Mbunge Babu Owino kuendelea kusalia rumande

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa upinzani Paul Ongili maarufu kama Babu Owino ameshtakiwa kwa makosa ya jaribio la kuua kwa kukusudia mjini Nairobi.
Hakimu mkuu Francis Andayi, ameagiza mbunge huyo Babu Owino asalie kizuizini kwa siku saba zaidi hadi kesi ya ombi la kutaka kuachiliwa kwa dhamana itakaposikilizwa.
Kilichojiri
Mbunge Owino amelala korokoroni wikendi iliyopita, na hii leo Jumatatu, amefikishwa katika mahakama ya milimani na kukanusha mashtaka ya jaribio la kuua kim
aksidi. Mbunge huyo kijana mwenye ushawishi, alikamawa na polisi baada ya madai ya kumpiga risasi deejay mmoja katika B Klabu mtaani kilimani Nairobi usiku wa manane Ijumaa iliyopita.
Deejay anaendelea kupata matibabu katika hospitali moja mjini Nairobi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolea risasi iliyokuwa amepigwa shingoni mwake.
Hata hivyo, babu Owino amekanusha mashtaka hayo huku jaji Francis Andayi akisema kwamba, ataendelea kuzuiliwa akidai kuwa mbunge huyo ana uwezo wa kuwashurutisha au kutatiza mashahidi katika kesi hiyo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Iwapo atapatikana na hatia, mbunge huyo anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.
Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa na wengi katika mitandao ya kijamii nchini kenya ambo wanakiu ya kutaka kujua hatma ya kesi hiyo.
Kesi ya Babu owino inawadia wakati ambao polisi imetangaza kwamba haitatoa tena ulinzi kwa viongozi wa serikali ambao wanakabiliwa na kesi za uhalifu hadi watakapofutiwa mashtaka yao na mahakama.
Aidha, viongozi kama hao ambao wanamiliki silaha leseni zao zitafutwa na silaha zao kuchukuliwa.












