Safari ya Rigathi Gachagua kama Naibu wa Rais wa Kenya yafika tamati
Gachagua alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge la Seneti mchana huu lakini wakati wake wa kujitokeza bungeni ulipofika, hakuwepo.
Muhtasari
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua hospitalini huku Seneti ikiendelea kujadili hoja ya kumuondoa madarakani
Kesi ya kumuondoa Gachagua madarakani kuamuliwa Jumamosi
Sinwar ndiye mlengwa mkuu wa Israel huko Gaza
'Tathmini zaidi' zinaonesha Sinwar amefariki dunia, duru zaiambia BBC
Naibu Rais Gachagua ana 'maumivu makali ya kifua'- asema wakili Muite
Israel 'inaangalia uwezekano' kwamba ilimuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar huko Gaza
Liam Payne: Tunachojua kuhusu kifo cha nyota huyo wa muziki
Naibu Jaji: Majaji watafuata utaratibu wa katiba kesi ya Gachagua ikirejea mahakamani
Naibu Rais Rigathi Gachagua ni mgonjwa na yuko hospitalini - Wakili Paul Muite
Bangladesh yatoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa zamani Hasina
Katiba ya Korea Kaskazini sasa yaitaja Korea Kusini kuwa 'nchi hasimu'
Marekani inaifuatilia Israel kuhakikisha haiendeshi 'sera ya kuwaangamiza watu kwa njaa' huko Gaza
HRW: Tanzania izingatie haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
Wanne mbaroni Tanzania kwa kumuua mume wa mdaiwa mkopo
Jeshi la Rwanda lakanusha madai ya kuwabaka wanawake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Marekani yashambulia hifadhi za silaha za Wahouthi zilizofichwa chini ya ardhi
Rigathi Gachagua:Je, ni kesi gani haswa inayomuandama naibu rais katika seneti?
Marekani kutenga dola milioni 425 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, huku Australia ikipeleka vifaru 49 vya Abrams
Rigathi Gachagua: Bunge la Seneti Kenya kupiga kura kuhusu hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais
Mbunge aliyewasilisha hoja ya kumuondoa naibu wa rais bungeni Kenya ajipata mashakani
Meya na watu wengine 15 waliuawa katika shambulio la Israeli kwenye mkutano wa baraza la Lebanon
Moja kwa moja
Na Asha Juma, Ambia Hirsi & Dinah gahamanyi
Rigathi Gachagua: Bunge la Seneti Kenya kupiga kura kuhusu hoja ya kumuondoa madarakani naibu rais
Chanzo cha picha, EPA
Baraza la juu la bunge la Kenya
linatazamiwa kupiga kura Alhamisi iwapo litamuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua
mamlakani katika sakata ya kisiasa ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini Kenya.
Bunge la
Seneti litatoa uamuzi wake mwishoni mwa siku ya pili ya kesi ya kuondolewa
madarakani dhidi ya Naibu huyo wa Rais.
Hii
inafuatia kura ya kihistoria iliyopigwa
wiki iliyopita katika bunge la kitaifa,
kumshtaki Gachagua kwa mashtaka 11 yakiwemo ufisadi, uasi, kuidhoofisha
serikali na kutekeleza siasa za migawanyiko ya kikabila.
Kesi katika Baraza la Seneti ilianza Jumatano baada ya Bw
Gachagua mwenye umri wa miaka 59, ambaye
pia anajulikana kama "Riggy G", kushindwa katika jitihada nyingi za
mahakama kusitisha mchakato huo.
Anatarajiwa kutoa ushahidi atakapojitetea mbele ya seneti siku
ya Alhamisi.
Mbunge aliyewasilisha hoja ya kumuondoa naibu wa rais bungeni Kenya ajipata mashakani
Chanzo cha picha, Senete Kenya/ X
Maelezo ya picha, Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse
Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi
Mutuse alijipata katika hali ngumu siku ya Jumatano wakati alipokuwa
akihojiwa ndani ya Seneti katika kesi ya kuondolewa madarakani aliyowasilisha kwa bunge dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Naibu Rais Rigathi Gachagua kupitia mawakili wake
wazoefu wanaoongozwa na Wakili Paul Muite wanapambana kuhakikisha haondolewi
mamlakani baada ya Bunge la taifa mnamo Oktoba 8 kupiga kura kuidhinisha
kutimuliwa kwake.
Mutuse alipata kibarua kigumu kujibu maswali makali ya
wakili wa Gachagua Elisha Ongoya ambaye aliupinga ushahidi wake mkuu dhidi ya
Bw Gachagua.
Miongoni mwa tuhuma ambazo wanasheria wa Gachagua
walitaka kuzifuta ni pamoja na kuihujumu serikali kwa kupinga hadharani sera
zake za kuwahamisha wafanyabiashara kutoka soko la wakulima na kuwapeleka
katika eneo jipya katika Barabara ya Outering na ubomoaji wa majengo katika
maeneo ya mabondeni.
Timu ya Gachagua ilitumia kanda za video kuwadhihirishia
maseneta kuwa alitoa matamshi akiiomba serikali kuwatendea raia utu na zile
zilizoonyesha kuwa baadhi ya kauli zilizotajwa kuchochea ukabila zimekuwa
zikitumiwa tangu awali pia na Rais william Ruto na kwamba zilikuwa msingi wa ugavi wa madaraka katika serikali ya sasa ya Kenya Kwanza .
Mawakili wa Gachagua walitoa video ambapo alitoa
matamshi akiiomba serikali kuwatendea raia utu kwa kuzingatia ahadi zake za
kabla ya kampeni.
“Naibu Rais
anasema ‘Tusiwe na vita na Wananchi.’. Je, unaona jambo lolote la kuudhi katika
taarifa hiyo?” Ongoya alimuuliza, Mutuse aliyejibu , hapana.
"Anatoa
wito wa huruma kwa wananchi. Je, unaona jambo lolote la kukera katika sehemu hiyo?” wakili aliuliza.
Chanzo cha picha, Senete
Maelezo ya picha, Rigadhi gachagua alikanusha mashtaka yote dhidi yake
Wakati mmoja kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea wakili wa Gachagua, alicheza kanda ya video ambapo Rais Ruto alionekana kwenye mkutano akiwaambia wananchi wa eneo la Mlima Kenya kuwa wana 'share' (hisa) katika serikali- kauli ambayo bunge linasema imekuwa ikitumiwa na Gachagua na inachochea ukabila. Gachagua alisema alijifunza kutumia kauli hiyo kutoka kwa Rais Ruto.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa na seneti leo asubuhi.
Meya na wengine 15 wauawa katika shambulio la Israeli kwenye mkutano wa baraza la Lebanon
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Gavana wa Nabatieh alisema idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka kwani bado wanasaka miili katika vifusi
Mratibu
maalum wa shughuli za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon ameikosoa Israel
baada ya mashambulizi ya anga kwenye majengo ya manispaa katika mji wa kusini
wa Nabatieh kumuua meya na watu wengine 15.
Jeanine
Hennis-Plasschaert aameyaita mauaji ya
meya Ahmad Kahil "ya kutisha" na kusema ukiukaji wowote wa sheria za
kimataifa za kibinadamu "haukubaliki kabisa".
Takriban watu watano kati ya waliouawa katika shambulio la Jumatano walikuwa wafanyakazi wa manispaa
walioratibu misaada kwa ajili ya raia
waliosalia katika eneo hilo, Gavana wa Nabatiyeh Howaida Turk ameiambia BBC.
Kaimu Waziri mkuu wa Lebanon,
Najib Mikati amelaani shambulio hilo, akisema "lililenga" mkutano wa
baraza.
Shambulio hilo lilikuwa kubwa zaidi dhidi
ya jengo la serikali ya Lebanon tangu kuongezeka kwa mapigano ya hivi karibuni,
ambayo yalianza takriban wiki mbili zilizopita, na limezua wasiwasi juu ya
usalama wa miundombinu ya serikali ya nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi la Israel amesema vikosi
vyake vimefanya mashambulizi yakilenga makumi ya maeneo ya Hezbollah katika
eneo hilo na kuharibu handaki linalotumiwa na kundi hilo linaloungwa mkono na
Iran.
"Tunajua kwamba Hezbollah mara nyingi
hutumia fursa ya vituo vya kiraia," balozi wa Umoja wa Mataifa wa Israel
Danny Danon alisema katika mkutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York Jumatano.