Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Jeshi la Madagascar lasema limenyakua mamlaka - ripoti

Hii ni baada ya Wabunge kupiga kura kumuondoa madarakani Rais Andry Rajoelina.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma, Lizzy Masinga & Ambia Hirsi

  1. Rais wa Madagascar asema 'nimejificha mahali salama' huku akionya kuhusu jaribio la mapinduzi

    Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema "nimejificha mahali salama" baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kumtaka ajiuzulu.

    Katika matangazo ya moja kwa moja kwa taifa kupitia ukurasa wa Facebook, Rajoelina, 51, alisema "kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua".

    Hakufichua eneo aliko, lakini ripoti ambazo hazijathibitishwa awali zilidokeza kwamba alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

    Hilo limetokea baada ya maandamano ya nchi nzima, hasa yakiongozwa na vijana, yenye lengo la kumuondoa madarakani.

    Jaribio lililofeli la Rajoelina kuwatuliza waandamanaji hao vijana - walioitwa "Gen Z Mada" - lilimshuhudia rais akiifuta kazi serikali yake yote na kufanya makubaliano mengine bila mafanikio.

    Hajaonekana tangu Jumatano, na mwishoni mwa wiki ofisi ya Rajoelina ilisema jaribio lilikuwa linaendelea kumlazimisha kuondoka madarakani.

    Hotuba yake kwa taifa ilicheleweshwa mara kadhaa Jumatatu huku kukiwa na machafuko, wanajeshi nao wakitishia kuteka makao makuu ya Televisheni ya taifa katika kisiwa cha Bahari ya Hindi.

    Hatimaye, katika matangazo ya Facebook alisema: "Tangu Septemba 25, kumekuwa na majaribio ya kuniua na ya kufanya mapinduzi. Kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua.

    "Nililazimika kutafuta mahali salama ili kulinda maisha yangu."

    "Kuna njia moja tu ya kutatua masuala haya; ambayo ni kuheshimu katiba inayotumika nchini".

    Soma zaidi:

  2. Trump atangaza mwisho wa vita vya Gaza

    Hamas iliwaachilia mateka wa mwisho wa Israel kutoka Gaza Jumatatu chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, na Israeli iliwarudisha nyumbani mabasi ya wafungwa wa Kipalestina, huku Rais wa Marekani Donald Trump akitangaza kumalizika kwa vita vya miaka miwili Mashariki ya Kati.

    Saa kadhaa baadaye, Trump aliwaita viongozi wa Kiislamu na Ulaya nchini Misri kujadili mustakabali wa Ukanda wa Gaza na uwezekano wa kupatikana kwa amani ya eneo hilo, hata kama Hamas na Israel, zote hazikuwepo kwenye mkutano huo, bado hazijakubaliana juu ya hatua zinazofuata.

    Jeshi la Israel limesema limepokea mateka wote 20 waliothibitishwa kuwa hai, baada ya kuhamishwa kutoka Gaza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Tangazo hilo lilisababisha kushangiliwa, kukumbatiana na kulia miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa wakisubiri kwenye uwanja wa "Hosta Square" huko Tel Aviv.

    Huko Gaza, maelfu ya jamaa, wengi wakilia kwa furaha, walikusanyika katika hospitali ambapo mabasi yaliwarudisha nyumbani baadhi ya wafungwa 2,000 wa Kipalestina na waliokuwa wanazuiliwa na Israel kama sehemu ya makubaliano hayo.

    "Anga ni shwari, bunduki ziko kimya, ving'ora vimetulia na jua linachomoza kwenye ardhi ambayo hatimaye imepata amani," Trump aliambia Knesset, bunge la Israeli, akisema "jinamizi" kwa Waisraeli na Wapalestina limekwisha.

    Soma zaidi:

  3. Hujambo. Karibu katika matangazo yetu mubashara ya leo, tarehe ni 14/10/2025.