Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Wapinzani wapoteza ngome zao

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema Freeman Mbowe ni miongoni mwa viongozi waliopoteza majimbo yao .

Moja kwa moja

Asha Juma and Esther Namuhisa

  1. Na hapa ndio mwisho wa matangazo mubashara, tukutane tena hapo kesho.Shukrani

  2. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:Ubalozi wa Marekani wataka kero za uchaguzi zishughulikiwe

    Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tamko kwa wadau wote wa shughuli za uchaguzi, kushughulikia kero zilizotolewa na upinzani kwa uwazi ili kurudisha uaminifu na kuimarisha heshima kwa utawala wa sheria na utawala bora.

    Tamko hilo limetolewa baada ya vyama vya upinzani kutoa madai kuhusu udanganyifu katika uchaguzi huu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Hata hivyo hapo jana Tume ya uchaguzi ya Taifa NEC ilisema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na haijapokea rasmi malalamiko yoyote kuhusu uchaguzi huo.

  3. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Maalim Seif atangazwa kuwa mshindi wa pili wa urais Zanzibar

    vv
  4. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Hussein Mwinyi atangazwa mshindi Zanzibar

    tanzania
  5. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Hussein Mwinyi rais mteule Zanzibar

    Mwinyi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tume ya uchaguzi Zanzibar imemtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa urais Zanzibar.

    Mgombea wa chama tawala cha CCM Husein Mwinyi atangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87%.

    Baada ya kutangazwa mshindi Dkt.Mwinyi ameshukuru Wazanzibari na kusema;

    "Mimi Hussein Mwinyi si bora kuliko CCM ushindi huu ni wa Wazanzibari wote ,uchaguzi sasa umekwisha turudi kujenga Zanzibar mpya".

    Ushindi huu umetangazwa wakati Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye ni mgombea wa urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Seif Sharif Hamad akiwa amekamatwa kwa mara pili.

    Maalim

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maalim Seif alikamatwa majira ya asubuhi ,muda mfupi baada ya kutangaza kuongoza maandamano ya amani ili kutetea haki yao ya kidemokrasia.

    Siku ya Jumanne Maalim Seif alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na kupelekwa aliachiliwa saa kadhaa baadaye katika hatua ambayo ilishutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.

  6. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:Wafuasi wa CCM wakishangilia matokeo ya awali

      • Author, Munira Hussein
      • Nafasi, BBC Africa
    ccm
    Wafuasi wa ccm
    Wafuasi
    ccm
    ccm1
  7. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:Zitto aangushwa Kigoma Mjini

    Zitto

    Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe amepoteza jimbo la Kigoma Mjini .

    Zitto alikuwa alikuwa anatetea kiti chake katika jimbo hilo ambalo ameliongoza kwa kipindi cha miaka mitano ilopita. Awali alikuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa kipindi cha miaka 10.

    Zitto amebwagwa na mgombea wa CCM Kilumbe Ng'enda. Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Ng'enda amepata kura 27,688 huku Zitto akipata kura 20,600.

    Hata hivyo Zitto kupitia mtandao wa Twitter amedai jimbo lake "limechukuliwa kwa nguvu."

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  8. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Msanii wa Bongo Fleva Joseph Haule amepoteza ubunge

    Profesa Jay

    Chanzo cha picha, Facebook/Profesa Jay

    Msanii wa Bongo Fleva Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay wa chama cha CHADEMA ameshindwa kutetea jimbo la Mikumi, ambalo alikuwa mbunge kwa kipindi cha miaka mitano.

    Profesa Jay amepata kura 17,375 huku mpinzani wake Denis Lazaro wa chama cha CCM akiibuka mshindi kwa kupata kura 31,411.

    Profesa Jay alipata wadhfa wa ubunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro tangu mwaka 2015.

    Mwanamuziki huyo alitamba na wimbo wa 'Ndio mzee' ambao ulikuwa unaeleza namna kiongozi anaweza kutoa ahadi bila kuzitimiza.

  9. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020:Matokeo ya awali ya Urais yaanza kutangazwa

    Kura za urais zimeanza kutangazwa Tanzania

    Chanzo cha picha, TUME YA UCHAGUZI

    Maelezo ya picha, Kura za urais zimeanza kutangazwa Tanzania

    Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage ametangaza matokeo ya awali ya kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano kutoka majimbo 12 ya Njombe Mjini, Nsimbo, Misungwi, Sengerema, Mpanda Mjini, Babati Mjini, Donge, Musoma Mjini, Mahonda, Bumbwini.

    Wakati huohuo visiwani Zanzibar pia wanatangaza matokeo ya awali ya urais ya majimbo 25 ya Unguja na Pemba.

  10. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Kiongozi wa wa ACT Wazalendo Maalim Seif akamatwa tena visiwani Zanzibar

    Maalim

    Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Maalim Seif na viongozi wengine wa chama hicho wamekamatwa visiwani Zanzibar.

    Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kukamatwa kwa Maalim Seif pamoja na viongozi wengine akiwemo Makamu Mwenyekiti Juma Duni Haji na Mjumbe wa Kamati Kuu.

  11. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020:Siku tatu mfululizo mitandao ya kijamii yaendelea kuminywa

    whatsapp

    Ni siku ya tatu leo raia wa Tanzania bado wanalalamikia ukosefu wa mitandao ya kijamii jambo ambalo limefanya iwe changamoto kwao kuwasiliana na wengine au kuwasilisha maoni kwenye majukwaa mbalimbali.

    Walioathirika zaidi ni watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Twitter, WhatsApp, Instagram na YouTube.

    Shirika la Netblocks linalofuatilia usalama na usimamizi wa mtandao pia lililalamikia kuminywa kwa intaneti.

    Maelezo ya video, Uchaguzi Tanzania 2020:Watanzania wanasema nini kuhusu kuminywa kwa mitandao ya kijamii?

    Hata hivyo mtandao wa Facebook ulitoa hakikisho kwamba utaendelea kutoa taarifa kwa wapiga kura na kuimarisha juhudi zao katika kukabiliana na taarifa za uongo na muingilio wowote kwenye uchaguzi huo.

    Mtandao wa Twitter ulitoa taarifa kwa umma kuhusu kushuhudia kuminywa kwa mtandao huo nchini Tanzania wakati taifa hilo.

    Tangu mwanzoni mwa wiki, watumiaji wa WhatsApp wameshindwa kupakua picha au video.

    Jitihada za BBC kupata maelezo kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini humo (TCRA) hayakuzaa matunda.

    Watumiaji wengi wanahusisha suala hili la zuio la intaneti na uchaguzi mkuu.

  12. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:Jumuiya za Kimataifa ziingilie kati uchaguzi

    uchaguzi

    Mgombea wa urais kupitia Chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema bwana Tundu Lissu amezitaka Jumuiya za kimataifa pamoja na jumuiya za kikanda ziingilie kati taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Tanzania.

    "EAC, SADC wasitoe taarifa za kuhalalisha uharamia huu. Waseme ukweli. Watanzania waingilie kudai haki yao kwa amani kwa njia ya kidemokrasia,"Tundu Lissu amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari.

    Aidha ameongeza kusema kuwa chama chake kimeweka wagombea 244 wa ubunge nchi nzima, kati ya hao 63 walienguliwa, udiwani 3754 kati yao wagombea 1025 walienguliwa, hivyo takribani 30% walienguliwa- 'haijawahi kutokea tangu tumefanya uchaguzi wa vyama vingi nchini".

    Aliongeza kusema kuwa mbali na kuwa kulikua na changamoto ya kutokuwa na fedha, hawakuweka picha za mgombea nchi nzima lakini "watanzania walituunga mkono".

    Lissu amedai kuwa mawakala wengi wa upinzania hawakupewa barua ya kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

    "Mawakala waliobaki kwenye vituo hakuna aliyepewa nakala ya matokeo ya uchaguzi kama sheria inavyotaka,hiyo peke yake inathibitisha hakuna uchaguzi wa vyama vingi, hata kwa sheria zetu kama zilivyo huu haukua uchaguzi majimbo yote , kata zote CCM wametangaza ushindi,"Lissu alifafanua.

    Hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imekanusha madai hayo ya upinzani na kusema tuhuma zinazotolewa hazijawasilishwa rasmi.

  13. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Shamsia Mtamba ashinda kupitia CUF

    Shamsia Mtamba

    Chanzo cha picha, BUNGE LA TANZANIA

    Maelezo ya picha, Shamsia Mtamba

    Mgombea wa chama cha CUF Shamsia Mtamba ameshinda ubunge wa jimbo la Mtwara vijijini baada ya kupata kura 26,262, dhidi ya mpinzani wake Hawa Ghasia wa CCM aliyepata kura 18,505.

    Shamsia alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia chama cha CUF kabla ya kuamua kuwania ubunge jimbo la Mtwara vijijini.

  14. Uchaguzi Tanzania 2020: Priscus Tarimo ashinda ubunge wa Moshi mjini

    Priscus Tarimo

    Chanzo cha picha, INSTAGRAM

    Maelezo ya picha, Priscus Tarimo

    Mgombea wa CCM, katika Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo ameibuka mshindi katika uchaguzi wa eneo hilo.

    Tarimo alimshinda mpinzani wake wa Chama cha Chadema Raymond Mboya kwa kura 31,169 dhidi ya 22,555.

    Jimbo la Moshi Mjini lina kata 21, na kati ya kata hizo 20 madiwani wa CCM wameibuka kidedea huku CHADEMA KIshinda katika kata moja kulingana na msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi.

  15. Uchaguzi Tanzania 2020: Matokeo ya Mbeya mjini

    Tulia Ackson

    Chanzo cha picha, FACEBOKK

    Maelezo ya picha, Tulia Ackson

    Mgombea wa Chama cha mapinduzi katika jimbo la Mbeya Tulia Akson ameibuka mshindi katika uchaguzi wa eneo hilo.

    Dkt Tulia Akson alimshinda mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Chadema Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kwa kujipatia kura 75,225.

    Joseph Mbilinyi alipata kura 37, 591.

    MR TWO

    Chanzo cha picha, INSTAGRAM/MR TWO

    Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr.Two au Sugu amekuwa mbunge wa Mbeya mjini kupitia chama cha upinzani cha chadema nchini humo tangu mwaka 2010 mpaka 2020.

    Mwaka 2018, Joseph Mbilinyi alishtakiwa kwa kumtumia lugha ya fedheha dhidi ya rais Magufuli na kutumikia kifungo cha miezi mitano.

  16. Habari za hivi punde, Uchaguzi Tanzania 2020: Freeman Mbowe ashindwa kutetea kiti chake jimbo la Hai

    Kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe
    Maelezo ya picha, Kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe

    Hatimaye raia wa Tanzania wametekeleza wajibu wao wa kupiga kura katika uchaguzi wa kihostoria nchini humo.

    Kwasasa kura zinaendelea kuhesabiwa huku baadhi ya maeneo yakiwatangaza washindi.

    Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema ambaye pia alikuwa kuwa mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe ameshindwa kutetea kiti chake, baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura na mgombea wa CCM, Saashisha Mafuwe.

    Matokeo: Jimbo la Hai Mkoa wa Kilimanjaro

    Mbaruku Salehe Muhina ACT Wazalendo ….315

    Saasisha Mafuwe CCM…..89,786

    Freeman Mbowe Chadema…27,684

    Jumla ya kura zilizopigwa….101785

  17. Habari ya asubuhi wasomaji wetu. Bila shaka hamjambo, karibuni katika matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo ikiwa ni tarehe 29.10.2020.