Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu
Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji, baadhi yao kuwaua, na kuwateka nyara au kuwakamata mamia kiholela.
Muhtasari
- Ujerumani yashtushwa na njama ya kumuua mkuu wa kampuni kubwa ya silaha nchini humo
- Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu
- Miili iliyowekwa kwenye mifuko yapatikana eneo la jalalani mjini Nairobi
- Katika picha: Kim Kardashian, Bieber na Rihanna wakiwa kwenye harusi ya mtoto wa tajiri zaidi barani Asia
- Nepal: Makumi ya watu hawajulikani walipo baada ya mabasi kusombwa na maporomoko ya ardhi
- China yaijibu NATO kutokana na shutuma za Urusi
- Wafungwa walitoroka kutoka jela ya Niger ambayo inayowashikilia wanamgambo wa jihadi
- Mwanajeshi wa Australia ashtakiwa kwa kuifanyia ujasusi Urusi
- Walliokuwa mawaziri Kenya wamshukuru Rais Ruto baada ya kufutwa kazi
- Biden amtambulisha kimakosa rais wa Ukraine Zelensky kama ‘Rais Putin’
- Video: Tazama wakati ndege mbili zilipokaribia kugongana New York
- Man Utd inakaribia kusaini mkataba wa pauni milioni 33.7 kumnunua mshambuliaji Zirkzee
- Jeshi la Israel 'lilishindwa katika kazi ' ya kuilinda kibbutz dhidi ya mashambulizi ya Hamas
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi, Seif Abdalla & Asha Juma
Ujerumani yashtushwa na njama ya kumuua mkuu wa kampuni kubwa ya silaha nchini humo

Chanzo cha picha, REUTERS/Fabian Bimmer
Wanasiasa wa Ujerumani wamejibu kwa hasira ripoti kwamba Urusi ilikuwa na njama ya kumuua mkuu wa kampuni kubwa ya silaha nchini Ujerumani ya Rheinmetall, Armin Papperger.
Ripoti ya CNN ilisema maafisa wa Marekani waliwaambia wenzao mjini Berlin mapema mwaka huu na usalama wake ukaimarishwa.
Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani ilikataa kutoa maoni yake lakini Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock alionekana kuthibitisha maelezo hayo.
"Kwa kuzingatia ripoti za hivi punde kuhusu Rheinmetall, hili ndilo ambalo tumekuwa tukiwasiliana kwa uwazi zaidi katika miezi ya hivi karibuni," aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa kilele wa Nato mjini Washington. "Urusi inaendeleza vita vya uchokozi."
Mjini Moscow, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikataa madai hayo. "Yote yamewasilishwa kwa mtindo wa simulizi nyingine ya uwongo, kwa hivyo ripoti kama hizo haziwezi kuchukuliwa kwa uzito."
Rheinmetall aliepuka kutoa maoni yake kuhusu masuala ya "usalama wa kampuni", lakini Bw Papperger sasa anaelezewa kuwa mtu anayelindwa sana katika uchumi wa Ujerumani…".
Kampuni hiyo ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa risasi duniani na imekuwa kiungo muhimu katika kuipatia Ukraine silaha, magari ya kivita na vifaa vingine vya kijeshi.
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu

Chanzo cha picha, NPS/X
Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya amejiuzulu kufuatia wiki kadhaa za maandamano yenye ghasia ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa.
Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji, baadhi yao kuwaua, na kuwateka nyara au kuwakamata mamia kiholela.
Maandamano yalizuka nchini Kenya katikati ya mwezi uliopita kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Waandamanaji walivamia bunge muda mfupi baada ya wabunge kupitisha mswada huo tata. Hatua ya Rais William Ruto kuiondoa ilifeli kuzima maandamano. Alivunja baraza la mawaziri siku ya Alhamisi .
Kuna mipango ya kuendelea na maandamano ya kuchochea mageuzi.
"MHE. William Samoei Ruto, Ph.D, CGH, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, tarehe 12 Julai, 2024, amekubali kujiuzulu kwa Eng. Japheth N. Koome, MGH, kama mkuu waPolisi," sehemu ya taarifa hiyo imesema
Miili iliyowekwa kwenye mifuko yapatikana eneo la jalalani mjini Nairobi
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Asha Juma
- Nafasi, BBC Swahili

Chanzo cha picha, Videograb/Twitter
Miili takriban 11 iliyowekwa kwenye mifuko imepatikana katika eneo la jalalani karibu na kitongoji duni cha Mukuru Kwa Njenga mjini Nairobi.
Idara ya upepelezi wa jinai inasema imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo huku uchunguzi maiti ukifanywa kuitambua .
Wanaharakati waliopata miili hiyo wamebaini kuwa baadhi ya miili imekatwa viungo.
Hussein Khalid kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika amesema baadhi ya miili hiyo ilikuwa imeoza ilhali mingine huenda imetupwa huko maajuzi .
Ameiambia BBC Swahili kwamba wakaazi wa eneo hilo wamesema miili hiyo ilitupwa huko kutoka sehemu nyingine .
Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai Mohamed Amin amesema kupitia taarifa kwamba wananchi wanafaa kushirikiana na mamlaka inapoendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Maelezo ya sauti, Miili kadhaa yapatikana imetupwa jalalani Nairobi Haya yanajiri huku mamlaka huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) ikitoa taarifa na kusema kufikia sasa imepokea malalamishi takriban 10 kuhusiana na visa vya kukamatwa, kutekwa nyara na kupotea kutokana na maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.
Nane kati ya hayo, IPOA ilisema kuwa waathirika walipatika wakiwa hai, mmoja bado hajulikani alipo huku mmoja akipatikana akiwa amefariki dunia.
IPOA pia ililalamikia ugumu wa kufikia waathirika na hivyo kuwa changamoto kwa wao kuhakikisha uchunguzi wa haraka unafanyika kuhusiana na madai yaliyopokelewa.
Soma zaidi:
Katika picha: Kim Kardashian, Bieber na Rihanna wakiwa kwenye harusi ya mtoto wa tajiri zaidi barani Asia

Chanzo cha picha, Reuters
Watu mashuhuri kutoka kote ulimwenguni wanawasili Mumbai kwa ajili ya harusi ya mtoto wa kiume wa tajiri zaidi barani Asia, Mukesh Ambani.
Anant Ambani anatarajiwa kufunga pingu za maisha na Radhika Merchant, binti wa mfanyabiashara wa maduka ya dawa wa India Viren na Shaila Merchant, katika sherehe ya kitamaduni ya Kihindu kwenye jiji la Mumbai siku ya Ijumaa.
Hafla za harusi zilianza na sherehe mnamo mwezi Machi.
Sherehe hizo zilizochukua miezi kadhaa zimehudhuriwa na mastaa wakubwa wa Bollywood, wanamuziki na vigogo wa biashara kama vile Bill Gates na Mark Zuckerberg.
Siku ya Ijumaa, nyota wa televisheni Kim Kardashian, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na rapa wa Nigeria Rema walikuwa miongoni mwa waliotua katika mji mkuu wa India kuhudhuria sherehe hizo.
Sherehe za harusi ya wanandoa hao huenda zikaendelea kwa siku kadhaa. Hafla zimepangwa kufanyika siku ya Jumamosi na Jumapili na sherehe kubwa ya mapokezi itafanyika siku ya Jumatatu.

Chanzo cha picha, Instagram

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwigizaji Priyanka Chopra aliwasili Mumbai na mumewe, mwimbaji Nick Jonas, siku ya Ijumaa 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Makazi ya Ambani mjini Mumbai yamepambwa kwa ajili ya harusi hiyo 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Gari lililopambwa likipita kwenye makazi ya Ambani 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Usalama umeimarishwa kuzunguka nyumba, huku vizuizi vya trafiki vikiwekwa kwenye barabara zinazoelekea eneo la harusi. 
Chanzo cha picha, ANI
Maelezo ya picha, Video ya Mukesh na mkewe Nita Ambani wakiwa na wajukuu zao ilitolewa kwenye sherehe ya kabla ya harusi wiki iliyopita. 
Chanzo cha picha, ANI
Maelezo ya picha, Wanandoa hao pia wametumbuiza katika baadhi ya hafla zao 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Onyesho la mwanamuziki wa pop Rihanna kwenye sherehe zilizofanyika Jamnagar liligonga vichwa vya habari duniani kote 
Chanzo cha picha, Instagram
Maelezo ya picha, Wiki hii, sherehe za mwisho zilipoanza mjini Mumbai, mwimbaji Justin Bieber alitumbuiza kwa sherehe ya harusi. Nepal: Makumi ya watu hawajulikani walipo baada ya mabasi kusombwa na maporomoko ya ardhi

Chanzo cha picha, AFP
Waokoaji wanawatafuta zaidi ya watu 60 waliotoweka nchini Nepal baada ya maporomoko makubwa ya ardhi kusomba mabasi mawili hadi kwenye mto.
Wengine walizungumza juu ya masaibu yao ya kutisha, huku mmoja akisema "alirushwa nje ya dirisha la basi hadi ndani ya mto".
Ni watu watatu pekee walioonekana kunusurika katika ajali hiyo iliyotokea alfajiri ya Ijumaa.
Mamlaka ilisema maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa.
Nepal, pamoja na maeneo mengine ya Asia Kusini, iko katikati ya msimu wa monsuni na imeshuhudia mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni, na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yameathiri mamilioni ya watu.
Ajali hiyo ilitokea saa tisa usiku kwa saa za eneo siku ya Ijumaa huko Chitwan kando ya barabara kuu ya Narayanghat-Mugling, takriban kilomita 100 kutoka mji mkuu Kathmandu.
Nandan Das aliyenusurika aliambia Idhaa ya Nepali ya BBC kwamba basi hilo lilikuwa barabarani kwa takriban saa moja na nusu wakati "lilipoanza kubingirika ghafla kuelekea mtoni... nilihisi kama nitakufa".
Alisema alifanikiwa kuogelea hadi mahali salama ingawa ilikuwa "giza sana usiku ... mto ulikuwa umejaa mawe makubwa na majani.
“Tulikuwa tukitaja jina la Mungu tukaogelea na kuogelea na kuogelea, Mungu alituokoa.
"Sikujua kama nilikuwa nikiogelea kuelekea nje ya mto au narejea ndani... lakini nilifika ukingoni. Kisha nikaanza kupanda mteremko."
Alisema kuwa yeye na mtu mwingine aliyenusurika walifika kwenye barabara kuu kwa wakati mmoja, na muda mfupi baadaye mwingine wa tatu akafika. Walifanikiwa kupata msaada kutoka kwa dereva, ambaye aliita polisi.
Pia unaweza kutazama:
China yaijibu NATO kutokana na shutuma za Urusi

Chanzo cha picha, AFP
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amejibu madai ya Nato "yasio na msingi" kwamba Beijing inaisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Pia imeonya muungano wa nchi za Magharibi dhidi ya kuchochea makabiliano.
Bw Wang alitoa maoni yake kwa njia ya simu na mwenzake wa Uholanzi, saa chache baada ya viongozi wa nchi wanachama wa Nato kukusanyika Washington DC na kutoa tamko lililotaja vita.
Waliishutumu China kwa kuwa "mwezeshaji madhubuti" wa Urusi kupitia "uungaji mkono wake mkubwa upande wa viwanda vya ulinzi wa Urusi", katika baadhi ya matamshi yao makali kuhusu Beijing.
Waliitaka China kusitisha "msaada wote wa nyenzo na kisiasa" kwa juhudi za vita za Urusi kama vile usambazaji wa vifaa vya matumizi mara mbili, ambavyo vinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiraia na kijeshi.
Mataifa ya Magharibi awali yaliishutumu China kwa kuhamisha teknolojia ya ndege zisizo na rubani na makombora na picha za satelaiti hadi Urusi.
Marekani inakadiria takriban asilimia 70 ya zana za mashine na asilimia 90 ya vifaa vidogo vya elektroniki zinazoagizwa na Urusi sasa zinatoka China.
Beijing pia ilishutumiwa kwa kuendesha "shughuli mbaya za mtandao, ikiwa ni pamoja na taarifa potofu" kuhusu mataifa ya Nato.
Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa alikuwa na majadiliano na viongozi wengine kuhusu kueleza madhara kwa China.
Soma zaidi:
Wafungwa watoroka kutoka jela ya Niger ambayo inayowashikilia wanamgambo wa jihadi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jaribio la hapo awali la kuvunja gereza la Koutoukale lilizuiwa mnamo 2019 Mamlaka nchini Niger imetangaza amri ya kutotoka nje katika eneo lenye hali tete la Tillaberi baada ya wafungwa kadhaa kutoroka katika gereza yenye ngome nyingi inayojulikana kuwa na idadi kubwa ya wanajihadi.
Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi katika gereza la Koutoukale lililoko takriban kilomita 50 kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Niamey, wizara ya mambo ya ndani ilisema.
Majaribio mengine mawili ya kutoroka gereza hilo ya mnamo 2016 na 2019 yalizimwa na maafisa wa usalama.
Vikosi vya kijeshi vya Niger vimelemewa na mashambulizi ya wapianaji wa jihadi magharibi na kuwalinda utawala wa kijeshi ambao ulichukua mamlaka kwa mapinduzi ya mwaka jana.
Mwanajeshi wa Australia ashtakiwa kwa kuifanyia Urusi ujasusi

Chanzo cha picha, Facebook
Maelezo ya picha, Kira Korolev alikuwa fundi katika huduma za mawasiliano katika jeshi Mwanajeshi wa Australia na mumewe wamekamatwa na kila mmoja kushtakiwa kwa kuifanyia ujasusi Urusi.
Wachunguzi wanasema wanandoa hao, wote raia wa Australia waliozaliwa Urusi - walipata nyaraka za Jeshi la Ulinzi la Australia (ADF) kwa ajili ya kuzitoa kwa serikali ya Moscow.
Hata hivyo, polisi ya Australia inasema "hakuna taarifa kubwa na za muhimu " za siri zilizobainika kuchukuliwa na washukiwa hao.
Hii ni mara ya kwanza kwa sheria kali za uingiliaji wa kigeni - zilizoanzishwa na Australia mnamo 2018 kutumika zimetumika katika kufungua mashtaka ya ujasusi.
Kira Korolev na mume wake Igor Korolev mwenye umri wa miaka 62 walishitakiwa na mahakama ya Brisbane siku ya Ijumaa, kila mmoja kwa kosa moja la kujiandaa kwa kosa la ujasusi na iwapo watapatikana na hatia watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka miaka 15 jela.
Walliokuwa mawaziri Kenya wamshukuru Rais Ruto baada ya kufutwa kazi

Chanzo cha picha, Reuters
Waliokuwa mawaziri katika baraza la mawaziri la Rais wa kenya William Ruto lililovujwa Jumanne wamekuwa wakielezea hisia zao kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ikiitwa Twitter).
‘’Kwa karibu miezi 20, nimekuwa na uzoefu wa kutimiza na wenye utajiri mkubwa nikihudumu kama Katibu wa Baraza la Mawaziri la moja ya sekta muhimu zaidi nchini Kenya - Elimu. Napenda kumshukuru Rais kwa kuniamini kwa heshima hii, na nina ninamshukuru kwa hatua zote kubwa tulizozipata ndani ya muda mfupi kama huu kwani tulitoa elimu kwa watoto wetu’’ , aliandika mwenye ukurasa wake wa X aliyekuwa Waziri wa elimu Ezekiel Machogu.
Alyekuwa waziri wa michezo Ababu Namwamba pia aliandika :''Ni heshima maalum, heshima na baraka kutumikia taifa la mtu, zaidi katika Baraza la Mawaziri, chombo cha juu zaidi cha kutengeneza sera nchini. Namshukuru Mheshimiwa Rais @WilliamsRuto
kwa imani na aliyokuwa aliyooonyesha kwa uteuzi wangu kuhudumu katika Baraza la Mawaziri kwa mara ya pili katika maisha yangu ya utumishi wa umma. Mungu ibariki Kenya na kumpa Rais neema na hekima ya kuendesha nchi yetu katika bandari salama.''
Waliokuwa mawaWote wamemshukuru Bw Ruto kwa kuwapatia fursa ya kuhudumia Wakenya na taifa.
Ujumbe kwa rais kutoka kwa waliokuwa mawaziri kwa ujumla ulikuwa wa kumshukuru Bw Ruto kwa kuwapatia fursa ya kuhudumia Wakenya na taifa.
Rais huyo wa kenya alilivunja baraza lake la mawaziri na kuziacha nafasi mbili pekee-ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi na ofisi ya naibu wa rais Rigathi Gachagua .
Alisema atachukua muda kufanya majadiliano ya kuunda baraza jipya la mawaziri litakalohusika na uendeshaji wa serikali.
Hatua ya Rais Ruto ya kulivunja baraza lake la mawaziri imefuatia shinikizo kubwa la vuguvugu la vijana wa nchi hiyo linaloitwa Gen-Z lililofanya maandamano yaliyosababisha vifo na majeruhi
Unaweza pia kusoma:
Biden amtambulisha kimakosa rais wa Ukraine Zelensky kama ‘Rais Putin’

Chanzo cha picha, Getty Images
Biden amtambulisha kimakosarais wa Ukraine Zelensky kama ‘Rais Putin’ “katika mkutano wa NATO unaofanyika mjini Washington. Baadaye alijirekebisha mwenyewe akisema “Nimemakinika sana kuhusu kumpiga Putin.”
Siku ya Alhamisi Rais Joe Biden pia alichanganya majina ya Makamu wa Rais Kamala Harris na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, huku akimuita Bi Kamala Trump, lakini akasisitiza kwamba anasonga mbele na azma yake ya kugombea tena kiti hicho licha ya kwamba Wademocratic wenzake wengi walimtaka asitisha kampeni
Biden, 81, alizungumzia uzoefu wa miongo kadhaa kwenye jukwaa la dunia huku akisema kwamba alikuwa na sifa za kipekee kumshinda Rais wa zamani Trump mwenye umri wa 78, na kuiongoza Marekani kwa muhula mwingine wa miaka minne.
"Kitu pekee ambacho umri hufanya ni kujenga hekima kidogo iwapo utazingatia," alisema Biden, ambaye tayari ndiye mtu mzee zaidi kuwahi kuhudumu kama rais.
Tangu utendaji wake duni dhidi ya Trump katika mdahalo wa urais wiki mbili zilizopita, Biden amekabiliwa na mashaka yanayoongezeka kutoka kwa wafadhili, wafuasi na Wanademokrasia wenzake kuhusu uwezo wake wa kushinda uchaguzi wa mwezi Novemba na kuendelea na kuendelea kutekeleza kazi yake ipasavyo.
Unaweza pia kusoma:
Je, ni nini kilichotokea kwa Mbappe na Ufaransa?
Video: Tazama wakati ndege mbili zilipokaribia kugongana New York
Maelezo ya video, Tazama: Wakati ndege mbili zilipokaribia kugongana New York Video ya kamera ya polisi ilinasa tukio wakati ndege mbili zilipokaribiana ndani ya umbali wa futi 725 (m221) ya juu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Syracuse Hancock.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Juni 8 na mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo inachunguza tukio hilo.
Man Utd inakaribia kusaini mkataba wa pauni milioni 33.7 kumnunua mshambuliaji Zirkzee

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Joshua Zirkzee alicheza mechi yake ya kwanza ya Uholanzi kwenye michuano ya Euro 2024 baada ya kuchukua nafasi ya kiungo Frenkie de Jong aliyejeruhiwa. Manchester United wanakaribia kukamilisha mkataba wa £33.7m kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee kutoka Bologna.
Vyanzo vya United vinasema kuwa klabu hiyo iko tayari kulipa kiasi kidogo cha malipo ya pauni milioni 33.67 ili kuongezewa muda wa malipo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza imedhamiria kufuata kanuni za faida na endelevu (PSR) kuhusu ukomo wa hasara na kukubali hali yao ya sasa ni ngumu na itahitaji nidhamu katika shughuli zao za uhamisho.
Mshambuliaji huyo wa muda mrefu Anthony Martial aliondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu uliopita mkataba wake ulipoisha.
Kutokuwepo kwa Mfaransa huyo kwa muda mrefu kwa sababu ya jeraha, pamoja na kushuka kwa kiwango cha Marcus Rashford, kulimuacha mchezaji mpya Rasmus Hojlund kuubeba mzigo huo.
Jeshi la Israel 'lilishindwa katika kazi ' ya kuilinda kibbutz dhidi ya mashambulizi ya Hamas

Chanzo cha picha, EPA
Wakazi wengi waliuawa katika eneo la Kibbutz Be'eri kuliko jamii nyingine yoyote ya Israel iliyoshambuliwa na Hamas tarehe 7 Oktoba
Waziri wa ulinzi wa Israel ametaka uchunguzi wa serikali ufanyike kuhusu kile kilichosababisha mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7, wakati jeshi likikiri kuwa lilishindwa katika jukumu lake la kulinda jamii ndogo ya watu 101 waliuawa.
Yoav Gallant alitoa matamshi haya baada ya ripoti ya kwanza ya jeshi la Israeli kuweka wazi jinsi jeshi lilivyoendesha shughuli zake katika eneo la Kibbutz Be'eri, ambalo liko karibu na uzio wa Gaza.
Wakazi wengi zaidi waliuawa katika eneo la kibbutz kuliko jamii nyingine yoyote ya Israel mnamo Oktoba 7, baada ya watu wenye silaha kuvuka kutoka Gaza na kuivamia nyumba zao.
Gallant alisema uchunguzi huru wa kitaifa unahitajika kuchunguza vitendo vya wale wote walio madarakani, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kuhusiana na jinsi nguvu za Hamas izilivyoongezeka na kuwa na uwezo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
Takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 walichukuliwa Gaza kama mateka katika shambulio hilo ambalo lamghafla mwaka jana.
Shambulio hilo lilisababisha operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ambayo imeuwa zaidi ya Wapalestina 38,000.
Unaweza pia kusoma:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo Ijumaa tarehe 12.06.2024
