Zaidi ya wanajeshi 750 wa Marekani wamejeruhiwa katika vita vya Iran
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa au kujeruhiwa katika vita vya Iran imefikia 774, baada ya wizara ya ulinzi kuongeza idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa hivi karibuni.
Kulingana na mfumo wa wizara ya ulinzi wa kurekodi majeruhi, kufikia sasa wanajeshi 18 wa Marekani wameuawa na wengine 756 kujeruhiwa katika vita vya Iran na Marekani.
Usitishaji mapigano kati ya Marekani na Iran ulikamilika siku ya Jumatatu na muda huo haujaongezwa, ila hakuna upande ambao umetekeleza oparesheni yoyote kubwa ya kijeshi.
Soma pia: