Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Hali ilivyo Kisumu na Eldoret kabla y IEBC kutangaza mshindi

Maelezo ya video, Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Hali ilivyo kisumu na Eldoret
Iliyochapishwa

Wakenya wamekuwa wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Hata kabla ya Tume ya Uchaguzi IEBC kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya ,baadhi ya wakazi katika maeneo ya Kisumu na Eldoret ambayo ni ngome za Raila Odinga na William Ruto wamefurika barabarani kuanza kusherehekea huku wakitaka mshindi kutangazwa.

Tangu wapiga kura kupanga foleni Jumanne iliyopita na kuwachagua viongozi wao-matokeo ya nafasi nyingine tano yameshatolewa.