Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Uchunguzi waidhinishwa kubaini chanzo cha ajali

Siku moja baada ya ajali ya ndege ya Ethiopian airlines kuanguka, sasa angazio ni kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo chapa Boeing 737 Max ambayo ni ya tano ya aina ya ndege hiyo katika miezi mitano - na ikiwa ni ndege mpya.

Moja kwa moja

  1. CAF lathibitisha kifo cha Hussein Swaleh Mtetu

    Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa taarifa rasmi kuhusu kufariki kwa aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la taifa na afisa mkuu wa soka Kenya, Hussein Swaleh Mtetu ambaye alikuwa miongoni mwa Wakenya 32 waliofariki.

    Inaarifiwa Hussein Swaleh alikuwa anarudi nyumbani baada ya kuhudumu kama kamishna katika ligi ya mabingwa ya CAF katika mechi kati ya Ismaily SC (Misri) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo) iliyochezwa Ijumaa huko Alexandria.

  2. Mambo 7 makuu kuhusu Boeing 737 Max-8

    • Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.
    • Injini yake iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake, ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing.
    • Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boeing 737.
    • Ndege iliyoanguka ni miongoni mwa sita kati ya 30 zilizoagizwa na shirika la ndege la Ethiopia kwa upanuzi wa shirika hilo.
    • Ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya shirika la Lion Air ambayo pia ilikuwa mpya ilitokea muda mfupi baada ya kuondoka.
    • Boeing ilisema imetuma ilani ya dharura kwa kampuni za ndege ikionya kuhusu matatizo ya mfumo wa kuzuia ndege kukosa nguvu.
    • Katika ajali ya nyuma, marubani walionekana kutatizika na mfumo huo wa kujitegemea ulioundwa kuizuia ndege hiyo kukwama, ulioidhinishwa katika Boeing 737 Max.
  3. Waliofariki katika ajali ni akina nani?

  4. China yasitisha usafiri wa ndege sawa na ya Ethiopia iliyoanguka

  5. Mambo makuu tunayoyafahamu kufikia sasa katika ajali hiyo