Waziri Mkuu wa Bangladesh ajiuzulu na kutoroka nchi huku waandamanaji wakivamia ikulu

Waziri Mkuu Sheikh Hasina wa Bangladesh amejiuzulu, mwandishi wa BBC nchini humo amethibitisha.

Muhtasari

  • Olimpiki 2024:Biles asalia na fedha huku Andrade akishinda dhahabu
  • Marekani hatimaye yaondoa wanajeshi wake nchini Niger
  • Je, mkuu wa jeshi la Bangladesh aliyetangaza kujiuzulu kwa Sheikh Hasina ni nani?
  • Katika Picha: Sherehe na uporaji katika mitaa ya Dhaka
  • Amesikitika sana, asema mtoto wa Hasina
  • Wito kwa wageni kuondoka Lebanon huku hofu ya vita ikiongezeka
  • Mbappe kujiunga na Real hakutaathiri nafasi Bellingham - Ancelotti
  • Kwanini Hasina amekimbilia India?
  • Umati wa 'washangilia' mjini Dhaka
  • Serikali ya mpito kuundwa Bangladesh - Mkuu wa jeshi
  • Bangladesh: Matukio ya hivi punde kwa ufupi
  • Bangladesh: Waandamanaji wapora makazi rasmi ya Waziri Mkuu
  • Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ajiuzulu
  • Takribani watu 90 wauawa katika maandamano ya kuipinga serikali Bangladesh
  • Waandamanaji wa Bangladesh wamtaka Waziri Mkuu aondoke madarakani
  • Wageni watakiwa kuondoka Lebanon haraka wakati hofu ya vita ikiongezeka
  • Wazambia waomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za injili makanisani na vilabuni
  • Washington yawaambia washirika kwamba shambulio la Iran "linaweza kuanza ndani saa 24 hadi 48"
  • Wagner: Mali yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine

Moja kwa moja

Lizzy Masinga & Ambia Hirsi

  1. Wageni watakiwa kuondoka Lebanon haraka wakati hofu ya vita ikiongezeka

    Hezbollah na Israel zilirushiana risasi asubuhi ya Jumapili

    Chanzo cha picha, EPA

    Nchi kadhaa zimewataka raia wao kuondoka Lebanon, huku hofu ikiongezeka ya mzozo mkubwa katika Mashariki ya Kati.

    Iran imeapa kulipiza kisasi "kikali" dhidi ya Israel, baada ya kifo cha mkuu wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh huko Tehran siku ya Jumatano.

    Israel haijasema chochote.

    Mauaji yake yalikuja saa chache baada ya Israel kumuua kamanda mkuu wa Hezbollah Fuad Shukr huko Beirut.

    Maafisa wa nchi za Magharibi wanahofia kwamba Hezbollah, wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran na vuguvugu la kisiasa lenye makao yake makuu nchini Lebanon, linaweza kuwa na jukumu muhimu katika ulipizaji kisasi wa aina hiyo, ambao nao unaweza kuibua shambulio kali la Israel.

    Juhudi za kidiplomasia za Marekani na nchi nyingine za Magharibi zinaendelea kujaribu kupunguza mvutano katika eneo hilo.

    Idadi inayoongezeka ya safari za ndege zimekatishwa au kusimamishwa katika uwanja wa ndege pekee wa kibiashara huko Beirut.

    Marekani, Uingereza, Australia, Ufaransa, Canada, Korea Kusini, Saudi Arabia, Japan, Uturuki na Jordan ni miongoni mwa nchi zilizowataka raia wao kuondoka Lebanon haraka iwezekanavyo.

    Hofu ya kuongezeka kwa uhasama ambao unaweza kuikumba Lebanon ni kubwa zaidi tangu Hezbollah ilipoanza mashambulizi yake dhidi ya Israel, siku moja baada ya mashambulizi mabaya ya Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.

    Unaweza kusoma;

  2. Wazambia waomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za injili makanisani na vilabuni

    Matthew Ngosa

    Chanzo cha picha, Ngosa family

    Baadhi ya wanamuziki wakubwa nchini Zambia wametumbuiza katika tamasha la kuomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za Injili Matthew Ngosa mwenye umri wa miaka 46, siku moja kabla ya kuzikwa kwake katika mji mkuu, Lusaka.

    Watazamaji walijiunga na kuvitangaza vibao vyake alivyovipenda sana katika kanisa la Praise Christian Centre.

    Huo ndio ulikuwa umaarufu wa baadhi ya nyimbo zake ambazo hazikupigwa tu makanisani bali pia katika vilabu vya usiku kwa kipindi cha miongo miwili.

    Ukumbi wa Lusaka ulikuwa umejaa mashabiki, marafiki, familia na maafisa wa serikali.

    Kaka yake Boyd, pia mwanamuziki, maarufu kama BJ, aliwaongoza waombolezaji.

    Matthew alianza kuimba na BJ na mdogo wake Hezron walipokuwa bado shule ya sekondari, mara nyingi wakiimba cappella.

    Walijua walitaka kufanya kazi ya muziki, matarajio ambayo rahisi katika nchi ambayo uharamia hufanya wanamuziki wengi kupata pesa kidogo kutoka kwenye muziki wao.

    Matthew na Hezron waliitwa The Ezma Brothers ndani ya kundi kubwa linalojulikana kama The Tribe Called Christians.

    Baadaye, katika Kanisa la Northmead Assemblies of God la Lusaka, Matthew alijiunga na Kwaya ya The Christ Ambassador, ambako aliboresha ujuzi wake.

    Mnamo 2004 alitoa albamu yake ya kwanza yenye mafanikio makubwa ya Umutima Wandi (Moyo Wangu), ambayo ilitawala chati za muziki.

    Nyimbo za Injili zikiwemo Ukololela na Ndakunkula zilifuata , hizo mbili pia zikawa nyimbo za kutumbuiza kwenye vilabu.

    Matthew Ngosa hakuwahi kutajirika, lakini aliweza kujikimu kimaisha kutokana na vibao vyake kabla ya kugundulika kuwa na saratani ya ini mwezi Januari.

  3. Washington yawaambia washirika kwamba shambulio la Iran "linaweza kuanza ndani saa 24 hadi 48"

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewaambia viongozi wenzake wa G7 kwamba Washington inaamini kwamba mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yanaweza kuanza ndani ya saa 24 hadi 48 zijazo, Axios iliripoti, ikinukuu vyanzo vinavyofahamu wito huo.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Blinken alizungumza na wenzake huku kukiwa na juhudi za Marekani za kutuliza hali ya wasiwasi katika eneo hilo na kuzuia vita.

    Kwa kuwa Marekani inaamini kuwa shambulio la Iran haliwezi kuepukika baada ya kuuawa kwa maafisa wakuu wa Hezbollah na Hamas wiki iliyopita, Blinken aliwaambia maafisa kuhusu wito huo kwamba "kuishinikiza Tehran kupunguza mashambulizi yake ndiyo njia bora ya kuepusha vita vya kikanda."

    Blinken ameongeza kuwa Marekani haijui saa kamili ya shambulio lililopangwa la Iran, lakini inaamini kuwa linaweza kuanza mapema Jumatatu.

    Unaweza kusoma;

  4. Wagner: Mali yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine

    Mpiganaji

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mali inasema imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine, baada ya afisa wa kijeshi kusema kuwa Kyiv ilihusika katika mapigano makali karibu na mpaka wa Algeria mwezi uliopita.

    Makumi ya wanajeshi na mamluki wa Mali kutoka kundi la Wagner la Urusi waliuawa katika mapigano ya siku kadhaa na waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga na wapiganaji wanaohusishwa na al-Qaeda.

    Andriy Yusov, msemaji wa idara ya ujasusi ya jeshi la Ukraine, alisema wiki iliyopita kwamba waasi walipewa "taarifa muhimu" ili kutekeleza mashambulizi hayo.

    Afisa wa ngazi ya juu wa Mali, Kanali Abdoulaye Maiga, amesema serikali yake ilishtushwa kusikia madai hayo na kuishutumu Ukraine kwa kukiuka mamlaka ya Mali.

    Matamshi ya Yusov "yalieleza kuhusika kwa Ukraine katika shambulio la kuogofya, la kisaliti na la kinyama la makundi ya kigaidi yenye silaha" ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wa Mali, ilisema taarifa ya Kanali Maiga.

    Mali imeamua kuvunja uhusiano "ikiwa ni hatua ya haraka", alisema.

    Wiki iliyopita, jeshi la Mali lilikiri kuwa limepata hasara "kubwa" wakati wa mapigano ya siku kadhaa ambayo yalizuka tarehe 25 Julai.

    Mapigano hayo yametokea katika jangwa karibu na Tinzaouaten, mji wa kaskazini-mashariki kwenye mpaka na Algeria.

    Ripoti zinasema kuwa wanajeshi hao wa Mali na Urusi walishambuliwa na waasi wa Tuareg na wapiganaji wa kundi tanzu la al-Qaeda, Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin wakati wakisubiri kuongezwa nguvu, baada ya kuondoka Tinzaouaten.

    Si wanajeshi wa Mali wala Wagner, ambao tangu wakati huo wamejiunga na kundi linaloitwa Africa Corps, ambao wametoa takwimu kamili, lakini makadirio ya vifo vya wapiganaji wa Wagner ni kati ya 20 hadi 80.

    Unaweza kusoma;

  5. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu