Rais Trump atia saini hati ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza katika mkutano wa kilele wa amani Misri
Mpango wa amani wa Trump wenye vipengele 20 unasema Gaza itasimamiwa na kamati ya muda ya mpito ya wanateknolojia wa Palestina - inayosimamiwa na "Bodi ya Amani" inayoongozwa na Trump.
Muhtasari
Trump atia saini hati ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza katika mkutano wa kilele wa amani
Habari za hivi punde, IDF yapokea mateka saba wa kwanza
Chanzo cha picha, IDF
Jeshi la Israeli limethibitisha kuwa mateka saba wa kwanza
sasa wamepokelewa na Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF).
Wizara ya mambo ya nje ya Israel imethibitisha majina ya mateka saba wa kwanza walioachiliwa kutoka Hamas asubuhi ya leo:
Eitan Mor
Gali Berman
Ziv Berman
Omri Miran
Alon Ohel
Guy Gilboa-Dalal
Matan Angrest
Imeshiriki majina hayo katika machapisho kwenye mitandao ya kijamii, na picha za mateka kando yake na nukuu inayosomeka: "Karibu nyumbani."
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Eitan Mor alitekwa nyara katika shambulio la Oktoba 7, 2023
Machozi na furaha yashuhudiwa huko Tel Aviv kuachiliwa kwa mateka kulipoanza
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Reuters
Habari za hivi punde, Hamas yathibitisha imewakabidhi mateka - Reuters
Hamas imethibitisha kuwa imewakabidhi mateka saba wa
kwanza kwa Shirika la Msalaba Mwekundu, kulingana na shirika la kwanza la
Reuters
Habari za hivi punde, Hamas imeanza kuwaachilia huru mateka wa Israel huko Gaza
Mateka wa kwanza wa Israel sasa wamehamishwa kutoka Hamas
hadi kwenye Shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza, afisa aliyehusika katika
operesheni hiyo ameliambia shirika la habari la Reuters.
Mateka saba wa Israel waripotiwa kukabidhiwa na Hamas
Bado tunasubiri uthibitisho rasmi kutoka kwa jeshi la
Israeli na ICRC, lakini vyombo vya habari vya Israeli vinaripoti kwamba mateka
saba wa Israeli wameachiliwa huru na Hamas na sasa wako chini ya Shirika la
Msalaba Mwekundu
Eitan
Mor
Gali
Berman
Ziv
Berman
Matan
Angrest
Omri
Miran
Alon
Ehal
Guy
Gilboa Dallal
Mali yaweka ada ya viza ya $10,000 kwa wageni wa Marekani
Chanzo cha picha, Tribune News Service via Getty Images
Mali
imetangaza kuwa raia wa Marekani wanaotembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi
watatakiwa kulipia ada ya hadi $10,000 (£7,500) kwa ajili ya viza za biashara
na utalii, ili kukidhi matakwa sawa na hayo ambayo utawala wa Trump umeweka kwa
raia wake.
Ubalozi wa
Marekani nchini Mali ulisema siku ya Ijumaa ada hiyo ilianzishwa ili kuimarisha
"dhamira ya Marekani ya kulinda mipaka ya Marekani na kulinda usalama wa
taifa la Marekani".
Wizara ya
mambo ya nje ya Mali ilisema Jumapili kwamba ada hiyo iliwekwa kwa kuegemea upande
mmoja, na imeamua "kuanzisha mpango wa viza sawa na huo" kwa raia wa
Marekani.
Mabadiliko
ya sera ya viza yanakuja licha ya hatua za kuboresha uhusiano wa kidiplomasia
kati ya nchi hizo mbili.
Trump asema huenda akatuma makombora ya Tomahawk nchini Ukraine
Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa
Marekani Donald Trump anafikiria kutuma makombora ya masafa marefu ya Tomahawk
nchini Ukraine, akisema itakuwa "hatua mpya" katika vita vyake na
Urusi.
Alipoulizwa
kwenye Air Force One kama angetuma Tomahawks nchini Ukraine, Trump alijibu
"tutaona... naweza".
Hii inafuatia
simu ya pili mwishoni mwa juma kati ya Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr
Zelensky, ambaye alishinikiza kuwepo kwa uwezo mkubwa wa kijeshi kuanzisha
mashambulizi ya kukabiliana na Urusi.
Hapo awali
Moscow iliionya Washington dhidi ya kutoa makombora ya masafa marefu kwa Kyiv,
ikisema kuwa hatua hiyo itasababisha kuongezeka kwa mzozo huo na kuzorotesha
uhusiano kati ya Marekani na Urusi.
