanakabiliwa na gharama ya juu ya maisha.

Chanzo cha picha, Twitter
Katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna amesema wakati huo sio wakati mzuri kupandisha bei ya mafuta kwa sababu janga la Corona limeathiri mapato ya watu wengi.
Mwezi uliopita mamlaka hiyo pia ilitoa tathmini nyingine iliyoongeza bei ya mafuta na ilitarajiwa na wengi kwamba tathmini ya mwezi huu ingewapa afueni kwa kupunguzwa.
Bw.Sifuna amesema serikali inafaa kuwa na utu kuhusu inavyowatoza kodi Wakenya huku akieleza kwamba anafahamu haja ya serikali kujipa pato zaidi kufadhili oparesheni na miradi mbali mbali.
‘Katika desturi za kiafrika huwezi kumkamua ng’ombe aliyekufa’ amesema Sifuna.
Museveni amshutumu Bobi Wine kuiba kura
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isack Mumena
- Nafasi, BBC Swahili Kampala

Kwa mara ya kwanza Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekituhumu chama cha siasa cha NUP kwa kuhusika na vitendo vya udaganyifu wa wizi wa kura katika zoezi la uchauzi mkuu uliofanyika tarehe 14 January 2021.
Museveni amesema madai ya Kyagulanyi yaani Bobi Wine kwamba ushindi wake katika uchaguzi mkuu ulichukuliwa na rais Museveni na kumutaka kurudisha maamuzi ya wananchi.
Katika hotuba yake usiku wa kuamukia leo rais Museveni amedai kwamba chama cha NUP kilifanya udaganyifu mkubwa katika zoezi la uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ndiyo sababu walipata kura hizo hasa katika mkoa wa kati na baadhi ya sehemu za mkoa wa Busoga na kumuonya Kiongozi wa chama cha NUP mipango yake anayopanga kufanya ya maandamano:
"Ni upande wa upinzani hususani kundi la Kyagulanyi ambao walifanya udaganyifu mkubwa kila mtu nchini Uganda anafahamu nani aliyeiba ni kundi la Kyagulanyi.Hizo kura wanazodai zaidi ya milioni tatu hazipo, kulikuwa na vitisho vilivyofanywa na wafasi wa NUP.Na sasa wapinzani wanapanga kuzuia kuapishwa rais hawawezi yoyote anayepanga jeshi litawakamata," Museveni alisisitiza.
Rais ameongeza kumlaumu Kyagulanyi kwa kuwashauri vijana kufanya vitendo vya uhalifu ndiyo sababu wamewekwa mbaroni na vyombo vya usalama.
Uholanzi kusitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca

Uholanzi nayo imeamua kusitisha matumizi ya chanjo ya corona ya Oxford-AstraZeneca kwa kuhofia kuwa na madhara.
Serikali ya Uholanzi imeamua kuchukua hatua hiyo mpaka Machi 29 ili kuchukua tahadhari.
Awali Jamuhuri ya Ireland ilichukua uamuzi huohuo kwa kuhofia hatari ya watu kuganda damu baada ya kupata chanjo hiyo nchini Norway.
Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.
Shirika la madawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema awali kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kugada kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake.
Denmark, Norway, Bulgaria, Iceland na Thailand pia wamesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca.
Soma zaidi
Mseveni: Kwanini sijapewa chanjo ya corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Uganda' Yoweri Museveni amesema bado anaangalia ni chanjo ipi atakayochomwa, siku chache baada serikali yake kuanza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa wananchi.
Tayari marais wengine barani Afrika wameonesha kwa umma wakipata chanjo ili kuhakikishia usalama na ubora wa chanjo.
Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutosha ". Aisema mke wake, Janet Museveni,pia bado hajapata chanjo hiyo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwezi uliopita Waziri wa afya wa nchini humo Jane Aceng , alikanusha taarifa kuwa rais na watu wake wa karibu walikuwa wanapokea chanjo nyingine kwa siri kabla ya taifa hilo kupokea chanjo rasmi.
Alitoa ufafanuzi baada ya gazeti la nchini humo la Daily Monitor na gazeti la Marekani la jarida la Wall Street.
Aidha rais Museveni amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kwa kuandika barua kwenye kurasa ya mbele ya gazeti au atawafuata.
Uganda ina mpango wa kutoa chanjo kwa 49.6% ya idadi ya watu katika awamu ya kwanza.
Nchi hiyo imepokea dozi 864,000 za chanjo kutoka Covax mapema mwezi huu na inatarajia kupokea nyingine 2,688,000 mwishoni mwa mwezi Juni.
- Hakuna sababu ya kusitisha kutumia chanjo ya AstraZeneca - WHO imesema
- Viongozi waliochanjwa chanzo ya corona moja kwa moja kwenye televisheni
- DRC wataka kujihakikishia usalama wa chanjo
Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya BBC Swahili, leo ikiwa Jumatatu tarehe 15.03.2021


