Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Rigathi Gachagua: Wabunge wapiga kura kuamua hatma ya naibu wa Rais

Mbivu na mbichi kujulikana baada ya ya Spika wa bunge kutangaza kwamba wabunge sasa watapiga kura ili kuamua kuhusu hatma ya naibu wa rais Rigathi Gachagua

Muhtasari

  • Ofisi za Save the Children zavamiwa Guatemala
  • ‘‘Gachagua hana heshima kwa wamama aliita mbunge wetu malaya’’
  • Hoja ya kumtimua mamlakani Naibu wa Rais Kenya: Haya ndiyo unayopaswa kujua
  • Hezbollah yarusha makombora zaidi ya 100 kaskazini mwa Israel
  • Rais wa Korea Kaskazini, Kim amuita Putin 'rafiki wa karibu zaidi'
  • Rigathi Gachagua: Hoja ya kumuondoa madarakani Naibu wa Rais wa Kenya yaanza kujadiliwa bungeni
  • Israel inasema imeongeza operesheni ya ardhini kusini mwa Lebanon
  • Israel yasema ilimuua kamanda wa Hezbollah huko Beirut
  • Cissy Houston, mwimbaji nguli na mama wa Whitney Houston, afariki dunia
  • Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon asema nchi yake imetelekezwa na jumuiya ya kimataifa
  • 'Jinsi Israeli inavyojilinda ni muhimu,' asema Kamala Harris
  • Israel yaadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio la Hamas huku mapigano yakiendelea

Moja kwa moja

Na Asha Juma, Lizzy Masinga, Dinah Gahamanyi &Seif Abdalla

  1. Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon asema nchi yake imetelekezwa na jumuiya ya kimataifa

    Aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon wakati wa vita vyake vya mwisho na Israel mwaka 2006 ameambia BBC kuwa nchi yake imetelekezwa na jumuiya ya kimataifa.

    Fouad Siniora alisema ni jambo lisilokubalika kuiacha Lebanon isambaratike, na kulikuwa na ukosefu wa kujitolea linapokuja suala la kujaribu kurejesha amani.

    “Sasa tuko katika hali ngumu sana inayohitaji juhudi za kweli ndani ya nchi, pia kwa upande wa Waarabu na kimataifa.

    "Unaweza kushinikiza mambo - wakati mwingine hadi kufikia hatua ya kukaribia kusambaratika - katika janga kubwa bila kutambua baadaye itakuwa inamaanisha nini.

    "Inatokea wakati utawala wa Marekani una shughuli nyingi na uchaguzi.

    "Na hatuna uwezo wa kumchagua rais, kwa sababu baadhi ya makundi hasa Hezbollah, yamekuwa yakisisitiza kwamba wanataka rais ambaye hatakuja kusaliti kundi hilo baadaye," Siniora alisema.

    Vita vya mwisho kati ya Lebanon na Israel, karibu miaka 20 iliyopita, vilianza pale wapiganaji wa Hezbollah walipovuka mpaka na kuwashambulia wanajeshi wa Israel.

    Wawili walitekwa nyara na watatu waliuawa, na kusababisha vita vya mwezi mzima.

    Katika siku zilizofuata, Siniora alitoa taarifa kwa umma kuitenganisha serikali ya Lebanon na kile kilichotokea.

    Anafikiria, viongozi wa sasa wa nchi wameshindwa kufanya kile ambacho raia waliwaamini nacho, kufanya kama ilivyotokea wakati ule.

    "Serikali hii haikufanya kile ambacho serikali yangu ilifanya siku hiyo. Serikali yangu ilikuwa wazi na ilidhamiria kusema kwamba hatukujua, na hatukuwa tumearifiwa juu ya mpango wa Hezbollah wa kuvuka mpaka na kuteka nyara na kuua wanajeshi wa Israel.

    "Wakati huu hakujakuwa na hatua yoyote iliyofanywa na serikali ya Lebanon. Faida ya tulichofanya ni kwamba tuliweka mpaka kati ya serikali ya Lebanon na Lebanon upande mmoja, na Hezbollah kwa upande mwingine," alielezea.

    Siniora hajaegemea upande wowote katika tathmini yake ya uhuru uliopotea wa Lebanon.

    "Kiuhalisia, Lebanon kama taifa imetekwa nyara na Hezbollah. Na nyuma ya Hezbollah ni Iran.

    "Bunduki hii iliyokuwa inashikiliwa na Hezbollah, badala ya kunyooshewa Israel, ilianza kunyooshewa ndani ya nchi na ikaanza kutumika kama njia ya Iran kuingilia Syria, Iraq na Yemen. Lebanon haiwezi kujihusisha na vita vya namna hiyo.

    " Siniora pia alikuwa mmoja wa wasanifu wa azimio la UN 1701, makubaliano ambayo yalimaliza vita vya 2006.

    Soma zaidi:

  2. 'Jinsi Israeli inavyojilinda ni muhimu,' asema Kamala Harris

    Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amefanya mahojiano ya dakika 60 na shirika la habari la CBS News ambapo amebanwa kuhusu masuala kama vile Mashariki ya Kati, Ukraine, umiliki wa bunduki na uhamiaji.

    Katika mahojiano hayo yaliyorekodiwa, Harris aliulizwa nini Mashariki ya Kati inaweza kufanya kuzuia vita kuenea au hata kufikia kiwango cha "kutoweza kudhibitika".

    "Israel ina haki ya kujilinda," alisema. "Tungefanya hivyo. Na namna inavyofanya hivyo ni muhimu. Wapalestina wengi mno wasio na hatia wameuawa. Vita hivi lazima vikome," Harris alijibu.

    Pia aliulizwa jinsi Marekani ilivyomwomba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukubali kusitishwa kwa mapigano, ili kutoingia Lebanon - lakini maombi yote mawili yamepuuzwa.

    Harris alisema Marekani "haitaacha kutafuta kile ambacho ni muhimu kwa Marekani, kuwa wazi kuhusu wapi tunasimama ili vita hivi viishe".

    Aliongeza kuwa muungano wa Israel na Marekani bado ni imara.

    Soma zaidi:

  3. Israel yaadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio la Hamas huku mapigano yakiendelea

    Israel imefanya sherehe za kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya watu na utekaji nyara uliofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, huku mapigano yakiendelea katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

    Mwaka mmoja baada ya shambulio hilo - ambalo lilishuhudia takriban watu 1,200 wakiuawa na 251 kuchukuliwa mateka - Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliapa kusitisha shambulio kama hilo kutokea tena, akisema vikosi vya kijeshi vya Israel "vilikuwa vinabadilisha uhalisia wa hali ya usalama" eneo hilo.

    Tangu tarehe 7 Oktoba, karibu watu 42,000 wameuawa wakati wa mashambulizi ya Israel huko Gaza, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

    Wakati siku ya kumbukumbu hiyo ikiendelea, Israel ilisema imenasa zaidi ya makombora 100 yaliyorushwa na Hezbollah nchini Lebanon pamoja na makombora yaliyorushwa na Wahouthi wa Yemen na Hamas huko Gaza.

    Oktoba iliyopita, watu wenye silaha kutoka Hamas huko Gaza walivunja uzio wa mpaka na kuvamia vijiji vya karibu vya Israel, Kibbutzim, vituo vya kijeshi na tamasha la muziki la Nova.

    Siku ya Jumatatu, familia za mamia waliouawa na makumi ya watu waliochukuliwa mateka katika tamasha hilo walikusanyika kwenye eneo kwa hafla ya kumbukumbu ya kwanza ya siku hiyo.

    Wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao walisikiliza wimbo wa mwisho uliochezwa kwenye tamasha hilo kabla ya Rais wa Israel Isaac Herzog kuongoza kimya cha dakika moja saa 06:29, muda ambao shambulio hilo lilianza.

    Soma zaidi:

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 08/10/2024