China yaishutumu Marekani kwa 'uonevu' juu ya tishio la ushuru
Chanzo cha picha, Getty Images
Tishio la
hivi punde la Donald Trump la kutoza ushuru wa ziada wa 100% kwa bidhaa za
China ni "mfano wa kawaida wa uonevu wa Marekani", serikali ya China
imesema.
Msemaji wa
wizara ya biashara pia alisema China inaweza kuanzisha "hatua" zake
ambazo hazijabainishwa ikiwa rais wa Marekani atatekeleza tishio lake, akiongeza
kuwa "haiogopi" uwezekano wa vita vya kibiashara.
Siku ya
Ijumaa, Trump alijibu hatua ya Beijing ya kutekeleza sheria kali za mauzo ya madini
adimu, akiishutumu kwa "kuwa na uadui" na kujaribu "kushikilia"
ulimwengu. Pia alitishia kujiondoa katika mkutano na Rais wa China Xi Jinping
baadaye mwezi huu.
Lakini siku
ya Jumapili, Trump aliandika: "Usijali kuhusu China, yote yatakuwa
sawa!"
Mapigano yamezuka kati ya vikosi vya Hamas na wanaukoo wenye silaha katika mji wa Gaza
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Takriban watu 27 wameuawa katika mapigano makali kati ya
vikosi vya usalama vya Hamas na watu wenye silaha wa familia ya Dughmush katika
mji wa Gaza, katika moja ya makabiliano makali zaidi ya ndani tangu kumalizika
kwa operesheni kuu za Israel katika eneo hilo.
Wanachama wa Hamas waliokuwa wamejifunika yuso walirushiana
risasi na wapiganaji wa koo karibu na hospitali ya mji wa Jordan, walioshuhudia
walisema.
Afisa mkuu katika wizara ya mambo ya ndani inayoongozwa na
Hamas alisema vitengo vya usalama viliwazingira na kushiriki katika mapigano
makali kuwazuilia.
Wizara hiyo ilisema wanachama wake wanane waliuawa katika
"shambulio la silaha na wanamgambo".
Duru za kimatibabu zilisema watu 19 wa ukoo wa Dughmush na
wapiganaji wanane wa Hamas wameuawa tangu mapigano yaanze siku ya Jumamosi.
Waisraeli wakusanyika kusubiri mateka 'huku Trump akisema' Vita vimekwisha 'Gaza
Chanzo cha picha, Getty Images
Hamas
inatazamiwa kuwaachilia mateka 48 waliosalia Gaza ifikapo saa sita
mchana (09:00 GMT). Kati ya hao, 20 wanaaminika kuwa hai, na wanatarajiwa
kupelekwa haraka kwa matibabu kabla ya kuunganishwa tena na wapendwa wao. Miili
ya wengine 28 inastahili kurejeshwa.
Haya
yanajiri wakati Rais wa Marekani Donald Trump anafanya ziara nchini Israel kufuatia
makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani, Misri na Qatar.
Trump atalihutubia
bunge la Israel kabla ya kusafiri hadi mji wa wa Misri wa Sharm El-Sheikh
kuandaa mkutano wa kilele wa amani katika Mashariki ya Kati, utakaojumuisha
takriban viongozi wengine 20 wa dunia.
Trump
atapokelewa na "makundi ya Waisraeli kwa shukrani na urafiki", Rais
wa Israel Isaac Herzog alisema Jumapili, huku Waisraeli wengi wakimsifu rais wa
Marekani kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kwa
mabadilishano ya kurejesha mateka hao, Israel itawaachia huru wafungwa 250
wa Kipalestina, wakiwemo wanaotumikia kifungo cha maisha jela. Hiyo ni pamoja
na kuwaachilia zaidi ya wafungwa 1,700 waliokuwa wakizuiliwa bila kufunguliwa
mashtaka katika kipindi cha vita - wakiwemo karibu Watoto zaidi ya kumi.
Kwingineko, malori
yaliyobeba misaada yanavuka mpaka na kuingia Gaza huku Wapalestina,
waliohamishwa kwa nguvu kuelekea kusini kutokana na mashambulizi ya Israel,
wakiendelea kurejea eneo la kaskazini mwa eneo hilo. Wanakumbana na uharibifu uliotokea,
maeneo makubwa ya Jiji la Gaza yakiwa vifusi.