Donald Trump aapishwa rasmi kuwa rais wa Marekani

Rais mteule wa Marekani pamoja na makamu wake JD Vance hatimaye wameapishwa rasmi kuwa rais na makamu wake wa Marekani. Kiongozi huyo sasa atakuwa rais wa 47 kulitawala taifa la Marekani.

Muhtasari

Moja kwa moja

Ambia Hirsi & Rashid Abdallah

  1. Utajiri wa mabilionea duniani uliongezeka mara tatu zaidi mwaka 2024- Ripoti

    x

    Chanzo cha picha, AFP/Getty

    Shirika la kimataifa la kutoa misaada la Oxfam limesema utajiri wa mabilionea duniani, uliongezeka mara tatu zaidi mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2023.

    Ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa kabla ya jukwaa la kimataifa la kiuchumi linalotarajiwa kufanyika huko Davos, inaonya kuhusu nguvu kubwa ya kisiasa na kiuchumi inachipuka kutoka kwa matajiri hao na kuutaja kuwa mfumo wa matajiri wachache walio na ushawishi mkubwa.

    Oxfam inabashiri kuwa matajiri watanufaika pakubwa na kurejea uongozini kwa Rais wa Marekani Donald Trump na kusababisha kuongezeka kwa pengo la ukosefu wa usawa kati ya matajiri na masikini katika jamii.

    Wametoa mfano wa mmiliki wa kampuni ya magari ya kifahari ya Tesla ambaye pia anamiliki mtandao wa kijamii wa X Elon Musk ambaye alifadhili pakubwa kampeini za Trump.

    Matajiri watatu wakubwa ulinwenguni Leon Musk,Jeff Bezos wa kampuni ya Amazon na Mark Zuckerberg wa kampuni ya Meta watakuwa katika hafla ya kuapishwa kwa Donald Trump.

    Mkurugenzi mkuu wa Oxfam Amitabh Behar amesema wanatoa ripoti huyo kuangazia namna watu wa kawaida kote ulimwenguni wanateseka huku wachache wakiwa na mali nyingi kupita kiasi.

    Utajiri wa mabilionea hao uliongezeka kwa dola trilioni mbili zaidi mwaka jana na kufikia utajiri jumla wa dola trilioni kumi na tano.Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘wachukuaji na sio watengezaji’ imebaini mwaka jana kulikuwa na mabilionea 204 wapya na kufikisha idadi ya mabilionea ulimwenguni kufika 2,769.

    Kwa wastani inakadiriwa kila bilionea alipata dola milioni mbili kila siku mwaka 2024.

    Oxfam inasema huku matajiri wakizidi kuwa matajiri zaidi, idadi ya watu wanaoishi katika umasikini haijabadilika tangu mwaka 1990.

    Pia unaweza kusoma:

  2. China yamnyonga dereva aliyewaua makumi ya watu katika shambulio la gari

    xx

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanamumu aliyewaua watu kadhaa kwa kuelekeza gari lake kwenye umati wa watu waliokuwa wakifanya mazoezi nje ya uwanja kusini mwa Uchina amenyongwa, vyombo vya habari vya serikali viliripoti.

    Fan Weiqiu, 62, aliwaua takriban watu 35 na kuwajeruhi makumi ya watu tarehe 11 Novemba baada ya kuendesha kwa kasi gari lake kwenye eneo la mazoezi huko Zhuhai, katika shambulio linalosadikiwa kuwa baya zaidi katika ardhi ya China kwa muongo mmoja.

    Mtu huyo alitekeleza mauaji hayo baada ya kudaiwa "kutoridhishwa" na jinsi mali yake ilivyogawanywa baada ya kutalakiana na mkewe, mahakama ilieleza.

    Hatua ya kunyongwa kwake inajiri chini ya mwezi mmoja baada ya mahakama kumhukumu adhabu ya kifo.

  3. Mwanaume akamatwa kwa kumchoma kisu mwigizaji wa Bollywood

    Saif Ali Khan

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Saif Ali Khan alichomwa kisu nyumbani kwake wiki iliyopita.

    Polisi katika mji wa Mumbai nchini India wamemkamata mwanamume mmoja kuhusiana na shambulio la kisu dhidi ya mwigizaji wa Bollywood Saif Ali Khan wiki iliyopita. Khan, mmoja wa nyota wakubwa wa India, alidungwa kisu na mvamizi nyumbani kwake, katika shambulio lililoishangaza nchi hiyo. Anapata nafuu baada ya upasuaji.

    Siku ya Jumapili, polisi walisema wamemkamata mshukiwa mkuu, Mohammad Shariful Islam Shehzad, na kuongeza kuwa alikuwa raia wa Bangladesh ambaye alikuwa akiishi India kinyume cha sheria.

    Wakili wa Bw Shehzad amekanusha madai hayo na kusema yeye hatoki Bangladesh.

    Polisi wanasema walimkamata Bw Shehzad kutoka Thane, wilaya iliyoko viungani mwa Mumbai.

    Ushahidi wa awali unaonyesha kwamba alikuja mjini kama miezi sita iliyopita na alikuwa akifanya kazi katika shirika la kutunza nyumba kwa kutumia jina na kitambulisho bandia, Dixit Gedam, naibu kamishna wa polisi wa Mumbai, aliambia mkutano na waandishi wa habari.

    Polisi wanashuku kuwa Bw Shehzad anadaiwa kuvamia nyumba ya Khan kwa nia ya kumwibia, Bw Gedam alisema. Siku ya Jumapili, mahakama ya Mumbai ilimtuma Bw Shehzad kuzuiliwa na polisi kwa siku tano.

    "Hakuna ushahidi wa maandishi unaoonyesha kuwa yeye ni raia wa Bangladesh," alisema wakali wake.

  4. Wachimba madini haramu saba wauawa nchini Ghana

    Jeshi la Ghana limesema wachimba madini haramu saba wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika eneo la Ashanti nchini humo.

    Mauaji hayo yamesababisha maandamano ya umma katika mji wa Obuasi ambako mabasi kadhaa yamechomwa moto

    Kulingana na jeshi la Ghana, takriban watu sitini wenye silaha walivunja uzio wa usalama kwenye mgodi unaosimamiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti.

    Katika taarifa yake ilisema askari walipojaribu kuwazuia watu hao, walifyatuliwa risasi.

    Mnamo Septemba kampuni nyingine ya uchimbaji madini katika eneo hilo hilo ilisema imekuwa ikivamiwa mara kwa mara na magenge yenye silaha.

    Kumekuwa na ongezeko la uchimbaji madini haramu kote nchini Ghana ambako kumechochewa na mgogoro wa kiuchumi ambao unatajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kizazi cha sasa.

    Athari za mazingira zimekuwa mbaya na serikali imekosolewa kwa kushindwa kuchukua hatua.

  5. Blinken amshukuru Waziri Mkuu wa Qatar kwa 'jukumu muhimu' katika juhudi za upatanishi

    Blinken

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amemshukuru Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdul Rahman Al Thani kwa "jukumu lake muhimu" katika juhudi za upatanishi ambazo zilichangia kusitishwa kwa mapigano ya Gaza.

    "Blinken alisisitiza haja ya mipango ya baada ya vita huko Gaza kuendelea, na kumtakia kila la heri Waziri Mkuu wa Qatar kwa juhudi zinazoendelea za kufikia amani ya kudumu katika eneo hilo," ilisema taarifa yake.

    huku hayo yakijiri Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema saa chache tu baada ya kuingia madarakani, atafutilia mbali kila amri ya rais iliyotekelezwa na mtangulizi wake Rais Joe Biden.

    Bwana Trump anaapishwa rasmi hii leo kuwa Rais.

    Amewaambia wafuasi wake mjini Washington kuwa Marekani inaingia katika enzi za ufanisi na kuwa utawala wake utashughulikia uhamiaji,kurejesha uzalendo,kufutilia mbali sheria kuhusu mazingira na pia amesema ni kutokana na ushindi wake katika uchaguzi wa Rais, makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza yamefikiwa.

    "Pengine kizuri zaidi,wiki hii tulifikia makubaliano mazuri ya kusitisha mapigano ambayo ni hatua ya mwanzo kueleka amani ya kudumu Mashariki ya Kati.'' alisema na kuongeza ''Nafurahi kuripoti kuwa mateka wa kwanza wameachiwa huru na nani anajua yapi yatajiri. Najua Biden anasema wamefikia makubaliano, Naam sikatai lakini makubaliano hayo yangefikiwa tangu mwanzo hatungefika hapa... kama ningekuwa rais haingetokea. Yaani hata hilo wazo halingekuwepo.''

    Maelezo zaidi:

  6. TikTok yarejesha huduma zake Marekani baada ya ahadi ya Trump

    Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    TikTok imerejesha huduma zake kwa watumiaji wake milioni 170 nchini Marekani baada ya Rais Mteule Donald Trump kusema atatoa agizo la kuipa programu hiyo ahueni atakapoingia madarakani rasmi hii leo.

    Jumamosi jioni, programu hiyo inayomilikiwa na Wachina ilisitisha huduma zakr kwa watumiaji wa Marekani, baada ya sheria ya kuipiga marufuku kwa misingi ya usalama wa taifa kuanza kutekelezwa.

    Trump, ambaye hapo awali aliunga mkono marufuku dhidi ya jukwaa hilo, aliahidi Jumapili kusitisha kwa muda utekelezaji wa sheria hiyo ili kutoa nafasi ya majadiliano.

    Baadaye TikTok ikasema kwamba ipo katika mchakato wa "kurejesha huduma".

    Muda mfupi baadaye, programu ilianza kufanya kazi tena. Watumiaji wake wa mtandao huo maarufu walimshukuru Trump kwa hatua hiyo.

    Katika taarifa, kampuni hiyo ilimshukuru rais huyo mteule kwa "kutoa uhakikisho unaohitajika" na kuongeza kuwa itafanya kazi na Trump "kutafuta suluhisho la kudumu ambalo litaisaidia TikTok kuendelea na shughuli zake nchini Marekani".

    Pia unaweza kusoma:

  7. Wafungwa 90 wa Kipalestina wachiwa huru baada ya Hamas kuwaachia mateka watatu wa Israel

    Mfungwa wa Kipalestina aliyeachiwa huru abubujikwa na machozi alipokutana na binti yake

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mfungwa wa Kipalestina aliyeachiwa huru abubujikwa na machozi alipokutana na binti yake

    Wapalestina tisini wameachiwa huru kutoka jela la Ofer lililoko katika Ukingo wa Magharibi, kuendana na makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza yaliyofikiwa kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

    Mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba wafungwa hao yalipokewa na umati wa watu waliokuwa wamejawa na furaha Gaza.

    Hamas inasema kwa kila mateka wa Israel aliyeachiliwa huru, wafungwa 30 wa Kipalestina wataachiwa kutoka jela za Israel.

    Wengi wa hao walioachiwa huru ni wanawake na inatarajiwa takriban wapalestina elfu mbili wataachiwa huru katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Aidha, zaidi ya malori 630 yaliyobeba misaada, yameruhiswa kuingia Gaza.

    Wakati mpango wa kusitisha mapigano ukisherehekewa Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, ameonya kwamba kushughulikia "mahitaji makubwa ya kiafya" ya walioko Gaza itakuwa "kabarua kigumu itakayokabiliwa na changamoto".

    Umati wa watu ulikuwa umekusanyika viunga mwa mji wa Ramallah kuwapokea wafungwa walioachiwa huru.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Umati wa watu ulikuwa umekusanyika viunga mwa mji wa Ramallah kuwapokea wafungwa walioachiwa huru.
    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

  8. Natumai hujambo.