Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Kamanda wa Hezbollah auawa katika shambulio la Israel - ripoti

Makumi ya watu wamejeruhiwa katika shambulizi la Israel dhidi ya mji mkuu wa Lebanon huku makabiliano ya mpakani yakiongezeka.

Muhtasari

  • Magari ya kubebea wagonjwa yawasili katika hospitali za Beirut huku 59 wakijeruhiwa
  • Israel inachunguza tukio la wanajeshi wake kurekodiwa wakitupa miili ya watu kutoka juu ya paa
  • Kamanda wa Hezbollah auawa katika shambulizi la Israel – Ripoti
  • Watu tisa wameuawa, 59 kujeruhiwa - wizara ya afya ya Lebanon
  • Wapalestina 14 wauawa katika mashambulizi ya hivi punde zaidi ya Israel
  • IDF yathibitisha roketi 140 zimerushwa kutoka Lebanon
  • Moshi waongezeka karibu na kijiji cha kusini mwa Lebanon
  • Hezbollah yaanzisha mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Israel
  • Makombora yarushwa Israel kutoka Lebanon, yasema IDF
  • Rwanda yaanza kutoa chanjo ya Mpox
  • India yakanusha ripoti ya uhamishaji wa silaha kwenda Ukraine ikisema "ni uvumi"
  • Kiongozi wa Hezbollah aita mashambulizi 'tangazo la vita'
  • IDF yasema shambulio lililenga 'kudunisha' uwezo wa Hezbollah
  • Mwanaharakati aliyetekwa nyara Bob Njagi yuko hai - Rais wa wanasheria
  • Stoltenberg: Kadiri NATO inavyoipa Ukraine silaha, ndivyo fursa ya kupatikana amani inavyoongezeka
  • Israel yasema imepiga mitambo 100 ya makombora ya Hezbollah nchini Lebanon
  • Zaidi ya watu 70,000 waliojitolea kuipigania Urusi wafa Ukraine

Moja kwa moja

Asha Juma, Ambia Hirsi & Lizzy Masinga

Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu