Uchaguzi Tanzania 2020: Mitandao ya kijamii yaendelea kuminywa Tanzania
Mtandao wa Twitter umetoa taarifa kwa umma kuhusu kushuhudia kuminywa kwa mtandao huo nchini Tanzania wakati taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu.
Twitter imesema kufungwa kwa intaneti ni jambo lenye madhara na kuvunja haki za binadamu.