Waziri Mkuu wa Sri Lanka alitaka jeshi 'kurejesha utulivu’
Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ametoa hotuba ya televisheni ambapo ameliamuru jeshi "kufanya kila liwezekanal kurejesha utulivu".
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Raheem Sterling athibitisha kujiunga na Chelsea
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Sterling amefunga mabao 10 au zaidi ya Ligi ya Primia katika misimu mitano iliyopita ya ligi hiyo.
Raheem Sterling amethibitisha kuondoka kwake Manchester City na kusema kuwa anaondoka katika klabu hiyo kama "mwanaume".
Uhamisho wa pauni milioni 50 wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwenda kwa wapinzani wa Ligi ya Primia Chelsea unatarajiwa katika saa 24 zijazo.
"Nilifika Manchester nikiwa na umri wa miaka 20. Leo, naondoka kama mwanaume," alisema Sterling.
"Misimu saba, makombe 11 makuu, kumbukumbu za maisha."
City ilimsajili Sterling kutoka Liverpool kwa mkataba wa £49m mwaka wa 2015. Alifunga mabao 131 katika mechi 339, akishinda mataji manne ya Ligi ya Primia.
Sterling atakuwa mchezaji wa kwanza mkubwa kusajiliwa na Chelsea tangu iliponunuliwa na Todd Boehly.
Aliongeza: "Ninashukuru kwa panda shuka nilizikumbana nazo, kwani ni kushuka kumejaribu nguvu na azimio langu na kuniwezesha kusimama hapa mbele yako kama mchezaji bora zaidi."
Sterling sasa ataungana na kikosi cha Chelsea kilichoondoka kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani siku ya Jumamosi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Kukumiwa ya gavana wa zamani wa Rwanda yapokelewa kwa furaha na manusura wa mauaji ya kimbari
Chanzo cha picha, AFP
Shirika kuu la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda
limeipokea hukumu ya miaka 20 jela iliyotolewa na mahakama ya Ufaransa kwa
gavana wa zamani kutoka kusini mwa Rwanda.
Mahakama ya mjini Paris ilimkuta Laurent Bucyibaruta, 78, na
hatia ya kuhusika katika mauaji ya kimbari ya 1994. Anaweza kukata rufaa kwa
hukumu hiyo.
Wakati wa kesi hiyo, iliyoanza mwezi wa Mei, ushahidi
ulisikika kuhusu jinsi gavana wa jimbo la lililokuwa Gikongoro, Bucyibaruta alishawishi
makumi ya maelfu ya Watutsi kukimbilia katika Shule ya Ufundi ya Murambi,
ambako waliuawa siku chache baadaye.
Egide Nkuranga, mkuu wa Ibuka - ambayo ina maana
"Kumbuka" kwa Kinyarwanda aliiambia BBC Maziwa Makuu kuwa taasisi hiyo
imeipokeaa hukumu hiyo na wameifurahia "kesi hiyo ilivyofanyika".
Waendesha mashtaka wa Ufaransa na mashirika kadhaa, ikiwa ni
pamoja na tawi la Ufaransa la Ibuka, walileta mashtaka dhidi ya Bucyibaruta.
Urefu wa kifungo chake umekuja kwa kuwa ukweli ni kwamba alikuwa
amekutwa na hatia, Bw Nkuranga alisema.
"Tulifikiri kwa sababu ya mashtaka dhidi yake kwamba
anaweza kupata kifungo cha maisha, lakini hakuna tatizo hata kwa miaka
20," alisema.
Ukumbusho umewekwa pale ambapo Shule ya Ufundi ya Murambi
iliwahi kuwepo. Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani
waliuawa katika muda wa siku 100 wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Papa Francis ateua wanawake watatu katika jopo linalowachagua maaskofu
Chanzo cha picha, Getty Images
Mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis ameteua wanawake
wawili kuwa watawa na Mlei mmoja wa kike
kuwa katika kamati ya awali ya wanaume wote ambayo humshauri katika kuchagua
maaskofu.
Mapema mwezi huu,
Papa alisema anataka kuwapa wanawake vyeo vya juu zaidi katika jopo la Holy
See.
Wanawake watatu
ambao sasa wameteuliwa katika “Dicastery for Bishops” ya Vatican watachunguza
rekodi za wanaotaka kuwa maaskofu na kisha kumshauri Papa ni nani anafaa
kuchaguliwa.
Katika kanisa
katoliki wanawake bado hawawezi kuwa maaskofu, wala hata makasisi, lakini Papa
Francis alisema atakuwa wazi kwa wanawake wanaoongoza idara yoyote ya Vatican.
Wanawake hao
watatu ni sister Raffaella Petrini, ambaye kwa sasa ni naibu gavana wa Jiji la
Vatican, mtawa raia wa Ufaransa Yvonne Reungoat na Maria Lia Zervino,
anayeongoza chama cha mashirika ya Kikatoliki ya wanawake, UMOFC.
‘Usiwe kijana wa madhabahu ya Putin’ - Ukosoaji usio wa kawaida wa Papa Francis kwa Patriaki Cyril kwa msaada wake kwa vita vya Ukraine
Papa Francis: Sheria mpya za Vatican zatoa adhabu kali kwa wanyanyasaji wa kingono
Diverticular: Fahamu maradhi hatari ya utumbo yaliomlazimu Papa Francis kufanyiwa upasuaji
Habari za hivi punde, Waziri Mkuu wa Sri Lanka alitaka jeshi 'kurejesha utulivu’
Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ametoa hotuba ya
televisheni ambapo ameliamuru jeshi "kufanya kila liwezekanal kurejesha
utulivu".
Amewatolea wito waandamanaji waliovamia ofisi yake na majengo mengine
waondoke na waonyeshe ushirikiano na mamlaka.
"Hatuwezi kukiuka
katiba yetu. Hatuwezi kuwaruhusu mafashisti kuchukua nchi. Lazima tumalize tisho
hili la ufashistila demokrasia ," aliongeza.
Mwandishi wa BBC mjini
Colombo anasema tangazo la hivi karibuni la Bw Wickremesinghe linaweza kuwa linaashiria
kwamba jeshi linakaribia kuimarisha usalama katika mji huo mkuu.
Unaweza pia kusoma:
Sri Lanka: Rais Gotabaya Rajapaksa akimbia nchi kwa ndege ya kijeshi
Madhila ya kila siku ya kuishi katika nchi iliyofilisika
Sri Lanka: Nyumba ya Waziri mkuu wa Ranil Wickremesinghe imechomwa moto
Mkanda maarufu wa ndondi uliotolewa kwa Mandela waibiwa
Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi wa Afrika Kusini wameanzisha msako wa kuwasaka washukiwa walioiba mkanda wa ndondi uliotolewa kwa Nelson Mandela na bingwa wa Marekani Sugar Ray Leonard.
Mkanda wa bingwa wa dunia, wenye thamani ya takriban $3,000 (£2,500), ulikuwa umewekwa kwenye jumba la makumbusho la Mandela House huko Soweto.
Msemaji wa polisi Kanali Dimakatso Sello aliambia BBC kwamba kesi ya wizi iliwasilishwa kwa polisi tarehe 2 Julai.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi walioripoti kazini katika jumba maarufu la makumbusho la mtaa wa Vilakazi, ambako mwanasiasa huyo aliyepinga ubaguzi wa rangi aliishi kati ya 1946 na 1962, walibaini kuwa kufuli hizo zilivunjwa siku moja kabla.
Wakati wa uchunguzi, ilibainika kuwa ukanda huo ulikuwa umechukuliwa.
Kwa sasa haijulikani ikiwa kuna kitu kingine chochote kiliibiwa.
Chanzo cha picha, Getty Images
Mandela, ambaye alikua rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kidemokrasia mwaka 1994 baada ya kukaa miaka 27 jela kwa kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi, alikuwa shabiki wa ndondi.
"Sikufurahia vurugu za mchezo wa ndondi. Nilivutiwa na jinsi mtu anavyosogeza mwili wake ili kujilinda, jinsi mtu anavyotumia mkakati wa kushambulia na kurudi nyuma, jinsi mtu anavyojisogeza kwenye mechi," aliandika katika kitabu cha maisha yake.
Ujenzi wa kituo cha dharura cha WHO wakumbwa na mzozo wa ardhi Kenya
Mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kujenga kituo cha dharura nchini Kenya umewekwa mashakani kutokana na mzozo wa umiliki wa ardhi.
Msimamizi mkuu wa chuo kikuu kimoja nchini Kenya amefutwa kazi kutokana na mzozo huo.
WHO na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) zilipewa ardhi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta na serikali ya Kenya.
Kituo hicho kitajumuisha kituo cha mafunzo, wataalamu wa nyumba ambao wanaweza kukabiliana na dharura ya matibabu ndani ya saa 24 za kwanza na akiba ya vifaa vya matibabu, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Serikali ya Kenya na WHO ilizindua ujenzi wa kituo hicho cha $5m (£4.2m) Jumamosi iliyopita.
Lakini Chuo Kikuu cha Kenyatta kilipinga mpango huo, kikisema ulifanywa bila idhini yake.
Rais Uhuru Kenyatta alimkosoa mkuu wa chuo hicho hadharani akisema atachukua hatua madhubuti dhidi ya wanaopinga mradi huo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Uchaguzi wa Kenya 2022: Mahakama Kuu yamuidhinisha Sonko kuwania ugavana wa Mombasa
Chanzo cha picha, SONKO/TWITTER
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko ameidhinishwa
na Mahakama Kuu kuwania kiti cha ugavana wa Mombasa kufuatia makabilianao
ya kisheria ya miezi kadhaa baada ya Tume Huru ya
Uchaguzi nchini Kenya kumzuia kushiriki uchaguzi huo.
Majaji wa mahakama hiyo pia waliagizi Tume
ya Uchaguzi kupokea makaratasi ya uteuzi wa Sonko na kumjumuisha rasmi katika
kinyang’anyiro hicho.
Majaji Olga Sewe, Ann Ong’injo’ na Stephen wamefikia
uamuzi huo siku kadhaa baada ya jina la Sonko kukosekana katika orodha ya
wawaniaji walioidhinishwa na tume hiyo kugombea kiti cha ugavana wa Mombasa.
Kupitia kwa wakili wake John Khaminwa, Sonko alidai kuwa hatua ya Tume ya Uchaguzi kumzuia haikuwa sawa, hauendani na utaratibu na kinyume cha sheria.
Sonko ni nani?
Gavana wa zamani wa jiji la Nairobi sio mgeni katika masuala yenye utata.
Maafisa wa magereza nchini Kenya hivi karibuni walimshtaki kwa kutoroka kutoka jela miaka 20 iliyopita.
Bwana Sonko amekiri hadharani kutoroka jela wakati wa mahojiano ya moja kwa moja ya runinga.
Mambo Muhimu kuhusu Mike Sonko
Alizaliwa Februari 1975
Alikuwa mbunge wa Makadara 2010-2013
Alichaguliwa seneta wa Nairobi Machi 2013
Alichaguliwa kuwa gavana wa Nairobi Agosti 2017
Serikali ilitangaza kupunguza walinzi wake hadi watano 16 Mei, 2018
Watu 230 wauawa Sudan Kusini kwenye mzozo wa mifugo
Chanzo cha picha, AFP
Mamlaka nchini Sudan Kusini zimesema zaidi ya watu 230 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita katika mapigano ya kikabila kusini mwa nchi hiyo.
Mzozo kuhusu ng'ombe na mashamba ya malisho ulitokea katika jimbo la Ikweta Mashariki kuanzia mapema mwezi huu.
Mauaji hayo yametokea katika kaunti ya Kapoeta Kaskazini ambapo jamii hasimu zilipambana kufuatia uvamizi wa mifugo katika mojawapo ya vijiji hivyo.
Waliouawa ni pamoja na chifu wa eneo hilo ambaye alipigwa risasi. Gavana wa jimbo hilo amelaani mauaji hayo na kuiomba serikali kutuma haraka vikosi vya usalama katika eneo hilo ili kusaidia kurejesha hali ya utulivu.
Ilikuja wakati Sudan Kusini inaadhimisha miaka 11 ya uhuru.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mapigano baina ya jamii ambayo yamesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.
Habari za hivi punde, Sri Lanka: Waziri Mkuu ateuliwa kuwa rais wa mpito
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda, kulingana na spika wa bunge.
Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Kaimu Rais: SpikaAfisa huyo anasema Rais Gotabaya Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka.
Hatahivyo, hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa Rajapaksa mwenyewe.
Matangazo yote katika siku za hivi karibuni yametoka kwa spika wa bunge na ofisi ya waziri mkuu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya rais ikiwa wazi, waziri mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka atakapochaguliwa rais kutoka miongoni mwa wabunge. Uchaguzi huo unapaswa kufanyika ndani ya siku 30 baada ya Rais kujiuzulu. Spika wa bunge la Sri Lanka alisema uchaguzi unaweza kufanyika Julai 20, 2022.
Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa kuhusu mzozo wa kiuchumi.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 amekimbilia Maldives.
Bingwa wa Afrika wa mita 100, Mkenya Ferdinand Omanyala 'hatihati' kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia
Chanzo cha picha, Getty Images
Bingwa wa Afrika wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala ni
miongoni mwa wanariadha sita wa Timu ya Kenya ambao mpaka tunachapisha taarifa hii walikuwa hawajapata hati za kusafiria kwenda kushiriki Mashindano ya Riadha ya Dunia yanayotarajiwa kuanza Ijumaa huko Oregon, Marekani.
Wakati ambapo timu hiyo ya wanariadha wa Kenya ilikua ikipokea
bendera ya taifa kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi, kwa ajili ya safari hiyo, wasimamizi wa timu hiyo walikuwa na shughuli nyingi kandokando wakitafuta
usaidizi kutoka kwa Waziri wa Michezo Amina Mohamed kupata hati (visa) hizo.
Timu hiyo ilipangiwa kuondoka nchini kwa makundi mawili siku
ya Jumatatu na Jumanne.
Kundi la kwanza la wanariadha 23 lililojumuisha wanariadha
19 liliondoka nchini kwa kutumia ndege tatu tofauti za Qatar Airways, KLM Royal
Dutch Airlines na Lufthansa Airlines.
Hata hivyo, Omanyala, meneja wa kikosi hicho Rono Bunei na
madaktari wote watatu wa timu ya Kenya hawakuwa wamepata hati za kusafiria kama
ilivyotarajiwa hatua iliowakosesha safari yao ya ndege.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Omanyala (kushoto), katika moja ya mashindano ya kimataifa alizowahi kushiriki
Daktari wa timu Victor Bargoria pia alitakiwa kuondoka
katika kundi la pili Jumanne jioni.
Bwawa Bunei alisema suala la visa lilikuwa likishughulikiwa
hata wakati walipoenda kupokea bendera ya taifa katika Ikulu.
Alisema kuwa itakuwa vigumu kwa Omanyala kujiandaa na mbio
zake hivi sasa kwani hatakuwa Oregon mapema kama ilivyopangwa
awali.
Omanyala anayeshikilia rekodi ya mita 100 barani
Afrika anatarajiwa kushiriki katika awamu ya kufuzu kwa fainali ya mbio hizo
siku ya Ijumaa kabla ya fanaili kufanyika siku ya Jumamosi.
Hali ya hatari yatangazwa Sri Lanka wananchi wakitaka Rais Rajapaksa na kaka yake, rais wa zamani Mahinda 'watiwe ndani'
Chanzo cha picha, re
Siku moja baada ya Rais Gotabaya Rajapaksa kuondoka nchini humo, Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ametangaza hali ya hatari na kutangaza amri ya kutotoka nje huko magharibi, taarifa ofisi ya waziri mkuu imesema.
Huko Galle Face Green - kitovu kikuu ya maandamano ya Sri Lanka - waandamanaji wamekasirishwa kwa kitendo cha kuondoka kwa Rais wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa.
Maelfu ya waandamanaji wamepambana na polisi leo, wakiandamana kwenye ofisi ya waziri mkuu wakimtaka aondoke.
Waziri mkuu huyo alitangaza wiki iliyopita kung;atuka madarakani lakini hakusema ni lini hasa atafanya hivyo. Hali hiyo kumefanya kuwa na ombwe la uongozi, kutokana na wananchi kutomuunga mkono waziri mkuu na hata spika wanaopaswa kikatiba kushika hatamu kwa muda kutokana ukaribu wao na rais Rajapaksa.
“Hatupendi. Tunataka asalie hapa. Tunataka kurudishiwa pesa zetu! Na tunataka kuwaweka Rajapaksa wote katika gereza la wazi ambapo wanaweza kufanya kazi za mashambani,” alisema mwandamanaji GP Nimal ambaye ametumia siku 43 zilizopita kuandamana katia eneo la Galle Face Green.
"Hakuna haki," alisema.
Tulipokuwa tukizungumza, tuliunganishwa na kijana mmoja ambaye alisema alikuwa anatoka Maldives na alihamia Sri Lanka hivi majuzi.
Alipoambiwa kwamba Bw. Rajapaksa alikuwa amekimbilia Maldives, alinung'unika kwa maneno ya upole na kucheka.
"Hii ni aibu sana," alisema. "Hii sio nzuri. Hata Maldives ni kuna ufisadi na inaelekea upande uleule.”
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa (kushoto) akisalimiana na kupongezana baada kumkabidhi nyaraka kaka yake, rais wa zamani wa taifa hilo Mahinda Rajapaksa (kulia) ambaye alikuwa ametoka kuapishwa kama waziri mkuu huko Colombo, Agosti 9, 2020.
Rajapaksa ni akina nani?
Ndugu kutoka familia moja ya Rajapaksa, Mahinda na Gotabaya, walisifiwa na wengi kuwa mashujaa kwa kushinda vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini sasa wanatukanwa kama viongozi walioshindwa kusaidia Sri Lanka.
Ni anguko kubwa la neema kwa familia hiyo ambayo imetawala siasa za Sri Lanka kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mahinda Rajapaksa aliwahi kuonekana shujaa kwa kukomesha takriban miongo mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati waasi wa Tamil Tiger walipoangamizwa mwaka wa 2009 wakati wa muhula wake wa kwanza kama rais.
Baba yake alikuwa mbunge na Mahinda mwenyewe polepole alipanda kutoka kuwa kiongozi wa upinzani bungeni hadi kuwa Waziri mkuu mnamo 2004.
Alipokuwa rais mwaka mmoja baadaye, alimteua ndugu yake Gotabaya (rais wa sasa aliyekimbia nchi) kuwa waziri wa ulinzi.
Ilikuwa kazi kubwa kwa kaka mdogo huyo ambaye alikuwa akiishi maisha ya utulivu huko Marekani baada ya kustaafu jeshi la Sri Lanka.
Gotabaya alipata umaarufu, na kupata sifa ya ukatili.
Muda si muda, ndugu na jamaa wengine wakaanza kupewa nafasi na kujiunga na serikali. Sasa wananchi wanaoandamana wanataka ndugu wote wa familia ya Rajapaksa wakamatwe na waswekwe ndani kwa shutuma za kujilimbikizia mali na kuwaaacha wananchi kuwa na hali mbaya kutokana na mdororo wa kiuchumi.
'Ujumbe wa twitter wa Trump chanzo cha ghasia za uvamizi wa bunge Marekani' - Uchunguzi wa Bunge
Chanzo cha picha, Reuters
Ujumbe wa Twitter wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ulihamasisha watu wenye itikadi kali za mrengo wa kulia kukusanyika Washington DC siku ya ghasia za uvamizi wa jengo la bunge, Capitol mwaka jana, uchunguzi wa bunge umeeleza.
Aliandikaujumbe huo baada ya "mkutano wenye vibweka zaidi katika utawala wa urais wa Trump", alisema mbunge kwenye jopo la uchunguzi.
Rais huyo wa zamani wa Marekani aliwahamasisha wafuasi wake ingawa wasaidizi walimwambia mara kwa mara kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa 2020 uliomuingiza madarakani Joe Biden.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Askari wa bunge Harry Dunn, alikuwa mmoja wa waliojitokeza mbele uya kamati kutoa ushahidi wa ghasia za uvamizi wa bunge za Januari 6, 2021
Kamati maalumu ya uchugunguzi inamshutumu Bw. Trump kwa jaribio la mapinduzi ili kusalia mamlakani.
