Jeshi lachukuwa uongozi wa nchi Sudan

Maandamano ya kumpinga Bashir yalianza mwezi Disemba 2018

Moja kwa moja

  1. 'Magari ya kijeshi yaingia katika makao ya rais Bashir' nchini Sudan

    Magari kadhaa ya kijeshi yameingia katika eneo ambako kuna makao makuu ya wizara ya ulinzi na makaazi rasmi ya rais Omar al Bashir, mapema leo alfajiri, shirika la habari la AFP limenukuu watu walioshuhudia hilo ambao hawakutajwa majina.

    Wakosoaji wa rais Omar al-Bashir wanasema ameongoza kwa mabavu tangu aingie madarakani kupitia mapinduzi mnamo 1989

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wakosoaji wa rais Omar al-Bashir wanasema ameongoza kwa mabavu tangu aingie madarakani 1989
  2. Hujambo!

    Haya ni matangazo ya moja kwa moja kuhusu matukio yanayojiri nchini Sudan kufuatia maandamano ya raia wanaopinga utawala wa rais Omar al Bashir.