Urusi ni 'tishio kubwa zaidi' kwa uchaguzi wa Marekani
Chanzo cha picha, Reuters
Jumuiya ya kijasusi ya Marekani imeelezea Urusi kama
"tishio kubwa zaidi" kwa uadilifu wa uchaguzi katika taarifa ya
pamoja iliyotolewa Jumatatu.
Ilitiwa saini na Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa
Kitaifa (ODNI), Ofisi ya Shirikisho ya Upelelezi (FBI) na Wakala wa Usalama wa
Mtandao na Miundombinu (CISA).
Katika tathmini yao, wanasema watu "wanaohusishwa na
Urusi haswa" wanatengeneza video na nakala za uwongo "kudhoofisha
uhalali wa uchaguzi, kuwatia hofu wapiga kura kuhusu mchakato wa uchaguzi, na
kupendekeza Wamarekani wanatumia vurugu dhidi ya kila mmoja wao kwa sababu ya
misimamo yao ya kisiasa
Iran yahimizwa kumwachilia mwanamke aliyezuiliwa baada ya kuvua nguo chuo kikuu
Chanzo cha picha, Telegram
Wanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito kwa mamlaka
nchini Iran kumwachilia mwanamke aliyekuwa kizuizini baada ya kuvua nguo chuo
kikuu, katika kile walichosema ni kupinga sheria za lazima za kuvaa hijab.
Video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya
Jumamosi ikimuonyesha mwanamke huyo akiwa amevaa nguo ya ndani huku ameketi
kwenye ngazi, kisha akatembea kwa utulivu kwenye barabara ya Tawi la Sayansi na
Utafiti la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad mjini Tehran.
Katika video ya pili, mwanamke huyo anaonekana kuvua
chupi yake. Muda mfupi baadaye, maafisa waliovalia kiraia wanaonekana
wakimshikilia kwa nguvu na kumsukuma ndani ya gari.
Chuo Kikuu cha Azad kilisema mwanamke huyo alikuwa na
"matatizo ya akili" na aamepelekwa "hospitali ya matatizo ya
akili".
Raia wengi wa Iran kwenye mitandao ya kijamii walitilia
shaka madai hayo na kueleza vitendo vyake kama sehemu ya vuguvugu linalojulikana
kama “Woman, Life, Freedom” ambalo limeshuhudia wanawake wengi wakipinga
hadharani sheria zinazowataka kufunika nywele zao na kuvaa nguo ndefu
zisizowabana.
Zaidi ya watu 500 waliripotiwa kuuawa wakati wa
maandamano ya nchi nzima yaliyozuka miaka miwili iliyopita baada ya mwanamke wa
Kikurdi, Mahsa Amini, kufariki akiwa mikononi mwa polisi baada ya kuzuiliwa kwa
kutovaa hijabu "vizuri".
Ilisema kichwa cha mwanamke huyo kiligonga mlango au
fremu ya gari la maafisa waliokuwa wamevalia kiraia wakati akizuiliwa na
kusababisha kuvuja damu na kupelekwa kusikojulikana.
Shahidi aliiambia BBC Persian kwamba mwanamke huyo
aliingia darasani mwao katika Chuo Kikuu cha Azad na kuanza kuwarekodi
wanafunzi. Wakati mhadhiri alipopinga hilo, aliondoka huku akipiga kelele.
Trump na Harris Trump na Harris wafanya mikutano yao katika majimbo muhimu
Kampeni inakaribia kufika mwisho lakini wagombea wote
wawili wana kule wanakoelekea dakika za lala salama kwenye shajara zao usiku wa
kumakia siku ya kupiga kura.
Trump atakuwa Grand Rapids, Michigan, ambapo wafuasi wa
chama cha Republican wamekuwa wakikusanyika kwa saa kadhaa kabla ya hotuba yake
ya mwisho ya kampeni hii.
Wakati huo huo, mkutano wa mwisho wa Kamala Harris huko
Philadelphia, Pennsylvania, tayari unaendelea, huku Katy Perry na Lady Gaga wakichangamsha
umati kabla ya makamu wa rais kuwasili.
Wote wawili wanamaliza kampeni hii katika majimbo muhimu
ambayo yanaweza kuamua ni nani atakuwa rais ajaye.
Idadi ya waliopiga kura mapema Marekani yapita milioni 81
Chanzo cha picha, Getty Images
Idadi ya waliopiga kura mapema nchini Marekani imepita
milioni 81, kulingana na Chuo Kikuu cha Florida
Election Lab.
Hadi mkesha wa kuamkia siku ya kupiga kura, watu 81,379,684,
tayari walikuwa wameshapiga kura, 44,402,375 wakiwa wamefika katika vituo vya
kupiga kura wenyewe huku kura 36,977,311 zikiwa zimepigwa kama barua kupitia
njia ya posta.
Kuna jambo moja tunaloweza kusema kwa hakika: Desturi za
kupiga kura za raia wa Marekani zimebadilika tangu kutokea kwa mlipuko wa Covid.
Ingawa idadi ya wapiga kura wa mapema mwaka huu haitapita
ile ya wakati wa janga la Covid, imezidi ile jumla ya kura za mapema
zilizopigwa mwaka wa 2016 (milioni 47.2) au 2012 (milioni 46.2).
Ingawa kila jimbo hushughulikia upigaji kura wa mapema
kwa njia tofauti na mengi yanazingatiwa.
Hata hivyo, maoni mengi kuhusu upigaji kura wa mapema yanatolewa
kulingana na data ya idadi ya watu pekee lakini huwezi kujua ni wagombea kina
nani wamepigiwa kura hadi siku ya kuanza kutolewa kwa matokeo.
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja. Ni siku ambayo nchini Marekani wanaamkia kupiga kura, tutakufahamisha jinsi shughuli hiyo inavyoendelea.