Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

John Heche ataka Tundu Lissu aachiliwe bila masharti

Tundu Lissu amekuwa mahabusu kwa siku 307 akikabiliwa na kesi ya uhaini ambapo leo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania

Muhtasari

Moja kwa moja

Mariam Mjahid & Rashid Abdallah

  1. Mshauri wa spika wa Iran:Trump na Netanyahu wanakutana kujadili kushambulia Iran, sio mazungumzo

    Wakati huo huo, Mshauri wa spika wa bunge la Iran anasema kuwa mada ya mkutano wa wiki hii kati ya Waziri Mkuu wa Israel na Rais wa Marekani itakuwa ni shambulizi dhidi ya Iran.

    Mehdi Mohammadi aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Trump na Netanyahu watajadili "operesheni" na sio mazungumzo." Mshauri wa kimkakati Mohammad Baqer Qalibaf aliongeza kuwa "hakuna utata kuhusu hili."

    Ofisi ya Benjamin Netanyahu ilitangaza kwamba anapanga kukutana na Donald Trump huko Washington Jumatano ili kujadili mazungumzo na Iran.

    Wawakilishi wa Iran na Marekani walikutana tena mjini Muscat Ijumaa iliyopita, na upatanishi wa Oman, baada ya mapumziko ya miezi kadhaa.

    Awali Israel ilisema kuwa haina haja ya kufanya mazungumzo na utawala wa sasa wa Iran kwani nchi jirani zinataka mabadiliko ya uongozi.

    Soma pia:

  2. Makubaliano yoyote kati ya Iran na Marekani hayana maana - Israel

    Waziri wa nishati wa Israel amesema kuwa makubaliano yanayoweza kufikiwa kati ya Washington na Tehran hayana maana yoyote.

    “Hakuna thamani yoyote katika kufanya makubaliano na utawala wa sasa. Mabadiliko ya utawala mjini Tehran yako katika maslahi ya nchi zote za Kiislamu zinazoizunguka Iran,” Eli Cohen aliliambia chombo cha habari cha Israel, Ynet, siku ya Jumapili.

    Bw. Cohen alisisitiza: “Hata kama makubaliano yatafikiwa, iwapo tishio litatokea dhidi ya Israel na tutalazimika kuchukua hatua, tutachukua hatua.”

    Wawakilishi wa Iran na Marekani walifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Muscat siku ya Ijumaa, yakisimamiwa na Oman.

    Muda na mahali pa mkutano unaofuata bado havijatangazwa.

    Baraza la mawaziri la usalama la Israel, ambalo Eli Cohen ni mjumbe wake, linatarajiwa kukutana leo.

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anasafiri kwenda Washington siku ya Jumatano kwa ajili ya kuzungumza na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mazungumzo na Iran.

    Soma zaidi:

  3. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ya tarehe 09/02/2026.