Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mamia ya wakazi wa Nkuhungu Dodoma waathirika na mafuriko
Mamia ya wakazi wa eneo la Nkuhungu lililopo jijini Dodoma nchini Tanzania wamejikuta bila makazi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi and Dinah Gahamanyi
Mamia ya wakazi wa Nkuhungu Dodoma waathirika na mafuriko
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC News, Dodoma
Mamia ya wakazi wa eneo la Nkuhungu lililopo jijini Dodoma nchini Tanzania wamejikuta bila makazi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Waathirika wa mafuriko hayo wamesema kutokuwepo kwa miundombinu kama vile mitaro ya maji ndio chanzo cha mafuriko, hivyo kuitaka serikali kuweka miundombinu ili madhara zaidi yasitokee.
Hali ya taharuki na fadhaa imewakumba wakazi wa maeneo haya ya Nkuhungu yaliyopo nje kidogo na jiji la Dodoma.
Sehemu kubwa ya makazi ya watu yameharibika na mengine kumezwa na maji.
Familia kadhaa zilizoachwa bila makazi zimelazimika kutafuta hifadhi sehemu nyengine hasa katika nyumba ambazo hazijakwisha maarufu kama mapagale, huku wakikosa uhakika wa maisha ya baadae.
Paulo Lazaro Yohana ni miongoni mwa waathirika wa mafuriko na anasema mpaka sasa hana pa kuishi.
“Naishi kwenye pagale, mtu anakuambia chumba elfu 40, na anataka miezi sita, kwa kweli ni athari kubwa sana, tunahangaika na watoto. Miaka yote maisha yalikuwa mazuri, mambo yalianza kuharibika mwaka jana na mwaka huu, baada ya haya ma karavati kuelekezwa maji huku na hivi mvua zinazonyesha ndio zimeleta mafuriko,” anasema Paulo, mkazi wa Nkuhungu, Dodoma.
Nae Hadija Ramadhani Mshirai anasema, tangu mwaka jana wamekuwa wakihama na watoto hivyo, kuiomba serikali kuwasaidia katika uwekaji wa miundombinu.
Tofauti na walioamua kutafuta hifadhi, kwa Bona Augostina Shayo ameamua kuendelea kuishi katika nyumba ambayo nusu umebomoka kutokanana mafuriko.
Ingawa sehemu ya nyumba iliyobaki inaonekana kutokuwa salama kwa sababu wakati wowote inaweza kuporomoka, lakini anasema, hana sehemu nyengine ya kwenda kuishi, hivyo ataendelea kuishi hapo hapo.
Wengi wanasema chanzo cha mafuriko hayo ni kukosekana kwa miundombinu thabiti pamoja kuwepo kwa mitaro inayotiririsha maji ya mvua kwenye makazi ya watu.
Akilitolea ufafanuzi suala hilo, Joseph Mafuru ambae ni mkurugenzi wa jiji la Dodoma amesema tayari ofisi yake inaishughulikia changamoto hiyo.
“Tumekuja na option ya tatu, tuyazuie maji yanayotoka Mlima Itega. Sisi kama jiji mkakati wa haraka, moja tumewaandalia viwanja, kwa sababu lazima tuwe na ufumbuzi kwa sababu kama bilioni 14 zitakosekana, tumeandaa viwanja katika eneo la Mahungu, viwanja vyote vimepimwa, tunatafuta utaratibu ili tuweze kuwapeleka pale,” amesema Mafuru.
Licha ya kauli hiyo ya mkurugenzi, waathirika hawa, wanaonekana kutokubaliana nayo, huku wakisisitiza kwamba eneo wanaloishi ni salama, hivyo kuitaka serikali kutafuta ufumbuzi mwengine ikiwemo kuchimba mitaro ya kuchepusha maji tofauti na kuwahamisha.
Rahma Abdurahmani Injimaa ambae ni mkazi wa Nkuhungu anasema, msaada pekee kutoka kwa serikali ni ujenzi wa miundombinu.
“Endapo serikali itatusaidia kuweka mtaro sisi tutakuwa salama, na ndio jambo tunalolililia. Hatuhitaji kupewa viwanja wala malipo, sisi tunahitaji miundombinu,” amesema Rahma.
Meli iliyobeba dozi za chanjo zaidi ya milioni 200 yawasili Nigeria
Mkuu wa Shirika la Afya duniani (who), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema zaidi ya dozi milioni 200 za chanjo ya AstreZeneca zinatarajiwa kupelekwa kwenye nchi 142 ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei.
Dozi hizo zitawasilishwa chini ya mpango wa Covax unaotoa bure chanjo hizo kwa nchi masikini.
Meli iliyobeba chanjo karibu milioni nne ya virusi vya corona imewasili nchini Nigeria-nchi ya tatu Afrika magharibi kupokea chanjo chini ya mradi wa Covax baada ya Ghana na Ivory Coast ambapo kampeni za chanjo sasa zimeanza.
Dkt Tedros amesema kuwasili kwa chanjo pia kulipangwa siku ya Jumanne kwa nchi za Angola, Cambodia, Jamuhuri ya demokrasia ya Congo.
Makamu mpya wa rais Zanzibar aapishwa
Makamu mpya wa rais wa kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania ameapishwa chini ya wiki mbili baada ya mtangulinzi wake kufarilki.
Othman Sharrif anachukua mahala pake Seif Sharrif Hamad aliyefariki tarehe 17 Februari akiwa na umri wa miaka 77.
Hakuna sababu rasmi iliotolewa kuhusu kifo chake lakini kinajiri wiki tatu baada ya chama chake kusema kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.
Bwana Masoud hapo awali amehudumu katika nyadhfa kuu katika serikali ya Zanzibar aikiwemo mwanasheria mkuu.
Sherehe ya kumuapisha kisiwani Zanzibar ilichapishwa katika mtandao wa You Tube .
Kamanda mpya achukua usukani wa majeshi ya Kenya AMISOM
BrigediaJeff Nyagahamechukua usukani kama kamanda wasekta ya pili ya wanajeshi wa Kenya katika kikosi cha kulinda Amani nchini Somalia ,Amisom .
Nyagah ameichukua nafasi hiyo kutoka kwa BrigediaPaul Njemakatika sherehe ndogo ya kupokezana usukani iliyofanywaDhobley nchini Somalia .
Idara ya jeshi nchini Kenya imesema Brigedia Njema alikuwa kamanda wa kikosi cha tisacha KDF kinachohudumuchini ya Amisomna BrigediaNyagah sasa atasimamaia oparesheni zakikosi cha kumi cha Amisom cha KDF .
Brig Njema amesema wanajeshi wa KDFwamefaulu kulianya dhaifu kundi la Al Shabaabkatika eneo hilona kuhimiza juhudi zaidi ili kulimaliza nguvukabisa kundi hilo la kigaidi ili kurejesha amani ya kudumu nchini Somaliana kanda hii .
Brig Nyagah ameahidi kuendelea kufanya oparesheni maalum zinazolenga uwezo wa Al shabaabna pia kuzidisha ushirikiano kati ya wanajeshi wa Kenya na maafisa wa usalama wa Somalia .
Kenya iliwatuma wanajeshi wake nchini SomaliaOktoba mwaka wa 2011baada ya msururu wa utekaji nyara uliowalenga watalii na kudai kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaabkatika eneo la pwani na kaskazini mashariki mwa Kenya .
Nigeria kupokea dozi milioni 3.92 za AstraZeneca
Nigeria inajiandaa kupokea dozi milioni 3.92 za chanjo ya AstraZeneca Covid-19 Jumanne.
Ni nchi ya tatu Afrika Magharibi kupokea chanjo hiyo kutoka kupitia mpango wa Covax - ambao unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhakikisha usambazaji sawa wa chanjo kote kote duniani.
Chanjo hiyo ambayo imetengezwa na Taasisi ya Serum nchini India zinatarajiwa kuwasili mji mkuu, Abuja, Jumanne ya leo.
Nchi hiyo inatarajia kupata jumla ya dozi milioni ya 16 za chanjo ya ambazo zitatolewa kwa awamu katika kipindi cha miezi kadhaa.
Shirika la Maendeleo na Huduma ya Afya Msingi nchini Nigeria limesema wahudumu wa afya watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza watakaopokea chanjo hiyo.
Serikali ina mpango wa kuwachanja walau asilimia 20 ya watu walio na miaka 18 na zaidi katika awamu nne ndani ya miaka miwili.
