Kesi ya uhaini dhidi ya Kizza Besigye kuanza kusikilizwa leo Uganda
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Kampala kuanza kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili.
Besigye na msaidizi wake, Obeid Lutale, wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama za kuipindua serikali ya Uganda.
Besigye alikamatwa mjini Nairobi mnamo Novemba 2024 na kurejeshwa kwa nguvu nchini Uganda, ambako amekuwa akizuiliwa tangu wakati huo.
Kesi hiyo inaanza kusikilizwa leo baada ya kuahirishwa mara kadhaa hapo awali.
Besigye, aliyekuwa daktari wa binafsi wa Rais Yoweri Museveni, mwaka jana hali ya afya yake ilidhoofika na kukimbizwa hospitalini kabla ya kurejeshwa gerezani.
Katika uamuzi wa kihistoria mwaka jana, Mahakama ya Juu ya Uganda ilitangaza kuwa ni kinyume cha katiba kwa mahakama za kijeshi kuwahukumu raia, na kuamuru kesi zote hizo kuhamishiwa katika mahakama za kiraia.
Uamuzi huo ulimkasirisha Rais Museveni, ambaye alipuuzilia mbali na kuutaja kuwa "uamuzi usio sahihi" na kuapa kuupinga.
Raia wengi wa Uganda ikiwemo mpinzani mwenza Bobi Wine aliandika kwa mtandao wa kijamii kushurutisha Besigye aachiliwe huru na aruhusiwe kupata huduma za matibabu.
Soma Zaidi: