Wagombea urais Tanzania warudisha fomu NEC

Rais wa Tanzania na mgombea wa urais kupitia chama tawala cha CCM, John Pombe Magufuli amerejesha fomu ya kugombea urais Tune ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho ya matangazo yetu ya moja kwa moja, tukutane tena kesho.

  2. Wagombea wa urais Tanzania wakirudisha fomu kwa Picha

    Nchini Tanzania, wagombea wa urais kutoka vyama mbalimbali vya siasa wanaendelea kurejesha fomu na kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mnamo Oktoba 28.

    Baadhi ya waliokamilisha mchakato huo ni kama wafuatao:

    NEC

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateuwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa tiketi ya SAU, Bw. Mutamwega Mgaiwa na Bi. Satia Musa Bebwa.
    ADA-TADEA

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, John Shibuda kutoka chama cha ADA-Tadea pia amepitishwa na tume.
    Demokrasia Makini

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateuwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa tiketi ya Demokrasia Makini, Bi. Cecilia Augustiono Mwanga na Tabu Mussa Juma.
    NEC

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateuwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa tiketi ya NRA, Bw. Leopold Mahona na Hamid Ally Hassan.
    ccm

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, Wagombea kutoka CCM John Magufuli na Samia Hassan ndio walikuwa wakwanza kupitishwa na NEC.
    NCCR

    Chanzo cha picha, NEC

    Maelezo ya picha, Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi baada ya kupitishwa na NEC.
  3. Mike Pompeo awasili Sudan baada ya safari ya kihistoria

    Mike Pompeo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amewasili nchini Sudan kwa ndege akitoka Israel katika ziara ya kwanza yaafisa ya ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kuifanya nchini humo kwa miaka 15.

    Ni afisa wa ngazi ya juu wa Marekani kuitembelea nchi hiyo tangu yafanyike mapinduzi ya kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.

    Sudan inataka kuondolewa katika orodha ya Marekani ya mataifa yanayodhamini ugaidi, huku Bwana Pompeo akipigia debe uhusiano baina ya Israel na mataifa ya kiarabu.

    Uhusiano baina ya Marekani na umekua mwema baada ya kung’olewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir.

  4. Ronaldinho aachiliwa huru Paraguay

    Ronaldinho, kushoto,na kaka yake  Roberto de Assis Moreira wakiwa mahakamani Jumatatu

    Chanzo cha picha, ASUNCION COURTHOUSE/EPA

    Maelezo ya picha, Ronaldinho, kushoto,na kaka yake Roberto de Assis Moreira wakiwa mahakamani Jumatatu

    Mchezaji wa soka wa Brazili Ronaldinho ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Paraguay baada ya kufungwa kwa kumiliki paspoti gushi.

    Mwezi Machi yeye na kaka yake walidaiwa kutumia paspoti gushi kuingia nchini Paraguay.

    Mshindi huyo wa kombe la dunia na kaka yake wamekuwa gerezani kwa mwezi mmoja na miezi mingine minne alifungiwa katika hoteli ya kifahari iliyopo katika mji mkuu Asuncion kwa dhamana.

    Ronardinho akiingia mahakamani

    Chanzo cha picha, Getty Images

  5. Pascal Lissouba afariki dunia

    Rais Pascal Lissouba
    Maelezo ya picha, Bwana Pascal Lissouba amefariki katika mji wa kusini magharibi mwa Ufaransa wa Perpignan

    Rais wa zamani wa Congo/Brazaville Pascal Lissouba, amefariki dunia nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 88, chama chake kimeliambia shirika la habari la AFP.

    "Rais Lissouba amekufa baada ya kuugua," Mbunge na msemaji wa chama cha Pan-African Union for Social Democracy (UPADS) Honore Sayi amesema.

    Kifo chake pia kimethibitishwa kwenye ukurasa wa Facebook na mwanae wa kiume Jeremie Lissouba, ambaye pia ni mbunge.

    Bwana Lissouba mbaye alishinda katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingimwaka 1992, alitoroka nchi yake na kwenda Ufaransa baada ya kupinduliwa na rais wa sasa Denis Sassou Nguesso, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.

  6. Wanafunzi wa vyuo vilivyofungwa Rwanda waililia serikali

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
    College of Education ni moja ya taasisi zilizofungwa na serikali kwa kutoa elimu duni
    Maelezo ya picha, College of Education ni moja ya taasisi zilizofungwa na serikali kwa kutoa elimu duni

    Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo 3 vya binafsi vilivyofungwa wanaiomba serikali kuwaandalia mitihani ya kuhitimu wakidai kuwa wameashakamilisha masomo yao.

    Wizara ya elimu inasema wanafunzi kutoka vyuo vilivyofungwa watatafutiwa vyuo vingine.

    Serikali ilisema vyuo hivyo, University of Kibungo, College of Education na Christian University vilikua na kiwango duni cha elimu.

    ‘’Nilikuwa nasomea taaluma ya elimu.kwingine ambako kuna kitivo cha elimu ni mbali.kwenye mkoa wa kusini na pia mji wa Gitshumbi kaskazini...ikiwa nitasajiliwa katika moja wapo ya vyuo hivyo nitateseka sana ,gharama za safari na malazi zitakuwa juu sana’’ Pascifique Mukamana aliyekua katika Christian University aliiambia BBC

    Makaimu viongozi wa vyuo hivyo wanakiri kuwepo makosa ya kiutendaji na ufujaji wa fedha.