Kufikia sasa Nigeria imethibitisha kuwa na zaidi ya watu 150,000 waliambukizwa Covid-19. Karibu watu 2,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Amnesty yasema 'uhalifu wa kivita' ulifanywa Msumbiji
Shirika la Amnesty International limechapisha ripoti inayolaumu majeshi ya Msumbiji, wajezi wa kijeshi kibinafsi na wanamgambo wanaohudumu katika Mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado kwa kutekeleza uhalifu wa kivita.
“Wote watatu walifanya uhalifu wa kivita, kusababisha vifo vya mamia ya raia.
"Jamii ya kimataifa ilikosa kushughulikia mzozo ambao uligeuka kuwa vita kamili vya silaha kwa miaka mitatu iliyopita,” anasema Deprose Muchena, Amnesty Mkurugenzi wa kanda ya mashariki na kusinimwa Afrika.
Shirika hilo la kutetea haki limetoa wito kwa pande zote husika kukoma mara moja kuwalenga raia na kuishinikiza serikali ya Msumbiji kuchunguza maovu hayo.
Mwaka jana, videomkadhaa zilisambazwa mitandao zikidai kuonesha jinsi maaskari walivyowadhulumu watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo na wakazi wakati wa oparesheni yao Cabo Delgado.
Msumbiji imekuwa ikikabiliana na wanamgambo tangu Oktoba mwaka 2017 ambapo zaidi ya watu 2,300 wameuawa na wengine zaidi ya 600,000 kufurushwa makwao.
Maelezo zaidi:
- Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?
Padre aliyewanyanyasa watoto kingono afia gerezani
Padri wa zamani wa Kanisa Katoliki ambaye alifungwa jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto watatu pamoja na mwanafunzi aliyekuwa akisomea upadri amefariki jela.
Paul Moore, ambaye alikuwa na umbri wa miaka, alitekeleza uhalifu huo katika maeneo tofauti mjini Ayrshire kati ya mwaka 1977 na 1996.
Alifungwa miaka tisa jela kufuatia uchunguzi wa BBC, lakini kifungo hicho kilipunguzwa hadi miaka minane na majaji wa mahakama ya rufaa.
Uhalifu wa Moore ulichukua zaidi ya miaka 20 kujulikana na mmoja wa wahasiriwa alikuwa na miaka mitano.
Msemaji wa Dayosisi ya Galloway alisema: “Askofu Nolan ataombea roho ya Paul Moore msamaha na amani kwa wale walioteseka katakana na kitendo chake.
Othman Masoud: Hakuna anayeweza kukidhi vigezo wala viwango vya Maalim
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud ameapishwa rasmi leo kuchukua wadhifa huo mpya baada ya kifo cha mtanfulizi wake Maalim Seif.
Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika katika Ikulu ya Zanzibar saa nne kwa saa za Afrika ya Mashariki, tukio lililotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni.
Baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake hapa jana Bw Othman Masoud alisema hakuna anayeweza kukidhi vigezo wala viwango vya mtangulizi wake Maaalim Seif. Hakuna na hatotokea, alisema.
‘’Najua shauku na hamasa zenu kwa maendeleo ya nchi yetu. Najua imani yenu kwangu, hata wale waliokuwa wakihoji juu ya uwezo wangu au kufaa kwangu kwa nafasi hii walifanya hivyo kwa nia safi na hamu ya kupata mtu atayekidhi haja’’,imesema taarifa ya hotuba yake baada ya uteuzi.
Bw Masoud anaapishwa rasmi hii leo kuchukua wadhifa huo mpya baada ya kifo cha mtanfulizi wake Maalim Seif.
Wasichana wa shule wa Nigeria walioachiliwa na watekajinyara wakutana na gavana
Gavana wa jimbo la Nigeria la Zamfara, Bello Matawalle, amekutana na kikundi cha wanafunzi ambao walikuwa wametekwa nyara Ijumaa katika shule ya bweni.
Wasichana 279 walipelekwa katika ofisi ya gavana katika mji mkuu wa jimbo Gusau kwa ajili ya kupatiwa maelezo.
Gavana Matawalle ameiambia BBC kuwa wasichana hao waliachiliwa baada ya kufanya mazungumzo na wanamgambo wenye silaha. Maafisa nchini Nigeria wamekiri kuwalipa kikombizi watekaji nyara, ili waachilie wasichana hao.
Gavana huyo alituma za kukutana na wasichana hao baada ya kuachiliwa kwenye ukurasa wake wa twitter.
Karibu katika matangazo mubashara leo Jumanne 02.03.2021