Watu zaidi ya 80 wakamatwa kwa tuhuma za 'chanjo bandia’ China

China imesema kuwa inafanya msako juu ya mtandao wa uhalifu unaotengeneza "chanjo bandia " za Covid-19 ambao umekuwa ukiendesha shughuli hii tangu mwezi Septemba.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Mike Sonko akanusha mashitaka dhidi yake

    Mike Sonko

    Chanzo cha picha, FACEBOOK/MIKESONKO

    Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko amekanusha mashitaka 12 dhidi yake, ikiwa ni pamoja na ghasia na wizi wa kutumia ghasia, wakati wa kesi yake iliyofanyika katika mahakama ya sheria ya Kiambu, viungani mwa mji mkuu Nairobi.

    Hivi karibuni Bw Sonko alidai kwamba yeye na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho alihusika katika kupanga ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa mzozo wa matokeo ya uchaguzi.

    Vyombo vya habari nchini Kenya vimekua vikiripoti juu ya kesi ya Bw Sonko kwenye mitandao yake ya kijamii kiwa ni pamoja na Twitter:

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

  2. Uganda masomo kwa wanafunzi wasio watahiniwa

    Wanafunzi

    Serikali ya Uganda imekubali kufungua tena shule kwa ajili ya wanafunzi wasio watahiniwa isipokua wanafunzi wa madarasa ya chekechea, vimeripoti vyombo vya habari nchini Uganda.

    Hatua hii inakuja baada ya serikali kufungua masomo kwa wanafunzi wanaojiandaa mitihani ya kitaifa.

    Hata hivyo shule za chekechea zitaendelea kufungwa kutokana na kile serikali imesema watoto hao hawawezi kufuata kiwango cha maagizo yaliyowekwa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona .

    Aidha serikali ya Uganda imesema kuwa watoto wa shule za chekechea wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mfumo wa kupumua ikiwa ni pamoja na COVID na masomo ya wanafunzi hao wanafunzi na waalimu pamoja na wazazi kukaribiana na hivyo kuongeza hatari ya maambukizi

    Serikakali ilisema kuwa Wizara ya elimu na ile ya afya watafanya ziara katika shule mbali mbalikote nchini kuangalia maandalizi kwa ajili ya kufunguliwa kwa masomo.

    Uganda sawa na mataifa mengine duniani ilifunga shule mwaka jana kufuatia janga la Covid-19.

  3. Wanaharakati wa Zimbabwe wakamatwa

    Wanaharakati wa upinzani ncini Zimbabwena mbunge wamekamatwa kwa kutumia lugha ya matusi na chafu dhidi ya maafisa wa polisi

    Polisi ilisema watatu hao wamekamatwa baada ya kufanya maandamano nje ya jengo la serikali katika mji mkuu Harare.

    Haijafahamika wazi yalikuwa ni maandamano gani yaliyofanyika siku ya Jumatatu.

    " Polisi yaJamuhuri ya Zimbabwe imethibitisha kukamatwa kwa Mbunge, Netsai Marova na Cecilia Chimbiri mjini Harare baada ya maandamano yaliyofanyika katika jengo la serikali - New Government Complex.

    " Watatu hao, ambao walikuwa katika gari la aina ya ToyotaToyota Fortuner ambayo haikuwa na namba, walifuatwa na gari la polisi lililokua na maafisa wa polisi na kutumia lugha chafu na matusi jambo lililofanya," taarifa ya polisi ilisema.

    Watatu hao, wote kutoka chama cha Democratic Change (MDC) , walikamatwa mwezi Juni mwaka jana kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu kuteswa katika mahabusu.

    Walidai maafisa wa usalama waliwateka nyara kutoka polisi, kuwachapa na kuwanyanyasa kingono na kuwalazimisha kunywa mikojo ya kila mmoja wao.

    Polisi ilikanusha shutuma hizo, lakini wataalamu wa Umoja wa Mataifa walitoa wito wa kushitakiwa kwa ‘’wahusika wa uhalifuhuo’’ .

    Chama cha MDC kimetweet kwamba kukamatwa kwao kwa hivi karibuni ni muendelezo wa kuongezeka kwa ‘’vita vya serikali dhidi ya wanaharakati ":

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Aonekana akifanya ngono wakati shughuli za mahakama zikiendelea

      • Author, Munira Hussein
      • Nafasi, BBC Africa, Swahili
    Ngono

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wakili Héctor Cipriano Paredes amezua gumzo nchini Peru na duniani kwa ujumla mara baada ya kufanya ngono na mwanamke mmoja wakati kesi ikiendelea kusikilizwa kwa njia ya video mtandaoni.

    Paredes alianza kuvua nguo kisha kufuatiwa na mwanamke aliyekua nae na kuanza kufanya tendo hilo wakati mkutano huo ukiendelea mubashara. Video ya tukio hilo imesambaa kwenye mtandao wa Twitter.

    Tukio hilo lilikua likishuhudiwa moja kwa moja na majaji, mawakili na baadhi ya wafuatiliaji wa kesi hiyo.

    Paredes alikua wakili wa upande wa mshitakiwa katika kesi iliyohusisha kundi la wahalifu linaloogopewa nchini humo.

    Jaji John Chachua Torres aliyekua akiendesha kesi hiyo, alisitisha mara moja kusikilizwa kwa kesi hiyo na kusema kuwa wakili Paredes ameikosea heshima mahakama.

    Baada ya Jaji Torres kujiridhisha kuwa ilikua ni camera ya Paredes, aliamuru mara moja wakili huyu aanze kuchunguzwa na asimamishwe kushiriki katika kesi hiyo.

    ‘’Tunashuhudia kitendo cha udhalilishaji na kinaoneshwa moja kwa moja hapa, hivyo kitengo cha uchunguzi nataka wakili huyu achunguzwe mara moja’’ alisema Torres.

    Baada ya usikilizwaji wa kesi hiyo kusitishwa. Jaji Torres aliongeza katika taarifa iliyotolewa kwa maandishi kuwa kuanzia sasa wakili Paredes anatambulika kama mtu ambae ametia aibu mahakama, mawakili wenzake na tasnia ya sheria kwa ujumla.

    Hadi sasa wakili Paredes hajatoa maelezo yoyote baada ya tukio hilo.

    Mwezi Septemba , mbunge mmoja huko Argentina alijiuzuru mara baada ya kuonekana akibusu matiti ya mwanamke wakati wa kikao cha bunge kilichofanyika kwa njia ya mtandao wa video.

  5. Virusi vya corona: Watu zaidi ya 80 wakamatwa kwa tuhuma za 'chanjo bandia’ China

    Chanjo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    China imesema kuwa inafanya msako juu ya mtandao wa uhalifu unaotengeneza "chanjo bandia " za Covid-19 ambao umekuwa ukiendesha shughuli hii tangu mwezi Septemba, imeripoti taarifa ya CNN.

    Idara a polisi za Jiangsu, Beijing na Shandong zimewakamata zaidi ya watu 80 waliohusika katika utengenezaji wa zaidi ya dozi 3,000 bandia za chanjo ya Covid-19 , Shirika la habari la taifa hilo Xinhua limeripotiwa kusema.

    Xinhua limesema wizara ya usalama wa umma nchini Uchina inachunguza uhalifu unaohusiana na utengenezaji na mauzo ya chanjo hizo bandia " na uengenezaji haramu wa dawa na ufisadikatika sekta ya chanjo."

    Polisi walibaini kuwa tangu Septemba 2020, wahusika wa chanjo "wamekua wakipata faida kubwa kwa kujaza mchanganyiko wenye chumvi ndani ya sindano ili kutengeneza chanjo bandia za virusi vya corona na kuziuza kwa bei ghali," Xinhua limeripotiwa kusema.

    China imekuwa ikiwachanja watu wake kwa dawa kutoka makampuni mawili ya Sinovac na Sinopharm, na chanjo zake pia zimekwishaanza kutolewa katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Uturuki.

  6. Bunge la DRC laanza kampeni ya kumchagua Spika

    Bi Jeanine Mabunda kutoka chama  Joseph Kabila, aling'olewa madarakani  kwa ya kutokuwa na imani nae

    Chanzo cha picha, MBELECHI MSOCHI

    Maelezo ya picha, Bi Jeanine Mabunda kutoka chama Joseph Kabila, aling'olewa madarakani kwa ya kutokuwa na imani nae

    Kampeni za uchaguzi wa Spika mpya wa Bunge la Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo zimeanza.

    Hii ni baada ya kufuzwa kwa aliyekua spika wa bunge hilo Bi Jeanine Mabunda aliyekuwa mwanachama wa chama cha rais wa zamani Joseph Kabila.

    Bi Jeanine aliondolewa kwenye kiti cha spika baada ya wabunge kupiga kura ya kutokua na imani naye.

    Lakini baadhi ya wabunge wengi wanaomuunga mkono Bw Kabila na wengine waliomuunga mkono Rais Felix Tshikekedi wanaomba Mahakama kuu ya katiba kusimamisha uchaguzi huu kutokana na kile kilichoonekana kuwa majina mengi ya wagombea yalikataliwa.

  7. Uwindaji haramu wa Faru wapungua

    rhino

    Serikali ya Afrika Kusini imeripoti kupungua kwa idadi ya faru wanaouwawa na wawindaji haramu nchini humo.

    Maafisa wanasema sehemu kubwa ya matokeo hayo ni kutokana na vikwazo vilivyowekwa vya kudhibiti covid 19.

    Waziri wa mazingira nchini humo amesema kwamba karibu faru 394 ndio waliuawa mwaka jana ikilinganishwa na faru 594 waliouwawa mwaka 2019.

    Agizo la kusalia nyumbani limesababisha harakati za uwindaji haramu wa faru na usafirishaji wa pembe zao kupungua kwa kiasi kikubwa.

    Marufuku ya kutoka nje kumeweza kuzuia harakati za watakao kuwa wawindaji haramu na wasafirishaji wa pembe za faru, iliongeza.

    Ni mwaka wa sita sasa matukio ya uwindaji haramu yanarekodiwa kupungua nchini humo.

    Lakini watunza mazingira wanaonya kuwa idadi ya faru nchini Afrika Kusini imepungua katika miaka ya hivi karibuni na kwamba ujangili bado ni shida kubwa.

    Waziri wa Mazingira Barbara Creecy amesema kuwa wakati "mikakati ya kukabiliana na vita dhidi ya janga la Covid-19" zilichangia kupunguza ujangili kwa mwaka 2020, ulinzi , wafanyakazi wa usalama na juhudi za serikali kushughulikia suala hilo pia ilikuwa na jukumu muhimu.

    Lakini watunza mazingira wanasema kwamba kumekua na upungufu wa faru kwa asilimia 70% katika hifadhi ya Kruger - ambapo ujangili mwingi umefanyika kwa takribani muongo mmoja uliopita.

    Dk Jo Shaw wa World Wide Fund for Nature (WWF) nchini Afrika Kusini amesema kuwa wakati wakishangilia kupungua kwa idadi ya faru waliopotea kutokana na ujangili, "tunafahamu sana kuwa kupungua kwa ujangili kulikochochewa na vizuizi vilivvyowekwa ilikua tu suluhu la muda mfupi.

  8. Jeshi la Uganda lakemea ujumbe wa vitisho mitandaoni

      • Author, Isack Mumena
      • Nafasi, BBC Swahili Kampala
    COVI

    Jeshi la polisi nchini Uganda limeonya watu wanaosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wakitishia wananchi na kuleta hofu nchini humo.

    Ujumbe huo ulianza kusambwa mwishoni mwa juma, ambapo ulitaka watu wabaki nyumbani kwa siku tatu ujumbe ambao wameuita 'National Shut down'.

    Ujumbe huo unawaonya wananchi kuanzia Februari 03 hadi tarehe 7 Februari wasalie nyumbani kwao bila kufanya kitu chochote.

    Naibu wa jeshi la polisi nchini humo IGP Meja Jenerali Paul Oketch ametowa onyo kwa watu aidha makundi yanayosambaza vitisho hivyo kuacha mara moja kuwatisha wananchi la sivyo watachuliwa hatua kali za kisheria.

    Vitisho hivi vinakuja wakati taifa hilo likiwa na mgawanyiko wa kisiasa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais baada ya Rais Museveni kutangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa mshindi na kuongoza taifa hilo kwa muhula wa sita.

    Ingawa Jumatatu kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine aliwasilisha kesi mahakama ya juu kupinga ushindi wa Rais Museveni.

    Hata hivyo kumekuwa na msukumo toka kwa baadhi ya viongozi wa dini wakiomba Rais Museveni kufanya maridhiano na viongozi wa upinzani kwa maendeleo ya taifa.

  9. Miko Sonko kufikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za ghasia

    Gavana sonko

    Chanzo cha picha, FACEBOOK/MIKESONKO.

    Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani, huku wapelelezi wakitaka kupata muda zaidi kumuwajibisha juu ya madai ya kuhusika kwake katika ghasia za uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya.

    Hivi karibuni Bw Sonko alidai kwamba yeye na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho alihusika katika kupanga ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa mzozo wa matokeo ya uchaguzi.

    Mike Sonko

    Chanzo cha picha, FACEBOOK/MIKESONKO

    Jumatatu gavana huyo wa zamani alijiwasilisha binafsi katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma (DCI) baada ya kutaka agizo la mahakama la kumzuia kushitakiwa bila mafanikio.

    Wakili wake,John Khaminwa, alisema Mahakama ya juu ilitupilia mbali ombi kutaka mahakama isitishe kesi yake , na kumlazimisha Bw Sonko kujisalimisha katika makao makuu ya DCI.

    Sonko alitaka mahakama itoe agizo lake dhidi ya uamuzi wa Naibu Inspekta mkuu wa polisi na Mkuu wa upelelezi wa DCI John Kariuki wa kumtaka arekodi taarifa kuhusiana na ghasia alizodai kuzifanya katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2017.

    Katika ombi lake, Sonko alidai kwamba kuitwa kwake na DCI kulikua ni njama za kutaka akamatwe na polisi.

  10. Habari...Karibu kwenye kurasa yetu ya matangazo ya moja kwa moja ya BBC Swahili