Wakili Héctor Cipriano Paredes amezua gumzo nchini
Peru na duniani kwa ujumla mara baada ya kufanya ngono na mwanamke mmoja wakati
kesi ikiendelea kusikilizwa kwa njia ya video mtandaoni.
Paredes alianza kuvua nguo kisha kufuatiwa na mwanamke
aliyekua nae na kuanza kufanya tendo hilo wakati mkutano huo ukiendelea
mubashara. Video ya tukio hilo imesambaa kwenye mtandao wa Twitter.
Tukio hilo lilikua likishuhudiwa moja kwa moja na
majaji, mawakili na baadhi ya wafuatiliaji wa kesi hiyo.
Paredes alikua wakili wa upande wa mshitakiwa katika
kesi iliyohusisha kundi la wahalifu linaloogopewa nchini humo.
Jaji John Chachua Torres aliyekua akiendesha kesi
hiyo, alisitisha mara moja kusikilizwa kwa kesi hiyo na kusema kuwa wakili
Paredes ameikosea heshima mahakama.
Baada ya Jaji Torres kujiridhisha kuwa ilikua ni
camera ya Paredes, aliamuru mara moja wakili huyu aanze kuchunguzwa na
asimamishwe kushiriki katika kesi hiyo.
‘’Tunashuhudia kitendo cha udhalilishaji na
kinaoneshwa moja kwa moja hapa, hivyo kitengo cha uchunguzi nataka wakili huyu
achunguzwe mara moja’’ alisema Torres.
Baada ya usikilizwaji wa kesi hiyo kusitishwa. Jaji
Torres aliongeza katika taarifa iliyotolewa kwa maandishi kuwa kuanzia
sasa wakili Paredes anatambulika kama mtu ambae ametia aibu mahakama, mawakili
wenzake na tasnia ya sheria kwa ujumla.
Hadi sasa wakili Paredes hajatoa maelezo yoyote baada
ya tukio hilo.
Mwezi Septemba , mbunge mmoja huko Argentina
alijiuzuru mara baada ya kuonekana akibusu matiti ya mwanamke wakati wa kikao
cha bunge kilichofanyika kwa njia ya mtandao wa video.