Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Miili 53 yazikwa katika makaburi ya pamoja Morogoro Tanzania

Watu 71 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogogoro, Mashariki mwa Tanzania.

Moja kwa moja

  1. Habari za hivi punde, Waliothiriwa wazungumza na BBC

    Wakazi waliojawa na hofu huenda wamepoteza wapendwa wao wamekusanyika katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro kujulia hatma ya wapendwa wao.

    Habari zaidi zinasema kuwa jamaa hao wameombwa kuondoka hospitali hapo na kurejea kesho kwa maelezo zaidi.

  2. Habari za hivi punde, Baadhi ya majeruhi wapelekwa Muhimbili

  3. Miili ya watu 60 ajali ya lori la mafuta Morogoro imehifadhiwa mochwari

    Mkuu wa Mkoa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema miili ya watu 60 waliokufa baada ya lori la mafuta kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo imehifadhiwa mochwari.

    Akizungumza Gazeti la Mwananchi Dk Kebwe amesema zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Mkoa huo wa matibabu. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea miili 60 kufikia leo saa 5:30 asubuhi na kwamba bado wanaendelea kupokea mingine.

    “Majeruhi tuliowapokea hapa 52 wanaume na wanane ni wanawake. Tumelazimika kuwaomba madaktari na wauguzi kutoka hospitali na vituo vingine vya afya katika manispaa ya Morogoro kwa kuwa leo ni mapumziko,” amesema Lyamuya.

  4. Tanzania yaomboleza

    Watu kutoka kila pembe ya Tanzania wamekuwa wakituma risala za rambi rabi kufuatia mkasa wa moto wa lori la mafuta lililolipuka mjini Morogoro Mashariki mwa Tanzania.

    Wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii ya kuwafariji wale wote waliofikwa na msiba.

    Wito unazidi kutole wa watumiaji wa mitandao hiyo wakome kusambaza picha ya miili ya watu iliyoteketea vibaya.

  5. Habari za hivi punde, Hali ilivyo katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC Africa, Morogoro

    Baadhi ya waathiwa wa mkasa wa Morogoro ambao wako katika pilka pilka za kuwatafuta wapendwa wao ambao huenda wamehusika katika ajali ya lori la mafuta wamezungumza na mwandishi wa BBC Aboubakar Famau ambaye kwa sasa yuko katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro

  6. Jamaa za walioathiriwa wawatafuta wapendwa wao

    Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau ambaye yuko katika eneo la tukou anaripoti kuwa wakazi walio na hofu huenda wamepoteza wapendwa wao wamekusanyika karibu na eneo la tukio kujulia hatma ya wapendwa wao.

    ''Nimempigia ndugu yangu simu ambaye ni mwendesha piki piki lakin hapokei simu'' alisema mmoja wao

  7. Muda mfupi baada ya Lori la mafuta kushika moto Morogoro

    Si mara ya kwanza visa vya moto inayotokana na malori yaliobeba shehena ya mafuta kutokea katika enao la Afrika Mashariki na Kati. Mwaka 2010 watu 292 walifariki dunia nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya na miaka mitano baadae watu 203 wakafarikiki nchini Sudan Kusini.

  8. Nini kilichotokea Morogoro?

    Mmoja wa manusura wa mkasa huo alisikika akisimulia kilichojiri. "Hapa nilikuta watu wanang'ang'ania mafuta na watu walikuwa bizee kuchota mafuta na hawaelewi haya ni mafuta au maji. Katika huo mshangao sasa mimi nasikia moto umelipuka. Moto ulipozuka tukaanza kukimbiana, kila mmoja anajiokoa kivyake vyake, kufikia hapo nimeanguka chini nikaanza kutambaa kwa magoti nikufanikiwa kuondoka ." alisema manusura huyo

    Walioshuhudia ajali hiyo wanasema waendesha piki piki ndio walioathirika zaidi na mkasa huo.

  9. Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo umeaanza

    Watu 60 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 65 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro, Mashariki mwa Tanzania.

    Polisi wanasema watu hao walikuwa wakichota mafuta baada ya lori hilo kupinduka katika bara bara kuu mapema Jumamosi wakati ajali hiyo ilipotokea.

    Bado chanzo cha ajali hiyo hakijathibitishwa lakini kuna hofu huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

  10. Tamko la Rais Magufuli kuhusu ajali ya lori la mafuta Tanzania

    Rais wa Tanzania, John Magufuli amepokea amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 60 na wengine 70 kujeruhiwa vibaya baada yakuungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta kupata ajali na kisha kulipuka moto Mjini Morogoro.

    Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo na pia amewaombea majeruhi wapone haraka.

    Taarifa hiyo pia imekemea vitendo vya wananchi wanaovamia magari yenye milipuko akitaka vikomeshwe mara moja.

    Ajali hiyo ilitokea mapema Jumamosi mwendo wa saa mbili asubuhi wakati ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva

    wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.

    "Nimeumia sana kusikia idadi kubwa ya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, natoa pole kwa wote walioguswa na vifo hivi hasa familia za marehemu wote, nawaombea marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka" amesema Rais Magufuli.