Wafuasi wa Donald Trump walivamia bunge kwa vurugu za tarehe 6 Januari 2021
wakati wabunge walipokutana ili kuthibitisha ushindi wa Bw Biden.
Saa chache kabla ya kusikilizwa kwa kesi
hiyo, Bw Trump, ambaye ni wa chama cha Republican, alipuuzilia mbali jopo la
Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Democratic kupitia kwenye moja
ya mitandao aake ya kijamii.
Bw. Trump - ambaye amedokeza kuwa anaweza
kugombea tena urais katika uchaguzi mkuu wa 2024 - ameelezea vikao vya kamatio
na uchunguzi wao ni kama jaribio la kuwaondoa Wamarekani kutoka kwenye
"janga" la utawala wa Kidemokrasia huku kukiwa na mfumuko wa bei.
Twitter yamshtaki Elon Musk kwa kukiuka mkataba wa ununuzi wa mtandao huo
Chanzo cha picha, Getty Images
Twitter imempeleka bilionea Elon Musk mahakamani ili kujaribu kumshurutisha kununua kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii, na kuanzisha vita vya kisheria na mtu huyo tajiri zaidi duniani.
Hatua hiyo inakuja baada ya Bw. Musk kutangaza kufuata uamuzi wake wa kuinunua Twitter kwa $44bn (£37bn) siku ya Ijumaa.
Alidai Twitter haikutoa taarifa kuhusu idadi ya akaunti feki zilizoko kwenye mtandao huo.
Twitter sasa imeiomba mahakama ya Delaware iamuru Bw Musk kukamilisha mpango wake huo wa kutoa $54.20 iliyokubaliwa kwa kila hisa ya Twitter.
Bw Musk anashutumiwa kwa "orodha ndefu" ya shutuma za ukiukaji wa makubaliano ya ununuzi wa mtandao huo, ukiukwaji ambao "umeleta doa kwenye mtandao huo wa Twitter na biashara yake".
Mwenyekiti wa Twitter Bret Taylor aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kwamba wanataka "kumwajibisha Elon Musk kutekeleza majukumu yake ya kimkataba".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Bw Musk na yeye aliandika Jumanne: "Oh kejeli lol."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Tuhuma zinasema Bw Musk amejitoa katika mpango huo kwa sababu "hautumiki tena
kwa maslahi yake binafsi". Bw Musk ndiye afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya
magari ya umeme ya Tesla.
Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza haitachukua hatua dhidi ya Mo Farah
Chanzo cha picha, Getty Images
Sir Mo Farah amesema "amefarijika" kwamba
Ofisi ya Mambo ya Ndani haitamchukulia hatua baada ya kufichua kuwa
alisafirishwa kinyume cha sheria hadi Uingereza.
Nyota huyo wa Olimpiki alifichua Jumatatu kwamba
jina lake halisi ni Hussein Abdi Kahin, lakini alipata uraia wa Uingereza chini
ya jina Mohamed Farah.
Mohamed Farah ndilo jina alilopewa na watu
waliompeleka nchini Uingereza kinyume cha sheria.
Ofisi ya Mambo ya Ndani iliiambia BBC kwamba
haitamchunguza Sir Mo.
"Inanifariji," alisema katika
mahojiano na kipindi cha Leo cha BBC Radio 4.
"Hii ni nchi yangu. Kama isingekuwa
[mwalimu wangu wa viungo] Alan na watu ambao waliniunga mkono katika utoto
wangu wote basi labda hata nisingekuwa na ujasiri wa kufanya hivi.
"Kuna watu wengi ambao nina deni la maisha
yangu kwao - haswa mke wangu, ambaye amekuwa akiniunga mkono sana katika kazi
yangu yote, na ambaye alinipa nguvu ya kuja na kuzungumza juu yake, akiniambia
ni sawa kufanya hivi."
Kisheria, serikali inaweza kuondoa uraia wa mtu
wa Uingereza ikiwa uraia wake ulipatikana kwa njia ya udanganyifu.
Lakini afisa wa Ofisi ya Mambo ya Ndani
aliiambia BBC News kwamba haitachukua hatua kuhusu uraia wa Sir Mo, kwani
inadhaniwa kuwa watoto hawashiriki upatikanaji wa uraia wao kwa udanganyifu.
Haujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja