Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah
Taarifa kutoka wizara ya afya ya Lebanon zinasema kuwa watu 182 wameuawa na wengine 727 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, wanawake na wahudumu wa afya katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon yaliyoanza asubuhi ya leo.
Muhtasari
Katika picha: Maelfu wakimbia huku Israel ikizidisha mashambulizi Lebanon
Tazama: Moshi ukifuka kusini mwa Lebanon baada ya mashambulizi ya Israel
Israel inakabiliwa na siku ngumu zijazo, asema Netanyahu
Watoto 21 wuawa Lebanon katika mashambulio ya Israel huku idadi ya vifo ikifikia 274
Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah
Viongozi wa Chadema miongoni mwa watu 14 wanaotuhumiwa na polisi Tanzania kwa maandamano yaliyopigwa marufuku
Mke wa kiongozi wa upinzani Tanzania Freeman Mbowe na bintie waachiliwa huru
Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kupinga tabia ya Naibu wa Rais
Tazama: Hali ilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam katika siku ambapo upinzani ulikuwa umepanga maandamano
Tazama: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alivyokamatwa
Lebanon yawaonya wakazi wa Kusini kwa ujumbe wa simu kuepuka maeneo ya Hezbollah yanayolengwa
Polisi yathibitisha kuwakamata viongozi wa Chadema na wengineo
IDF kutekeleza mashambulizi 'makubwa na kwa usahihi' zaidi nchini Lebanon
Kwa Picha: Hali ilivyo katika mji wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akamatwa
Polisi watanda Dar es Salaam kuelekea maandamano ya Chadema
Sri Lanka yamuapisha rais mpya anayeegemea mrengo wa kushoto
Watu sita wafariki dunia baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko Japan
Zelensky kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwa Biden, Harris na Trump
Kocha wa Arsenal asema sare na Man City ni 'muujiza'
Italia: Watu wanne wa familia moja wafariki dunia katika mlipuko wa gesi
Trump asema hatagombea tena ikiwa atashindwa katika uchaguzi wa Novemba
Moja kwa moja
Na Asha Juma & Dinah Gahamanyi
Kocha wa Arsenal asema sare na Man City ni 'muujiza'
Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ni
"muujiza" timu yake kukaribia ushindi baada ya kucheza kipindi cha
pili na wachezaji 10 katika mechi ya Ligi Kuu England.
"Ni muujiza tulicheza dakika 56 pale Etihad tukiwa
na wachezaji 10," alisema Arteta. "Siamini tulichokifanya."
Bao la kusawazisha la John Stones wa Manchester City
katika dakika ya 98 liliinyima Arsenal ushindi muhimu dhidi ya mabingwa hao
watetezi.
Baada ya winga wao Leandro Trossard kutolewa kwa kadi
nyekundu katika muda wa majeruhi wa kipindi cha kwanza, The Gunners walimiliki
mpira kwa asilimia 12.5 pekee katika kipindi cha pili.
Arsenal walikuwa wamebakia na sekunde chache kabla ya
kuwa timu ya kwanza ya ugenini kushinda katika uwanja wa Etihad tangu Brentford
mwezi Novemba 2022.
Italia: Watu wanne wa familia moja wafariki dunia katika mlipuko wa gesi
Chanzo cha picha, Vigili del Fuoco
Watu wanne wa familia moja wakiwemo watoto wawili
wamefariki katika mlipuko wa gesi kusini mwa Italia.
Nyumba yao ya ghorofa mbili katika mji wa Saviano, karibu
na Naples, iliporomoka kwa kiasi fulani katika mlipuko huo, na kuwaua ndugu -
mvulana na msichana - pamoja na mama na bibi yao.
Baba na mtoto mchanga walipatikana kutoka kwenye vifusi
wakiwa hai, wazima moto wa Italia walisema.
Bado yuko hospitalini huko Naples akiwa katika hali
mbaya, wakati majeraha ya mtoto sio ya kutishia maisha, vyombo vya habari vya
ndani viliripoti.
Idara ya zimamoto ya Vigili del Fuoco, Italia, iliripoti
kwamba wazazi na watoto watatu waliishi kwenye ghorofa moja ya nyumba hiyo,
wakati mwanamke mwingine - anayesemekana kuwa bibi - aliishi kwenye ghorofa ya
juu.
"Wazima moto waliwaokoa baba na mtoto mchanga wakiwa
hai, na kuwakabidhi chini ya uangalizi wa wafanyikazi wa afya mahali hapo,
wakati hawakuweza kufanya chochote kwa watoto wawili, mvulana na msichana,
ambao kwa bahati mbaya miili yao ilitolewa wakiwa washafariki dunia," Idara
ya zimamoto ilisema katika taarifa.
Ingawa mamlaka haijathibitisha umri wa watoto hao, vyombo
vya habari vya ndani viliripoti kwamba walikuwa wa miaka minne na sita.
Wazima moto waliwapata watoto na baba asubuhi, kisha ikawachukua
siku nzima kutafuta kwenye vifusi, na hawakumpata mama huyo hadi saa 16:45.
Vikosi vya utafutaji na uokoaji, vinavyofanya kazi na
mbwa wa kunusa, viliendelea na utafutaji wa bibi huyo hadi usiku, na kutangaza
kuwa wamempata na walikuwa wamemaliza shughuli hiyo kufikia saa 01:00.
Uchunguzi
unaendelea kubaini chanzo hasa cha kuporomoka kwa jengo hilo, lakini nadharia
za awali zinaonyesha kuwa nyumba hiyo ilianguka baada ya mlipuko wa gesi.
Trump asema hatagombea tena ikiwa atashindwa katika uchaguzi wa Novemba
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa zamani Donald Trump amesema hatarajii kugombea
tena uchaguzi mwaka 2028 iwapo atashindwa katika uchaguzi wa urais wa Marekani
utakaofanyika Novemba mwaka huu.
Trump, mwenye umri wa miaka 78, amekuwa mgombea wa chama
cha Republican kwa chaguzi tatu za kitaifa mfululizo na amekijenga upya chama
hicho kwa miaka minane iliyopita.
Katika mahojiano na Sinclair Media Group, aliulizwa kama
anaweza kujiona akiwania tena urais iwapo atashindwa na Makamu wa Rais wa chama
cha Democratic Kamala Harris.
"Sioni
hilo hata kidogo." Lakini aliongeza kuwa "natumai, tutakuwa na mafanikio
makubwa".
Sheria za Marekani zinawazuia marais kuhudumu kwa zaidi
ya mihula miwili, na hivyo Trump hatarajiwi kugombea mwaka 2028 iwapo atashinda
pia.
Katika siku za nyuma, tajiri huyo mmiliki wa majengo ni
mara chache sana amekubali uwezekano wa kushindwa katika uchaguzi, mara nyingi
zaidi akiwachochea wafuasi wake kwa hotuba na jumbe za kwenye mitandao ya
kijamii akiahidi ushindi katika uchaguzi.
Lakini hii ni mara ya pili ndani ya siku nne ametaja kuwa
pia anaweza kushindwa.