Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Iran: Tutashambulia "Ukanda wa Gaza"

Jeshi la Iran IRGC limesema katika taarifa kwamba Israel "imevuka mipaka yote myekundu katika mauaji ya halaiki na kuendelea kwa mchakato huu sio jambo la kustahimili."

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma & Mariam Mjahid

  1. Ndege ya jeshi yaanguka Colombia na kuua watu 66

    Watu wasiopungua 66 wamefariki dunia baada ya ndege ya Jeshi la Anga la Colombia iliyokuwa imebeba watu 128 kuanguka Jumatatu katika eneo la Puerto Leguízamo, mkoa wa Putumayo, kusini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Peru.

    Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Anga, Carlos Fernando Silva Rueda, kulikuwa na watu 128 wakiwemo wanajeshi, na wafanyakazi ndani ya ndege aina ya C-130 Hercules wakati wa ajali hiyo.

    Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa kuwa watu wasiopungua 66 wamefariki, huku watu wanne hawajulikani walipo, idadi iliyothibitishwa pia na vyanzo viwili vya kijeshi. Gavana wa mkoa wa Putumayo, Jhon Gabriel Molina, naye alithibitisha idadi hiyo.

    Hata hivyo, wakati mamlaka zikisubiri takwimu rasmi, chanzo cha jeshi kililiambia BBC Mundo kuwa ripoti ya hivi karibuni inaonyesha vifo vinaweza kufikia 44, na huenda idadi hiyo ikaongezeka.

    Kabla ya kutolewa kwa takwimu hizo mpya, Rais wa Colombia, Gustavo Petro, alisema kuwa wanajeshi vijana 83 walikuwa bado hai wakati huo.

    Waziri wa Ulinzi, Pedro Sánchez, alisema ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kupaa, ikidondoka takriban kilomita 1.5 kutoka uwanja wa ndege ilikotoka.

    Aliongeza kuwa watu kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, na kwamba taarifa kamili kuhusu waliojeruhiwa na waliopoteza maisha itatolewa mara tu itakapothibitishwa rasmi.

    Awali, waziri huyo alithibitisha kuwa taratibu zote za kuwasaidia waathiriwa na familia zao zimeanzishwa, pamoja na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo.

    Soma zaidi:

  2. Trump aipa Iran 'nafasi ya mwisho' ya mazungumzo ya amani

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Iran ina “nafasi moja zaidi” ya kufikia amani, huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu uwepo wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

    Kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Trump alidai kuwa Marekani na Iran zimekuwa na mazungumzo kuhusu “suluhisho kamili la kumaliza uhasama” katika eneo la Mashariki ya Kati. Aidha, alisema ameahirisha mashambulizi aliyokuwa ametishia kuyafanya dhidi ya miundombinu ya nishati ya Iran kwa muda wa siku tano.

    Hatua hiyo ilichangia kushuka mara moja kwa bei za mafuta na gesi katika masoko ya dunia.

    Hata hivyo, Iran imekanusha vikali madai hayo. Spika wa Bunge la nchi hiyo, Mohammad-Bagher Ghalibaf, amesema hakuna mazungumzo yaliyofanyika na kudai kuwa taarifa hizo ni “habari za uongo” zinazolenga kuathiri na kudanganya soko la mafuta.

    Pamoja na msimamo huo wa Iran, afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo amenukuliwa akisema kuwa wamepokea mapendekezo kutoka Marekani kupitia wapatanishi, na kwamba yanapitiwa. Hata hivyo, alisisitiza kuwa hatua hiyo ni maandalizi ya awali na si uthibitisho wa mazungumzo rasmi yanayoendelea.

    Ripoti mbalimbali zimeendelea kutofautiana kuhusu suala hilo. Baadhi ya vyanzo kutoka Marekani vinadai kuwa mazungumzo yalifanyika kwa njia isiyo ya moja kwa moja yakiwahusisha wajumbe wa karibu wa Trump, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa nchi kama Misri, Uturuki na Pakistan zilihusika kama wapatanishi.

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameunga mkono uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano, akisema hatua hiyo inaweza kusaidia kufanikisha malengo ya operesheni ya pamoja kati ya Marekani na Israel.

    Hali hii inajiri wakati mvutano katika eneo hilo ukiendelea kuongezeka, hasa baada ya mashambulizi kulenga pia miundombinu ya kiuchumi kama vituo vya gesi. Wataalamu wanasema hatua hiyo imeongeza hofu kuhusu usalama wa nishati na uthabiti wa uchumi wa kimataifa.

  3. Hujambo. Karibu katika matangazo yetu mubashara tarehe ni 24/03.2026.