Obama ampigia simu Trump kumpongeza

Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Moja kwa moja

  1. Trump: Nitachunguza kabla ya kukubali matokeo

    Katika mahojiano na kituo kimoja cha Runinga ,Donald Trump amesema kuwa ''atachunguza vile mambo yanavyoelekea'' kabla ya kukubali matokeo.

     Aliambia kituo cha runinga ya Fox News kwamba amesikia kuhusu visa vya dosari katika upigaji kura,ijapokuwa hakutoa maelezo zaidi.

     Wakati wa kampeni bwana Trump alidai kwamba uchaguzi ulikuwa unakabiliwa na udanganyifu na akasema kwamba atapinga matokeo ambayo yana dosari.

    Donald Trump amesema kuwa atachunguza kabla ya kukubali matokeo ya uchaguzi nchini Marekani
    Maelezo ya picha, Donald Trump amesema kuwa atachunguza kabla ya kukubali matokeo ya uchaguzi nchini Marekani
  2. Meya wa New York: Itakuwaje Trump akikataa kushindwa?

    Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema kuwa uchaguzi huu utakumbukwa na wengi ,lakini akaongezea kwamba hatoshangaa iwapo mgombea wa Republican Donald Trump atakataa kukubali kushindwa.

     ''Ukitathimini kile alichosema kufikia sasa sitashangaa akikataa kukubali kushindwa licha ya kuonekana wazi kwamba bi Hillary anaongoza.Nadhani itakuwa vigumu sana kwa yeye kukubali kushindwa''.

    Meya wa mji wa New York Bill De Blasio akiwa na mgombea wa Democrat Hillary Clinton katikati

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Meya wa mji wa New York Bill De Blasio akiwa na mgombea wa Democrat Hillary Clinton katikati
  3. Siku isiyo ya kawaida

     Kasuku akielekea kituo cha kupigia kura huko Los Angels, na mtu aliye nusu uchi akimkinga Trump kutoka kwa wanawake waandamanaji nje ya jumba la Trump Tower mjini New York.

    Kasuku foleni

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kasuku foleni
    Trump akikingwa kutoka wa waandamanaji

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Trump akikingwa kutoka wa waandamanaji
  4. Sanders: 'Mshinde vibaya'

     Aliyekuwa mshindani wa Clinton wakati wa mchujo Bernie Sanders, ametoa wito kwa wapiga kura kumshinda Trump "vibaya" . 

    Senator huyo wa Vermont alisema kuwa ni wakati wa kumjisha Donald Trump kuwa utajiri na makampuni makubwa sasa yatalipa mgao wao. 

  5. Habari za hivi punde, Trump ashtaki kwa kupitishwa muda wa kupiga kura

     Kundi la kampeni ya Trump linamshtaki msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Nevada kwa kuacha vituo vya kupigia kura vikiwa vimefunguliwa . 

     Linamlaumu Joe P Gloria kwa kuacha vituo wazi saa mbili zaidi ya muda ambao vinastahili kufungwa. 

    Akijibu msemaji wa kaunti Dan Kulin, aliliambia shirika la CNN kuwa ni wapiga kura ambao tayari walikuwa kwenye foleni wakati kufungwa kwa vituo waliruhusiwa kupiga kura. 

     Mawakili wa Trump pia wanataka kura zilizopigwa mapema kuwekwa kando na kura zingine. 

    Trump anadai vituo vilifungw saa mbili baada ya muda rasmi

    Chanzo cha picha, clark county courts

    Maelezo ya picha, Trump anadai vituo vilifungw saa mbili baada ya muda rasmi
  6. Vita vya roho za Wamarekani

     Gazeti moja huko San Francisco la the East Bay Times, limeandika " hivi ni vita vya roho na wamarekani". 

    Linamuunga mkono Clinton lakini linasema kuwa Trump anaweza kushinda ikiwa raia wema watabaki nyumbani licha ya kupiga kura.

     Clinton alizuru San Francisco alipokuwa akichangisha fedha mwezi Oktoba na hii ndiyo picha ya umati.

    Umati uliojitokeza San Francisco

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Umati uliojitokeza San Francisco
  7. Merkel: Ushindi wa Clinton utaleta usawa katika uongozi

     Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa ushindi wa Hillary Clinton itakuw hatua ya kuelekea kuwepo usawa wa kijinsia miongoni mwa viongozi wa dunia. 

     "Halafu tutakuwa karibu na kuwepo usawa kati ya wanawake na wanaume katika nyadhifa za juu," Chansela huyo wa kwanza mwanamke nchini Ujerumani alisema. 

    Alikuwa akiongea mjini Berlin akiwa na Erna Solberg, ambaye ni waziri mkuu wa pili mwanamke nchini Norway.

    Merkel (kulia), Erna Solberg (kushoto)

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Merkel (kulia), Erna Solberg (kushoto)
  8. Mpiganiaji haki za wanawake akumbukwa

    Wakati wa siku ya kupiga kura foleni tofauti kabisa inaweza kuonekana eneo la makaburi la Mount Hope mjini New York, ambapo watu walijitokeza kutoa heshima kwa Sudan B Antony (1820-1906) ambaye alipigania haki wanawake kupiga kura. 

     Baadhi ya watu waliacha maua huku kaburi lake likiwekwa vibandiko vyenye maandishi" Nilipiga kura" au "Nilipiga kura leo." 

     Baada ya zaidi ya karne moja tangu Antony aage dunia, huenda Marekani ikamchagua mwanamke wa kwanza kama rais, Hillary Clinton.

    Susan B Antony alipigania haki ya mwanamke kupiga kura

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Susan B Antony alipigania haki ya mwanamke kupiga kura
  9. Obama: Kura zinaendelea kupigwa

    Rais wa Marekani Barack Obama ameandika katika mtandao wa Twitter akitoa wito wa wapiga kura zaidi kujitokeza kiga kura. "Kura zinaendelea kupigwa," aliandika Obama. 

  10. Trump: Ifanye Marekani tukufu tena

     Taarifa zaidi kuhusu bwana Trump akipiga kura: Alifika katika kituo cha kupigia kura Mashariki mwa Manhattan akiandamana na mkewe Melania, bintiye Ivanka na shemeji wake 

     "Ni kwa heshima kubwa, alisema huku akipiga kura. Alipoulizwa kuhusu madai ya wizi wa kura, alisema kuwa kila wakati hilo ni suala wanalolifikiria. 

     "Ifanye Marekani tukufu tena," Trump aliwaambia wapiga kura.

  11. Siku ya kuamua

     Kama umeungana nasi  ni kuwa mamilioni ya wapiga kura nchini Marekani wanamchagua rais mpya baada ya kinyanganyio kikali katika historia ya Marekani. 

     Hillary Clinton na Donald Trump wote washapiga kura zao. 

     Foleni ndefu za wapiga kura zinaripotiwa maeneo kadha lakini shughuli hiyo inaonekana kuwa shwari. 

    Tutaendeea kukuletea habari punde zinavyo chipuka. 

    Watu wapiga kura Marekani

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watu wapiga kura Marekani
  12. Upigaji kura ni shwari

    Ni wapiga kura wachache wanaoonekana kukumbwa na matatizo wa mujibu wa shirika la habari la AP. Uchaguzi wa urais kawaida unakumbwa na matatizo yakiwemo vifaa kutofanya kazi jinsi inavyotakikana kwa mujibu wa AP. 

    AP inasema kuwa matatizo ya kiufundi yameripotiwa katika majimbo ya Virginia na North Carolina. 

  13. Trump: 'Watu wanaumia'

    Akiongea kwa njia ya simu na Fox News kabla ya kupiga kura, Bw Trump alisema: "Naona watu wengi wenye matumaini na ndoto nyingi huko nje ambazo hazikutimia, lakini zingetimia, kama tungekuwa na uongozi, uongozi bora. Na watu wanaumia sana."

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

  14. Habari za hivi punde, Trump apiga kura

    Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump amepiga kura yake. Amepiga kura yake katika shule ya Public School 59 eneo la Manhattan, jijini New York si mbali sana na jumba la Trump Tower.

  15. Milolongo mirefu ya wapiga kura yaripotiwa Marekani

    Milolongo mirefu ya wapiga kura inaripotiwa sehemu tofauti nchini Marekani. Watu hawa walikuwa wamepanga mlolongo mjini Washington DC.

    Mlolongo wa wapiga kura

    Chanzo cha picha, AFP

  16. Marekani itakuwa kama 'Brexit'?

     Mwanasiasa wa Uingereza Nigel Farage, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele kwenye kampeni ya kuiondoa Uingereza kutoka Muungano wa Ulaya mwezi Juni ameandika kwenye mtandao wa Twitter, akisema kuwa ana matumaini kuwa Jumanne itakuwa siku ya Marekani ya "Brexit" ambayo ndiyo siku Uingereza iliondoka kutoka Muungano wa Ulaya.

    Kiongozi huyo wa chama cha UK Independence Party UKIP amemuunga mkono bwana Trump, na alionekana akiwa naye katika mji wa Jackson jimbo la Mississippi mwezi Agosti. 

  17. Clinton: Nina furaha sana

    Bi Hillary Clinton, alipokuwa akitoka kituo cha kupigia kura Chappaqua, New York akiwa mwenye tabasamu yele amewasalimia wafuasi wake na kusema: "Nina furaha sana. Nina furaha isiyo na kifani. Marafiki zangu na majirani zangu, hili ninanifanya nifurahi sana."

    Amesindikizwa na mumewe, aliyekuwa Rais Bill Clinton.  

    Bw na Bi Clinton

    Chanzo cha picha, Reuters

  18. Wanakijiji Kenya 'wampigia kura' Clinton

    Wakazi katika kijiji alikozaliwa babake Rais wa Marekani Barack Obama wameandaa uchaguzi wa mwigo ambapo mgombea wa Democratic Hillary Clinton ameibuka mshindi.

    Bi Clinton amepata 78% ya kura dhidi ya Bw Trump aliyepata 22% kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya.

    Babake Obama, Barack Obama Sr. alitoka kijiji cha Kogelo, jimbo la Siaya, magharibi mwa nchi hiyo.

    Nduguye wa kambo wa Rais Obama, Malik Obama, hata hivyo anamuunga mkono Bw Trump.

    Akihojiwa awali, alisema anampenda sana Bw Trump kutokana na “uwazi wake” na kuongeza kwamba amesikitishwa sana na uongozi wa Rais Obama.

    Aliambia BBC kwamba anaamini BwTrump, ni mtu mwenye huruma, mkweli na mwenye ushawishi.

    "Akizungumza kwenye runinga anaonekana mtu anasemaye ukweli, kuhusiana na dunia kwamba imeharibika na hakuna usalama,” amesema Bw Malik.

    Bw Malik Obama

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Bw Malik Obama
  19. Hillary Clinton apiga kura yake

    Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton amepiga kura yake Chappaqua, jimbo la New York state, akiwa ameandamana na mumewe Bill Clinton.

    Ndiye mwanamke wa kwanza wa chama kikuu Marekani kupata fursa ya kujipigia kura katika uchaguzi wa urais. Hapa, anaonekana kwenye video ya shirika la ABC News: 

  20. Matukio makuu uchaguzi Marekani

    Saa jumba la Trump

    Chanzo cha picha, AP

    Kuna mambo mengi sana yanayofanyika Marekani wakati wa uchaguzi na katika nyakati tofauti.

    Majimbo yote 50 pamoja na Washington DC (eneo ambalo halijatambuliwa kama jimbo) watapiga kura katika nyakati sita tofauti za uchaguzi.

    Tofauti hii inatokana na ukubwa wa taifa hilo, ambapo majimbo yaliyo mashariki yatatangulia kupiga kura na yale yaliyo magharibi yatakuwa ya mwisho.

    Maeneo mengi Marekani yatasubiri vituo vifungwe- sana kati ya 19:00 EST (24:00 GMT - Saa tisa usiku Afrika Mashariki) na 20:00 EST (01:00 GMT - Saa kumi usiku Afrika Mashariki) - kuanza kupokea matokeo na makadirio ya matokeo katika majimbo mbalimbali.