    Waalimu na watumishi wa vyuo hivyo wanadai malimbikizo ya mishahara yao, Muvunyi Pierre Celestin alikuwa mwalimu wa chuo cha Kibungo:

    Serikali alisema kwamba wanafunzi kutoka vyuo hivyo watatafutiwa vyuo vingine na kwamba walimu walio na mikataba watafwata sheria ya utumishi Rwanda.

  7. Watu wenye silaha wawauwa watu wapatao 15 kusini mwa Burundi

    Ramani inayoonyesha wilaya ya Rumonge

    Takriban watu 15 wameripotiwa kuuawa na wakati watu wenye silaha walipofanya mashambulio Kusini mwa Burundi.

    Mapigano hayo yaliyotokea katika wilaya ya Bugarama katika mkoa wa Rumonge yalianza Jumapili na kuendela hadi Jumatatu, yamewalazimisha watu kuzikimbia nyumba zao na kujificha kwenye misitu na vichakani .

    Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii kundi la waasi lenye makao yake katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo lilisema kuwa ndilo lililofanya shambulio hilo.

    Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Burndi amesema kuwa kuna uwezekano kwamba ghasia hizo zina uhusiano na kurejeshwa nyumbani kwa wakimbizi wa Burundi waliokimbilia Rwanda wakitoroka ghasia nchini mwao mwaka 2017.

  8. Kwa picha: Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akirejesha fomu za kugomea urais

    Rais Magufuli

    Chanzo cha picha, Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC)

    Rais Pombe Magufuli

    Chanzo cha picha, Tume ya uchaguzi Tanzania(NEC)

    Rais John Pombe Magufuli

    Chanzo cha picha, Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC)

    Rais Magufuli akiambatana na Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu kurejesha fomu ya kugombea urais

    Chanzo cha picha, Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC)

    Maelezo ya picha, Rais Magufuli akiambatana na Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu kurejesha fomu ya kugombea urais
  9. Jinsi corona ilivyogeuza shule kuwa mahala pa kufugia kuku Kenya

    Ubao wa mwalimu sasa umeandikwa ratiba ya chanjo za kuku
    Maelezo ya picha, Ubao wa mwalimu sasa umeandikwa ratiba ya chanjo za kuku

    Uamuzi wa Kenya kufunga shule zote hadi mwezi Januari mwaka ujao kwasababu ya janga la virusi vya corona umeziacha nyingi kati ya shule za kibinafsi zikihangaika kuendeleza shughuli zake.

    Madarasa katika Shule ya Mwea Brethren School, ambayo wakati mmoja yalikuwa yamejaa wanafunzi wanaosoma sasa yamejaa kuku.

    Ubao wa mwalimu wa kufundishia, ambao kwa kawaida ungeweza kuandikwa maswali ya hisabati au somo lingine, umegeuzwa kuwa wa kuandika ratiba ya chanjo za kuku.

    Joseph Maina, ambaye anamiliki shule hiyo eneo la kati mwa Kenya, alilazimika kugeuza madarasa kuwa eneo la mifugo ili kupata pesa za kujikimu kimaisha kwani kwa sasa hapati mapato yoyote kwa kutoa elimu.

  10. Wagombea urais Tanzania warudisha fomu NEC

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC Africa, Dar es Salaam
    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

    Chanzo cha picha, AFP

    Rais wa Tanzania na mgombea wa urais kupitia chama tawala cha CCM, John Pombe Magufuli amerejesha fomu ya kugombea urais Tune ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

    NEC inatarajiwa hii leo kuteua wagombea watakaoshiriki uchaguzi wa Oktoba 28. Magufuli ambaye anamaliza muhula wake wa kwanza anawania miaka mitano mingine kumaliza muhula wa pili kwa mujibu wa Katiba.

    Kipindi cha kampeni rasmi zitaanza Jumatano

    Chana cha Mapinduzi kilituma video ya Rais Magufuli ralipokuwa akitoka katika ofisi ya tume ya uchaguzi kurejesha fomu yake:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Hii inakuja siku moja kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

    Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini, wagombea wa vyama 17 vyenye usajili wa kudumu wamechukua fomu za uteuzi wa kiti cha urais, na makamu wa rais.

    Tundu Lissu atawakiisha chama kikuu cha upinzani Chadema, na Bernard Membe akipeperusha bendera ya Chama kinachoonekana kukua kwa kasi cha ACT wazalendo.

    Ama kwa upande wa ubunge na udiwani, tume imesema inaendelea kukusanya taarifa za waliochukua fomu baada ya kupendekezwa na vyama vyao.

    Kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi wa rais na ubunge za mwaka 2020, fomu hizo zitawekwa eneo la wazi ambapo wagombea watapata nafasi ya kuweka pingamizi.

    Awali, kulikuwa na pendekezo kutoka kwa baadhi ya wananchi wakivitaka vyama vya upinzani kusimamisha mgombea mmoja, lakini mpaka sasa inaonekana ndoto hiyo kufifia.

  11. Karibu katika matangazo mubashara leo Jumanne 25.08.2020