China yawasilisha kesi ikisema ushuru wa Trump ni wa 'kibaguzi'
China imeishutumu Marekani kwa kutoa "madai yasiyo ya msingi na ya uwongo" juu ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya za fentanyl, ili kuhalalisha nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za China.
Malalamiko hayo yamewasilishwa katika Shirika la Biashara Duniani (WTO), siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kupandisha ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka China kwa asilimia 10, hatua ambayo amesema inalenga kukabiliana na wimbi la dawa haramu.
Katika kesi hilo, China inasema hatua hiyo ni ya "kibaguzi na inalinda bidhaa za ndani dhidi ya ushindani kutoka nje" na hivyo kukiuka sheria za biashara.
Lakini Wataalamu wanaamini si rahisi kwa China kupata uamuzi utakao juu ya kesi hiyo, kwani jopo linalohusika kutatua mizozo ya kibiashara halifanyi kufanya kazi kwa sasa. Afisa mmoja wa zamani wa WTO ameiambia BBC "hakuna uwezekano wa kufanikiwa."
Trump amesema ushuru huo utachajihisha makampuni kutengeneza bidhaa zao nchini Marekani, akieleza wasiwasi wake kuhusu ukubwa wa nakisi ya biashara ya Marekani.
Lakini hatua yake dhidi ya China – akitishia kuijumuisha Canada, Mexico na Ulaya - zimezua wasiwasi juu ya athari zao kwa uchumi wa kimataifa, pamoja na Marekani yenyewe, huku wafanyabiashara wakikosa uhakika wa biashara zao na kusimamisha uwekezaji au kuweka gharama mpya kwa wateja.
Sheertex, kampuni ya utengenezaji wa nguo huko Canada, siku ya jana ilitangaza inapunguza kwa muda 40% ya wafanyikazi wake karibu 350, kwa sababu ya sakata la ushuru.
Pia unaweza kusoma: