Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vita vya Gaza: ICC yatafuta vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na viongozi wakuu wa Hamas

Mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan anasema kuna sababu za msingi kuthibitisha kwamba wawili hao walihusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliotekelezwa kuanzia tarehe 7 Oktoba 2023.

Muhtasari

  • Kifo cha Rais wa Iran: Matukio ya hivi punde
  • Katika Picha: Ulimwengu waomboleza kifo cha Rais wa Iran
  • Tunachojua kuhusu waathiriwa wa ajali ya helikopta Iran
  • Katika Picha: Ulimwengu unavyoomboleza kifo cha Rais wa Iran
  • Mahakama: Zuma hastahili kugombea uchaguzi wa Mei
  • Israel kuunda kamati maalum ya kupambana na uamuzi wa ICC
  • ICC yatafuta vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na viongozi wakuu wa Hamas
  • Ajali ya ndege Iran: Imam alinusurika kwa muda wa saa moja na kujaribu kutafuta msaada
  • Tunafahamu nini kuhusu helikopta iliyoanguka Iran?
  • Kifo cha Raisi ni pigo kwa 'ulimwengu wote wa Kiislamu' - kundi la Houthi
  • Mazishi ya Raisi kufanyika kesho - ripoti
  • Viongozi wa dunia wanasema nini?
  • Mohammad Mokhber ni nani, anayetarajiwa kuchukua usukani kama rais wa mpito wa Iran?
  • Rais William Ruto kuanza ziara ya kihistoria nchini Marekani
  • 'Acha kuitisha Taiwan', rais mpya William Lai aionya China
  • Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta - TV ya serikali
  • Wanajeshi wa Marekani kuondoka Niger katikati mwa Septemba
  • Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya msafara wa rais Ghana
  • Hakuna kilichothibitishwa lakini mazingira yanafanana na kilichofanyika kwa mwanzilishi wa taifa hilo
  • 'Hakuna dalili za yeyote aliye hai' katika eneo la ajali ya helikopta ya Raisi - TV ya serikali
  • Waokoaji kufikia helikopta iliyoanguka 'dakika chache zijazo' – chombo cha habari cha serikali
  • Vikosi vya uokoaji vyapata helikopta katika harakati za kumtafuta rais wa Iran
  • Helikopta iliyombeba rais wa Iran 'yatua kwa shida' - Runinga ya serikali
  • Vikosi vya uokoaji vyamtafuta Rais wa Iran Ebrahim Raisi

Moja kwa moja

Asha Juma & Ambia Hirsi

  1. 'Hakuna dalili za yeyote aliye hai' katika eneo la ajali ya helikopta ya Raisi - TV ya serikali

    "Hakuna dalili" za yeyote aliye hai katika helikopta iliyombeba Rais Ebrahim Raisi, TV ya serikali inasema.

    Shirika la habari la Reuters pia limeripoti kuwa helikopta hiyo "iliungua kabisa" katika ajali hiyo, ikimnukuu afisa wa Iran.

  2. Waokoaji kufikia helikopta iliyoanguka 'dakika chache zijazo' – chombo cha habari cha serikali

    Waokoaji watafika katika eneo la helikopta "dakika chache zijazo", mkuu wa Shirika la Red Crescent la Iran Pirhossein Kolivand ameambia chombo cha Habari cha serikali.

    Alisema walikuwa takriban kilomita 2 kutoka mahali ambapo inafikiriwa kutokea kwa ajili.

  3. Vikosi vya uokoaji vyamtafuta rais wa Iran baada ya ajali ya helikopta

    Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA limeripoti kuwa shughuli ya utafutaji Rais wa Iran yaendelea katika eneo linalodhaniwa kutokea ajali ya ndege lakini bado halijapatikana, eneo la utafutaji limepungua na sasa linaonyesha ukubwa wa kilomita 2.

    Televisheni ya Iran inaonyesha picha za waokoaji wakitembea kwenye miteremko mikali kwenye mvua na giza.

    Wakati huo huo Hossein Salami, kamanda wa Jeshi la Revolutionary Guards Corps (IRGC), aliwasili eneo la ajali ili kuchunguza na kuharakisha shughuli za uokoaji, shirika la habari la serikali IRIB linaripoti.

    Soma zaidi:

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 20/05/2024