Uchunguzi waidhinishwa kubaini chanzo cha ajali

Siku moja baada ya ajali ya ndege ya Ethiopian airlines kuanguka, sasa angazio ni kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo chapa Boeing 737 Max ambayo ni ya tano ya aina ya ndege hiyo katika miezi mitano - na ikiwa ni ndege mpya.

Moja kwa moja

  1. CAF lathibitisha kifo cha Hussein Swaleh Mtetu

    Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa taarifa rasmi kuhusu kufariki kwa aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la taifa na afisa mkuu wa soka Kenya, Hussein Swaleh Mtetu ambaye alikuwa miongoni mwa Wakenya 32 waliofariki.

    Inaarifiwa Hussein Swaleh alikuwa anarudi nyumbani baada ya kuhudumu kama kamishna katika ligi ya mabingwa ya CAF katika mechi kati ya Ismaily SC (Misri) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo) iliyochezwa Ijumaa huko Alexandria.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  2. Mambo 7 makuu kuhusu Boeing 737 Max-8

    • Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.
    • Injini yake iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake, ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing.
    • Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boeing 737.
    • Ndege iliyoanguka ni miongoni mwa sita kati ya 30 zilizoagizwa na shirika la ndege la Ethiopia kwa upanuzi wa shirika hilo.
    • Ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya shirika la Lion Air ambayo pia ilikuwa mpya ilitokea muda mfupi baada ya kuondoka.
    • Boeing ilisema imetuma ilani ya dharura kwa kampuni za ndege ikionya kuhusu matatizo ya mfumo wa kuzuia ndege kukosa nguvu.
    • Katika ajali ya nyuma, marubani walionekana kutatizika na mfumo huo wa kujitegemea ulioundwa kuizuia ndege hiyo kukwama, ulioidhinishwa katika Boeing 737 Max.
  3. Safari za ndege zote Boeing 737 Max zasitishwa Ethiopia

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Waliofariki katika ajali ni akina nani?

    Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.

    https://bbc.com.im/swahili/habari-47513713%3C/a%3E%3C/p%3E%3C/div%3E%3Cdiv dir="ltr" class="css-1k9op6x e17x9cvu0">

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Anthony Ngare

    Chanzo cha picha, @Anthony Ngare FB

    Maelezo ya picha, Anthony Ngare, mwanaharakati anayetetea uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi kwa habari Kenya

    Shirika la Umoja wa mataifa UNESCO limeelezea masikitiko kwa kumpoteza mwanaharakati anayetetea uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi kwa habari Kenya Anthony Ngare aliyehudumu katika kitengo cha tume ya kitaifa Kenya kwa UNESCO. Amekumbukwa kama mtu aliyesaidia kuidhinishwa miradi mingi iliyonuiwa kuimarisha sekta ya redio za kijamii Kenya.

    Kwa waliokuwa karibu naye wanamkumbuka kama shabiki sugu wa timu ya Arsenal - Uingereza.

  5. China yasitisha usafiri wa ndege sawa na ya Ethiopia iliyoanguka

    Mkaguzi wa safari za ndege China ameagiza kampuni zote za ndege nchini kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia ambayo ni ya muundo sawa.

    Kampuni za ndege ni lazima zisitishe usafiri wa abiria wa ndege zote za Boeing 737 Max 8 kufikia saa 18:00 kwa saa za huko.

    Ajali ya Ethiopian Airlines ni ya pili ya ndege aina hiyo chapa 737 Max 8 katika muda wa miezi mitano iliyopita.

  6. Viongozi waliotoa risala za rambi rambi

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Ruka X ujumbe, 4

    Mwisho wa X ujumbe, 4

  7. Mambo makuu tunayoyafahamu kufikia sasa katika ajali hiyo

    • Ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikielekea katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Addis Ababa, na kuwaua abiria wote walio kuwa ndani.
    • Ajali hiyo ilitokea 08:44 saa za Ethiopia, dakika sita baada ya ndege hiyo Boeing 737 Max-8 kuondoka.
    • Kampuni ya ndege imeeleza kuwa abiria 149 na maafisa 8 wa ndege hiyo ET302 wamefariki.
    • Waliofariki wametoka mataifa 30.
    • Ndege hiyo ya Boeing Max-8 iliwasilishwa kwa shirika la ndege la Ethiopia mnamo Novemba 15 mwaka jana.
    • Chanzo cha ajali hakijajulikana. Hatahvyo inaarifiwa rubani aliripoti kukabiliwana hitilafu na aliomba kurudi Addis.
    • Waziri mkuu ametangaza leo Machi 11 kama siku ya maombolezi ya kitaifa.
    Raia apiga picha ya masalio ya ndege katika eneo la mkasa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Raia apiga picha ya masalio ya ndege katika eneo la mkasa
    Huzuni imetanda kwa waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Huzuni imetanda kwa waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo
  8. Hujambo!, Karibu, hii ni taarifa maalum kufuatia ajali ya shirika la ndege la Ethiopia.