Wajumbe wa nchi
wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wanakutana mjini New York baadaye
leo kumchagua mwendesha mashita mpya wa mahakama hiyo.
Wagombea tisaikiwa ni pamoja na majaji wawili mmoja kutoka Nigeria na mmoja kutoka
Uganda, wako katika orodha ya kumrithi Mgambia Bi Fatou Bensouda, ambaye muhula
wake kama Mwendesha mashitakaMkuu wa
mahakama hiyo unamalizika mwezi Juni mwaka huu.
Bi Bensouda amekuwa Mwendesha
mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011- baada ya kuchukua nafasi ya wakili
Muargentina Luis Moreno Ocampo.
Katika muhula wake madarakani, aliweza kuwatia
hatiani washitakiwa Zaidi kuliko mtangulizi wake- na hivi karibuni ikiwa akiwa
ni muasi wa zamani wa Uganda kamandaDominic Ongwen ambaye mwezi huu alipatikana na hatia za
uhalifu wa kivita.
Hatahivyo alikabiliwa na ukosoaji mkubwa
hususan ni kuhusu kesi zake kuwalenga Waafrika. Mwezi Juni mwaka jana, Bensouda
alizuiwa kusafiri nchini Marekani wakati rais wa Marekani wa wakati huo Donald
Trump aliposaini sheria ya rais inayoweka vikwazo vya fedha dhidi yake.
Watu wengine
wanaowania nafasi ya Bensouda ni pamoja na:
1:Karim Khan- Wakili Kutoka Uingereza
2. Robert
Petit, Mwendesha mashitaka kutoka Canada
3.Susan
Okalany- Jaji kutoka Uganda
4. Morris
Anyah- Jaji kutoka Nigeria
5. Fergal
Gaynor - mwendesha mashitaka kutoka IRELAND
6. Fernandez Castresana- mwendesha
mashitaka kutoka Uhispania
7. Francesco
Lo Voi- mwendesha mashitaka kutoka Italia.
8.
Brigitte Raynaud – mwendesha mashitaka kutoka Ufaransa
9. Richard Roy – wakili kutoka Canada