Jenin: Vikosi vya Israel vyaanza kuondoka baada ya operesheni ya siku mbili
Vikosi vya Israel vimeanza kuondoka katika kambi ya wakimbizi ya Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, chanzo cha ulinzi kinasema.
Hii inahitimisha operesheni kubwa ya siku mbili ambapo Wapalestina 12 na mwanajeshi mmoja wa Israel wameuawa.
Milio ya risasi na milipuko viliweza kusikika katika kambi ya Jenin wakati habari zilipoibuka Jumanne jioni.
Jeshi la Israel lilisema baadaye kuwa lilinasa makombora matano yaliyorushwa kuelekea kusini mwa Israel na wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Hakuna kundi lililodai mara moja kwamba lilihusika na mashambulio.
Wakati Waisraeli wakiendelea kuondoka Jenin, maafisa wa afya wa Palestina waliripoti kwamba mwanamume mmoja wa Kipalestina aliuawa na vikosi vya Israeli. Ilisema alikuwa kifo cha 12 cha Wapalestina katika mji huo tangu Jumatatu.
Unaweza pia kusoma:
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Mzozo wa Israel na Palestina: Je kuwa na taifa moja ndio suluhisho?