Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wagombea urais Tanzania warudisha fomu NEC
Rais wa Tanzania na mgombea wa urais kupitia chama tawala cha CCM, John Pombe Magufuli amerejesha fomu ya kugombea urais Tune ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Wagombea wa urais Tanzania wakirudisha fomu kwa Picha
Nchini Tanzania, wagombea wa urais kutoka vyama mbalimbali vya siasa wanaendelea kurejesha fomu na kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mnamo Oktoba 28.
Baadhi ya waliokamilisha mchakato huo ni kama wafuatao:
Mike Pompeo awasili Sudan baada ya safari ya kihistoria
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amewasili nchini Sudan kwa ndege akitoka Israel katika ziara ya kwanza yaafisa ya ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kuifanya nchini humo kwa miaka 15.
Ni afisa wa ngazi ya juu wa Marekani kuitembelea nchi hiyo tangu yafanyike mapinduzi ya kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.
Sudan inataka kuondolewa katika orodha ya Marekani ya mataifa yanayodhamini ugaidi, huku Bwana Pompeo akipigia debe uhusiano baina ya Israel na mataifa ya kiarabu.
Uhusiano baina ya Marekani na umekua mwema baada ya kung’olewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir.
Ronaldinho aachiliwa huru Paraguay
Mchezaji wa soka wa Brazili Ronaldinho ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Paraguay baada ya kufungwa kwa kumiliki paspoti gushi.
Mwezi Machi yeye na kaka yake walidaiwa kutumia paspoti gushi kuingia nchini Paraguay.
Mshindi huyo wa kombe la dunia na kaka yake wamekuwa gerezani kwa mwezi mmoja na miezi mingine minne alifungiwa katika hoteli ya kifahari iliyopo katika mji mkuu Asuncion kwa dhamana.
Pascal Lissouba afariki dunia
Rais wa zamani wa Congo/Brazaville Pascal Lissouba, amefariki dunia nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 88, chama chake kimeliambia shirika la habari la AFP.
"Rais Lissouba amekufa baada ya kuugua," Mbunge na msemaji wa chama cha Pan-African Union for Social Democracy (UPADS) Honore Sayi amesema.
Kifo chake pia kimethibitishwa kwenye ukurasa wa Facebook na mwanae wa kiume Jeremie Lissouba, ambaye pia ni mbunge.
Bwana Lissouba mbaye alishinda katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingimwaka 1992, alitoroka nchi yake na kwenda Ufaransa baada ya kupinduliwa na rais wa sasa Denis Sassou Nguesso, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.
Wanafunzi wa vyuo vilivyofungwa Rwanda waililia serikali
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili
Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo 3 vya binafsi vilivyofungwa wanaiomba serikali kuwaandalia mitihani ya kuhitimu wakidai kuwa wameashakamilisha masomo yao.
Wizara ya elimu inasema wanafunzi kutoka vyuo vilivyofungwa watatafutiwa vyuo vingine.
Serikali ilisema vyuo hivyo, University of Kibungo, College of Education na Christian University vilikua na kiwango duni cha elimu.
‘’Nilikuwa nasomea taaluma ya elimu.kwingine ambako kuna kitivo cha elimu ni mbali.kwenye mkoa wa kusini na pia mji wa Gitshumbi kaskazini...ikiwa nitasajiliwa katika moja wapo ya vyuo hivyo nitateseka sana ,gharama za safari na malazi zitakuwa juu sana’’ Pascifique Mukamana aliyekua katika Christian University aliiambia BBC
Makaimu viongozi wa vyuo hivyo wanakiri kuwepo makosa ya kiutendaji na ufujaji wa fedha.
Waalimu na watumishi wa vyuo hivyo wanadai malimbikizo ya mishahara yao, Muvunyi Pierre Celestin alikuwa mwalimu wa chuo cha Kibungo:
Serikali alisema kwamba wanafunzi kutoka vyuo hivyo watatafutiwa vyuo vingine na kwamba walimu walio na mikataba watafwata sheria ya utumishi Rwanda.
Watu wenye silaha wawauwa watu wapatao 15 kusini mwa Burundi
Takriban watu 15 wameripotiwa kuuawa na wakati watu wenye silaha walipofanya mashambulio Kusini mwa Burundi.
Mapigano hayo yaliyotokea katika wilaya ya Bugarama katika mkoa wa Rumonge yalianza Jumapili na kuendela hadi Jumatatu, yamewalazimisha watu kuzikimbia nyumba zao na kujificha kwenye misitu na vichakani .
Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii kundi la waasi lenye makao yake katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo lilisema kuwa ndilo lililofanya shambulio hilo.
Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Burndi amesema kuwa kuna uwezekano kwamba ghasia hizo zina uhusiano na kurejeshwa nyumbani kwa wakimbizi wa Burundi waliokimbilia Rwanda wakitoroka ghasia nchini mwao mwaka 2017.
Kwa picha: Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akirejesha fomu za kugomea urais
Jinsi corona ilivyogeuza shule kuwa mahala pa kufugia kuku Kenya
Uamuzi wa Kenya kufunga shule zote hadi mwezi Januari mwaka ujao kwasababu ya janga la virusi vya corona umeziacha nyingi kati ya shule za kibinafsi zikihangaika kuendeleza shughuli zake.
Madarasa katika Shule ya Mwea Brethren School, ambayo wakati mmoja yalikuwa yamejaa wanafunzi wanaosoma sasa yamejaa kuku.
Ubao wa mwalimu wa kufundishia, ambao kwa kawaida ungeweza kuandikwa maswali ya hisabati au somo lingine, umegeuzwa kuwa wa kuandika ratiba ya chanjo za kuku.
Joseph Maina, ambaye anamiliki shule hiyo eneo la kati mwa Kenya, alilazimika kugeuza madarasa kuwa eneo la mifugo ili kupata pesa za kujikimu kimaisha kwani kwa sasa hapati mapato yoyote kwa kutoa elimu.
Wagombea urais Tanzania warudisha fomu NEC
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC Africa, Dar es Salaam
Rais wa Tanzania na mgombea wa urais kupitia chama tawala cha CCM, John Pombe Magufuli amerejesha fomu ya kugombea urais Tune ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
NEC inatarajiwa hii leo kuteua wagombea watakaoshiriki uchaguzi wa Oktoba 28. Magufuli ambaye anamaliza muhula wake wa kwanza anawania miaka mitano mingine kumaliza muhula wa pili kwa mujibu wa Katiba.
Kipindi cha kampeni rasmi zitaanza Jumatano
Chana cha Mapinduzi kilituma video ya Rais Magufuli ralipokuwa akitoka katika ofisi ya tume ya uchaguzi kurejesha fomu yake:
Hii inakuja siku moja kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini, wagombea wa vyama 17 vyenye usajili wa kudumu wamechukua fomu za uteuzi wa kiti cha urais, na makamu wa rais.
Tundu Lissu atawakiisha chama kikuu cha upinzani Chadema, na Bernard Membe akipeperusha bendera ya Chama kinachoonekana kukua kwa kasi cha ACT wazalendo.
Ama kwa upande wa ubunge na udiwani, tume imesema inaendelea kukusanya taarifa za waliochukua fomu baada ya kupendekezwa na vyama vyao.
Kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi wa rais na ubunge za mwaka 2020, fomu hizo zitawekwa eneo la wazi ambapo wagombea watapata nafasi ya kuweka pingamizi.
Awali, kulikuwa na pendekezo kutoka kwa baadhi ya wananchi wakivitaka vyama vya upinzani kusimamisha mgombea mmoja, lakini mpaka sasa inaonekana ndoto hiyo kufifia.
Karibu katika matangazo mubashara leo Jumanne 25.08.2020