Kamanda wa jeshi nchini Rwanda afariki dunia
Aliyekuwa Mkuu wa jeshi la Rwanda, Luteni Jenerali Jacques Musemakweli, amefariki "kifo cha kawaida" Alhamisi katika hospitali ya jeshi, kulingana na Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda.
"Ndio, Jenerali Musemakweli amefariki, alikuwa mgonjwa," afisa mwandamizi wa jeshi la Rwanda aliiambia BBC.
Jenerali Musemakweli aliteuliwa kuwa mkuu wa ukaguzi wa Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda mnamo Novemba 2019.
Hapo awali alishikilia nyadhifa za mkuu wa jeshi, mkuu wa walinzi wa rais na kamanda wa vikosi vya akiba.
Alikuwa mwanachama wa Rwandan Patriotic Front (RPF), kikosi cha waasi kilichoongozwa na Paul Kagame kilichoingia madarakani mnamo 1994.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe



