Wanasiasa na Wanaharakati watajwa kuchochea vurugu Oktoba 29
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, Jaji Mohamed Chande, amesema kauli mbiu na matamko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na waharakati yalichochea vurugu, kwani walitumia changamoto za wananchi, kama fursa za kuwashawishi kushiriki ghasia hizo.
Tume imebaini kulikuwa na vichocheo vikubwa vitatu vya kufanya ghasia:
Mitandao ya kijamii: Amesema mitandao ilitumika kabla na baada ya uchaguzi mkuu, na wabuni mada ambao walihamasisha watu wasishiriki katika uchaguzi mkuu au kuhakikisha haufanyiki.
Kauli mbiu: Amesema baadhi ya wanasiasa waliwahamasisha watu kufanya ghasia kwa kutumia kauli mbiu kama, "no reform no election, Oktoba hatutiki, Oktoba tunatoka, tumedhamiria uchaguzi hautofanyika, Samia Must Go, Tunataka kukomboa nchi yetu, hakuna uchaguzi chini ya serikali hii, tunahakikisha nchi haisimami, hakutakuwa na uchaguzi bila mabadiikio ya mfumo, serikali imepoteza uhalili, serikali iondoke, wagombea sio halali.
Wanasiasa: Kundi la tatu la vichocheo, ni baadhi ya maeneo ya nchi ambapo wagombea wa viti vya udiwani na ubunge, ambao waliona ghasia zinawasaidia kudai mabadiliko ya mfumo na kupata wagombea ndani vya vyama vyao, nao waliwahamasisha wafuasi wao kufanya ghasia.
Soma zaidi: