Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Iran yaapa kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Haniyeh

Rais wa Irani Masoud Pezeshkian anasema ataifanya Israel "ijutie" mauaji ya "uoga" ya Haniyeh, akiongeza kuwa Iran "italinda uadilifu wa eneo lake, fahari ya heshima na utu".

Muhtasari

  • Ukraine yazima shambulio 'kubwa' la ndege zisizo na rubani za Urusi
  • Iran yaapa kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Haniyeh
  • Nani anaweza kuchukua nafasi ya Haniyeh?
  • Nyimbo za hasira huku Wapalestina wakiandamana baada ya kifo cha Haniyeh
  • Timu za dharura zafanya msako kwenye vifusi kumtafuta kamanda wa Hezbollah
  • DRC na Rwanda wakubaliana kuhusu amani
  • Vita vya Ukraine: Urusi yadundua droni 19 za Ukraine
  • Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan anusurika katika jaribio la mauaji
  • Ngedere na Bundi wavuruga usafiri wa treni ya SGR
  • Kuuawa kwa kiongozi wa Hamas kunaisongesha Mashariki ya Kati 'karibu na vita'
  • Ismail Haniyeh alikuwa nani?
  • Harris anakaribia kumchagua mgombea mwenza wake na hawa ndio wanaozingatiwa
  • Kifo cha Haniyeh 'kinaifanya dunia kuwa mahali salama' - Waziri wa Israel
  • Israel inafanya 'tathmini ya hali', asema msemaji wa jeshi
  • Mauaji ya Haniyeh 'hayatapita bila kulipizwa kisasi' - afisa wa Hamas
  • Mauaji ya Ismail Haniyeh: Tunachojua kufikia sasa
  • 'Israel ilimuua Ismail Haniyeh kwa shambulizi la anga'-Hamas
  • Viongozi wengine wa Hamas ni akina nani?
  • Iran yasema inachunguza kifo cha Haniyeh
  • Maandamano yaendelea Venezuela huku hasira ikiongezeka kwa matokeo ya uchaguzi yenye utata
  • Israel yadai kumuua kamanda mkuu wa Hezbollah katika shambulizi la Beirut

Moja kwa moja

Na Asha Juma ,Yusuf Jumah & Dinah Gahamanyi

  1. Maandamano yaendelea Venezuela huku hasira ikiongezeka kwa matokeo ya uchaguzi yenye utata

    Maandamano yaendelea katika mji mkuu wa Venezuela Caracas baada ya matokeo yenye utata ya uchaguzi wa rais nchini humo.

    Maelfu ya watu walikusanyika katikati mwa jiji ili kuonyesha upinzani wao dhidi ya madai ya ushindi wa Rais Nicolas Maduro.

    Wengi walisema hawatakoma hadi kuwe na serikali mpya, na wengine walisema hili litaafikiwa tu ikiwa vikosi vya usalama vitaungana na waandamanaji wa upinzani.

    Hata hivyo wanajeshi na polisi hadi sasa wamesalia watiifu kwa Bw Maduro na wamewafyatulia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira baadhi ya waandamanaji.

    Maafisa wa eneo hilo wanasema karibu watu 750 wamekamatwa. Mashirika mawili maarufu yasiyo ya kiserikali nchini humo yanasema watu kadhaa wamefariki dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa.

    Siku ya Jumanne waziri wa ulinzi wa Venezuela alielezea maandamano hayo kama "mapinduzi".

    Akiwa amezungukwa na wanajeshi wenye silaha, Jenerali Vladimir Padrino alisoma taarifa akisema kwamba "uaminifu" kwa Rais Nicolás Maduro uko imara "na uungwaji mkono usio na masharti" wa jeshi

    Mwanasheria mkuu wa Venezuela, ambaye ni mshirika wa karibu wa Bw Maduro, alisema mwanajeshi mmoja aliuawa katika maandamano ya kuipinga serikali.

    Kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado alitaka maandamano yawe ya amani.

    "Lazima tuendelee kwa njia ya amani. Hatupaswi kutumbukia katika chokochoko ambazo serikali imetulenga. Wanataka kuwafanya Wavenezuela wakabiliane dhidi yao," alisema.

    "Mgombea wetu alipata 70% ya kura. Tuliunganisha nchi, Wavenezuela ambao wakati fulani walimwamini Maduro wako nasi leo."

    Mwandamanaji mmoja anayeipinga serikali ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliambia BBC kwamba wameona ushahidi wa udanganyifu katika uchaguzi.

    Soma zaidi:

  2. Israel yadai kumuua kamanda mkuu wa Hezbollah katika shambulizi la Beirut

    Israeli inasema imemuua kamanda mkuu wa Hezbollah baada ya kufanya shambulizi katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

    Takriban mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea Dahiyeh, ngome ya kundi la waasi la Lebanon.

    Jeshi la Israeli linasema kuwa Fuad Shukr alikuwa akilengwa "kumalizwa kijasusi" na ndege za kivita.

    Maafisa wanasema alihusika na shambulio la roketi kwenye eneo la Milima ya Golan linalokaliwa na Israeli siku ya Jumamosi ambalo liliua watu 12, wengi wao wakiwa watoto. Hata hivyo, Hezbollah imekanusha kuhusika na shambulio hilo.

    Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati alilaani "uchokozi wa wazi wa Israel".

    Alieleza kuwa ni "kitendo cha uhalifu" katika "msururu wa operesheni kali zinazoua raia katika ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa."

    Katika ujumbe uliwekwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya shambulio hilo, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema: "Hezbollah ilivuka mstari mwekundu".

    Bado haijabainika iwapo Fuad Shukr aliuawa katika shambulio hilo. Vyanzo vya usalama mjini Beirut vinasema lengo lililokusudiwa halikuwa katika jengo hilo.

    Hezbollah bado haijatoa tamko lolote.

    Afisa mmoja wa Israeli ameithibitishia CBS News, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba Israeli ilitoa notisi kwa Marekani kuhusu shambulizi lake la Beirut.

    Tazama kilichotokea baada ya mlipuko

    Soma zaidi:

  3. Bila shaka uko salama msomaji wetu, karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 31/07/2024