Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Ndege ya abiria yatua baharini kwa dharura Mogadishu

Vikundi vya kutoa msaada vilitumwa mara moja, na watu wote 55 walihamishwa hadi eneo salama

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid & Asha Juma

  1. Wapalestina waituhumu Israel kwa 'kunyakua ardhi' katika Ukingo wa Magharibi

    Wapalestina, nchi za Kiarabu, makundi ya Waisraeli yanayopinga uvamizi, pamoja na Uingereza, wamezikosoa vikali hatua mpya zilizoidhinishwa na baraza la usalama la Israel kuhusu Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Wanasema hatua hizo ni sawa na kudhibiti rasmi eneo hilo kwa vitendo.

    Hatua hizo zilitangazwa na Waziri wa Hazina wa Israel mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich. Alisema zitafanya iwe rahisi zaidi kwa walowezi wa Kiyahudi kuchukua ardhi ya Wapalestina. Aliongeza akisema: “Tutaendelea kuua wazo la taifa la Palestina.”

    Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, makazi yote ya walowezi yanachukuliwa kuwa haramu.

    Hatua hizo ambazo zinatarajiwa kuidhinishwa rasmi na kamanda mkuu wa kijeshi wa Israel anayesimamia Ukingo wa Magharibi, zinalenga kuongeza udhibiti wa Israel katika eneo hilo, hasa katika masuala ya umiliki wa ardhi, mipango ya ujenzi, utoaji wa vibali na utekelezaji wa sheria.

    Wapalestina wamesema wana hofu kuwa mabadiliko hayo yataongeza shinikizo kwa watu binafsi kuuza ardhi yao, pamoja na kusababisha vitendo vya kughushi hatimiliki na udanganyifu.

    Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas ambaye anaongoza Mamlaka ya Palestina (PA) inayosimamia sehemu za Ukingo wa Magharibi, alizitaja hatua hizo kuwa “hatari” na kuwa ni “jaribio la wazi la Israel kuhalalisha upanuzi wa makazi ya walowezi, kunyang’anya ardhi na kubomoa mali za Wapalestina, hata katika maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya Palestina.”

    Abbas amezitaka Marekani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati mara moja.

    Kwa pamoja, mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Pakistan, Uturuki, Saudi Arabia na Qatar wamesema tangazo hilo “linaharakisha juhudi haramu za kuitwaa Ukingo wa Magharibi na kuwafukuza wananchi wa Palestina.”

    Soma Pia:

  2. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki: Utawala wa Iran hauwezi kuangushwa kwa shambulio la anga

    Katika mahojiano na CNN Turkey, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, alizungumza kwa kina kuhusu Iran, akionyesha matumaini kuhusu mazungumzo kati ya Tehran na Washington, na akasisitiza: “Eneo hili haliwezi kuvumilia vita vingine.

    Rais Erdogan anafuatilia kwa karibu suala hili, na juhudi zetu zote zinalenga kuzuia mzozo wa kijeshi.”

    Akijibu swali la mtangazaji wa kituo hicho kuhusu maandamano na mauaji makubwa ya Januari pamoja na madai ya mabadiliko ya utawala, Bw. Fidan alisema kuwa kwa maoni yake, serikali ya Iran “haitaangushwa kwa shambulio la anga, bali mfumo utadhoofishwa na huenda usiwe tena na uwezo wa kutekeleza majukumu yake… na udhaifu huu utailazimisha serikali kubadili mwelekeo wake kwa misingi.”

    Katika sehemu nyingine ya mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alizungumzia simu aliyopokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, wakati wa vita vya siku 12 kati ya Iran na Israel, na jinsi Bw. Rubio alimfahamisha kuhusu shambulio lililokuwa likitarajiwa dhidi ya Iran, naye akaijulisha haraka mwenzake wa Iran kuhusu jambo hilo.

    Soma zaidi:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ya tarehe 10/02 2026, tutakufahamisha yanayochipuka Afrika Mashariki na Kimataifa.