Hali ilivyo ukumbi wa kutangazia matokeo Bomas
Mwandishi wa BBC David Wafula amekuwa Bomas ambapo matokeo kamili ya urais yatatangazwa muda mfupi ujao na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati.
Tazama:
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bw Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98% na tume ya uchaguzi IEBC.
Mwandishi wa BBC David Wafula amekuwa Bomas ambapo matokeo kamili ya urais yatatangazwa muda mfupi ujao na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati.
Tazama:
Watu mashuhuri, wakiwemo waangalizi, wamekuwa wakiwasili ukumbi wa Bomas, Nairobi ambapo matokeo ya urais yanatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Miongoni mwa waliowasili ni Maspika wa mabunge yote mawili Ken Lusaka (Seneti) na Justin Muturi (Bunge la Taifa).
Kiongozi wa waandalizi wa Umoja wa Afrika (AU) rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki pia yupo ukumbini.
Waziri wa elimu Dkt Fred Matiang'i amesema mtihani wa taifa wa darasa la nane utaendelea kesho kama ilivyopangwa na hautatatizwa na uchaguzi.
Amesema karatasi za mitihani na vifaa vingine vimesafirishwa maeneo yote.
Watahiniwa 1,003,556 wanatarajiwa kufanya mtihani huo katika vituo 28,566 kote nchini.
Shule nyingi hutumiwa kama vituo vya kupigia kura.
Naibu mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Kenya Consolata Nkatha Maina amesema matokeo ya urais kutoka maeneo ambayo uchaguzi wa marudio ulifanyika yatatangzwa saa tisa unusu alasiri.
Amesema wagombea wote wa urais wamealikwa kwa shughuli hiyo.
Bi Maina amesema maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika hayawezi kuathiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.
Taarifa zinasema vijana ambao wamekuwa wakirusha mawe wamekabiliana na maafisa wa polisi katika shule ya msingi ya Gatina eneo la Kawangware, Nairobi.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alikuwa amezuru eneo hilo jana na kuhusu kanisani.
Mtaa wa Kawangrware umekubwa na makabiliani ya wakazi kwa wakazi kuhusiana uchaguzi huo wa marudio uiiokumbwa na utata.
Vijana hao wamekuwa wakiwarushia polisi mawe baada ya waziri wa elimu Dkt Fred Matiang'i, ambaye ndiye kaimu waziri wa usalama, kuzuru shule hiyo kufuatilia jinsi mtihani wa kitaifa wa darasa la nane unaendeshwa.
Kumekuwa na dalili kwamba huenda Tume ya Uchaguzi IEBC ikatangaza matokeo kamili ya maeneo ambayo uchaguzi ulifanyika wakati wowote leo.
Tume hiyo ilikuwa imepanga kikao na wanahabari jana jioni lakini baadaye kikaahirishwa hadi "nusu ya kwanza ya siku leo".
Katika kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas, Nairobi kumekuwa na shughuli ambazo si za kawaida.
Viti vinapambwa na baadhi ya maafisa wakuu serikali wanaonekana katika pilka pilka za hapa na pale.
Mwandishi wetu Abdifitah Ibrahim anasema shughuli hizo si za kawaida jambo ambalo linadokeza huenda kukawa na "tangazo kubwa".
Ametutumia picha hizi:
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini Kenya mnamo 26 Oktoba. Matokeo kamili bado yanasubiriwa.