'Magari ya kijeshi yaingia katika makao ya rais Bashir' nchini Sudan
Magari kadhaa ya kijeshi yameingia katika eneo ambako kuna makao makuu ya wizara ya ulinzi na makaazi rasmi ya rais Omar al Bashir, mapema leo alfajiri, shirika la habari la AFP limenukuu watu walioshuhudia hilo ambao hawakutajwa majina.