Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Trump apiga kura huko Florida huku mamilioni wakimpigia kura rais ajaye wa Marekani

Baada ya kampeni kali ya miezi kadhaa kati ya Kamala Harris na Donald Trump, Marekani itachagua rais wake ajaye.

Muhtasari

  • Wauaji wa mwanariadha wa Uganda wahukumiwa kifungo cha miaka 35
  • Uchaguzi wa Marekani 2024: Tunachojua kufikia sasa
  • Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amfuta kazi waziri wa ulinzi Gallant
  • Waziri wa Georgia asema vitisho vya mabomu vilitoka Urusi
  • FBI yatoa onyo jingine kuhusu video ghushi za uchaguzi
  • 'Acha kuzungumzia hilo': Trump akwepa swali la kura ya utoaji mimba
  • Harris awataka Wamarekani 'kutoka na kupiga kura' katika mahojiano ya redio
  • Trump apiga kura katika eneo la Palm Springs akiwa na mkewe Melania
  • Vitisho vya uwongo vya mabomu vyasababisha wapiga kura kuhama Georgia
  • Bangladesh yaimarisha malipo kwa kampuni ya Adani kuzuia kukatwa kwa usambazaji umeme
  • Mgomo wa wanyakazi wa Boeing wamalizika
  • Kesi ya kukatwa kichwa kwa mwalimu aliyeonyesha katuni ya Mtume Muhammad yaanza kusikilizwa
  • Equtoarial Guinea kuwachukulia hatua wafanyakazi wa umma waliofanya mapenzi ofisini
  • Elon Musk anaweza kuendelea kutoa $1m kwa wapiga kura, jaji aamua
  • Urusi ni 'tishio kubwa zaidi' kwa uchaguzi wa Marekani
  • Iran yahimizwa kumwachilia mwanamke aliyevua nguo chuo kikuu
  • Trump na Harris wafanya mikutano yao katika majimbo muhimu
  • Idadi ya waliopiga kura mapema Marekani yapita milioni 81

Moja kwa moja

Na Asha Juma,Lizzy Masinga & Dinah Gahamanyi

  1. Urusi ni 'tishio kubwa zaidi' kwa uchaguzi wa Marekani

    Jumuiya ya kijasusi ya Marekani imeelezea Urusi kama "tishio kubwa zaidi" kwa uadilifu wa uchaguzi katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatatu.

    Ilitiwa saini na Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa (ODNI), Ofisi ya Shirikisho ya Upelelezi (FBI) na Wakala wa Usalama wa Mtandao na Miundombinu (CISA).

    Katika tathmini yao, wanasema watu "wanaohusishwa na Urusi haswa" wanatengeneza video na nakala za uwongo "kudhoofisha uhalali wa uchaguzi, kuwatia hofu wapiga kura kuhusu mchakato wa uchaguzi, na kupendekeza Wamarekani wanatumia vurugu dhidi ya kila mmoja wao kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa

    Soma zaidi:

  2. Iran yahimizwa kumwachilia mwanamke aliyezuiliwa baada ya kuvua nguo chuo kikuu

    Wanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito kwa mamlaka nchini Iran kumwachilia mwanamke aliyekuwa kizuizini baada ya kuvua nguo chuo kikuu, katika kile walichosema ni kupinga sheria za lazima za kuvaa hijab.

    Video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi ikimuonyesha mwanamke huyo akiwa amevaa nguo ya ndani huku ameketi kwenye ngazi, kisha akatembea kwa utulivu kwenye barabara ya Tawi la Sayansi na Utafiti la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad mjini Tehran.

    Katika video ya pili, mwanamke huyo anaonekana kuvua chupi yake. Muda mfupi baadaye, maafisa waliovalia kiraia wanaonekana wakimshikilia kwa nguvu na kumsukuma ndani ya gari.

    Chuo Kikuu cha Azad kilisema mwanamke huyo alikuwa na "matatizo ya akili" na aamepelekwa "hospitali ya matatizo ya akili".

    Raia wengi wa Iran kwenye mitandao ya kijamii walitilia shaka madai hayo na kueleza vitendo vyake kama sehemu ya vuguvugu linalojulikana kama “Woman, Life, Freedom” ambalo limeshuhudia wanawake wengi wakipinga hadharani sheria zinazowataka kufunika nywele zao na kuvaa nguo ndefu zisizowabana.

    Zaidi ya watu 500 waliripotiwa kuuawa wakati wa maandamano ya nchi nzima yaliyozuka miaka miwili iliyopita baada ya mwanamke wa Kikurdi, Mahsa Amini, kufariki akiwa mikononi mwa polisi baada ya kuzuiliwa kwa kutovaa hijabu "vizuri".

    Ilisema kichwa cha mwanamke huyo kiligonga mlango au fremu ya gari la maafisa waliokuwa wamevalia kiraia wakati akizuiliwa na kusababisha kuvuja damu na kupelekwa kusikojulikana.

    Shahidi aliiambia BBC Persian kwamba mwanamke huyo aliingia darasani mwao katika Chuo Kikuu cha Azad na kuanza kuwarekodi wanafunzi. Wakati mhadhiri alipopinga hilo, aliondoka huku akipiga kelele.

    Soma zaidi:

  3. Trump na Harris Trump na Harris wafanya mikutano yao katika majimbo muhimu

    Kampeni inakaribia kufika mwisho lakini wagombea wote wawili wana kule wanakoelekea dakika za lala salama kwenye shajara zao usiku wa kumakia siku ya kupiga kura.

    Trump atakuwa Grand Rapids, Michigan, ambapo wafuasi wa chama cha Republican wamekuwa wakikusanyika kwa saa kadhaa kabla ya hotuba yake ya mwisho ya kampeni hii.

    Wakati huo huo, mkutano wa mwisho wa Kamala Harris huko Philadelphia, Pennsylvania, tayari unaendelea, huku Katy Perry na Lady Gaga wakichangamsha umati kabla ya makamu wa rais kuwasili.

    Wote wawili wanamaliza kampeni hii katika majimbo muhimu ambayo yanaweza kuamua ni nani atakuwa rais ajaye.

    Soma zaidi:

  4. Idadi ya waliopiga kura mapema Marekani yapita milioni 81

    Idadi ya waliopiga kura mapema nchini Marekani imepita milioni 81, kulingana na Chuo Kikuu cha Florida Election Lab.

    Hadi mkesha wa kuamkia siku ya kupiga kura, watu 81,379,684, tayari walikuwa wameshapiga kura, 44,402,375 wakiwa wamefika katika vituo vya kupiga kura wenyewe huku kura 36,977,311 zikiwa zimepigwa kama barua kupitia njia ya posta.

    Kuna jambo moja tunaloweza kusema kwa hakika: Desturi za kupiga kura za raia wa Marekani zimebadilika tangu kutokea kwa mlipuko wa Covid.

    Ingawa idadi ya wapiga kura wa mapema mwaka huu haitapita ile ya wakati wa janga la Covid, imezidi ile jumla ya kura za mapema zilizopigwa mwaka wa 2016 (milioni 47.2) au 2012 (milioni 46.2).

    Ingawa kila jimbo hushughulikia upigaji kura wa mapema kwa njia tofauti na mengi yanazingatiwa.

    Hata hivyo, maoni mengi kuhusu upigaji kura wa mapema yanatolewa kulingana na data ya idadi ya watu pekee lakini huwezi kujua ni wagombea kina nani wamepigiwa kura hadi siku ya kuanza kutolewa kwa matokeo.

    Soma zaidi:

  5. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja. Ni siku ambayo nchini Marekani wanaamkia kupiga kura, tutakufahamisha jinsi shughuli hiyo inavyoendelea.