Wafuasi wa upinzani waanza kuingia Uhuru Park
Wafuasi wa upinzani nchini Kenya wameanza kuingia uwanja wa Uhuru Park baada ya polisi kuondoka.
Baadhi wanazunguka uwanja huo wakiimba 'Uhuru Must Go'.
Tazama:
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga amejiapisha kuwa rais wa wananchi, huku serikali ikifungia baadhi ya vituo vya habari vilivyokuwa vinapeperusha matangazo moja kwa moja.
Wafuasi wa upinzani nchini Kenya wameanza kuingia uwanja wa Uhuru Park baada ya polisi kuondoka.
Baadhi wanazunguka uwanja huo wakiimba 'Uhuru Must Go'.
Tazama:
Mabasi matatu yaliyokuwa yanawasafirisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaelekea Nairobi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga yamekamatwa na maafisa wa polisi katika mji wa Voi, katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Nairobi.
Mji wa Voi unapatikana takriban kilomita 330 mashariki mwa mji huo mkuu wa Kenya.
Afisa wa polisi amewaambia wanahabari kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wamevunja sheria kadha za barabarani.
Kituo cha habari cha kibinafsi cha Citizen kimeripoti kuwa maafisa wa polisi wameamrishwa kuondoka katika uwanja wa Uhuru Park.
Hata hivyo, ni kama bado hakuna maandalizi yoyote yaliyofanywa ndani ya uwanja huo.
Maafisa wa polisi walifika asubuhi na mapema katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi unaopanga kutumiwa na muungano wa Nasa kwa shughuli ya kumuapisha Bw Odinga.
Mwandishi wa BBC David Wafula alipiga picha hizi za polisi wakiwa na magari maalum ya kukabiliana na ghasia wakishika doria uwanjani humo asubuhi na mapema:
Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.
Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi.
Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu mpango wa upinzani Kenya wa kumuapisha kiongozi wao Raila Odinga kuwa kiongozi wa taifa hilo.